Ili kuweka matumizi sahihi ya maeneo kwenye miji yetu makaburi yote yakiondolewa kisha tutengeneze catacombs kama Paris au Italia

Mkuu, Tanzania ni tofauti sana na Ufaransa.
Usifananishe Tanzania ni kinchi chenye uhaba wa ardhi.
Kwa muda mrefu jiji la Dar es salaam limekuwa na utaratibu wa kuhamisha makaburi kila inapobidi na jiji hili halijapata vikwazo vya mahali pa kuhamishia maiti wetu.
Kwa kifupi kuhifadhi makaburi ni sehemu ya ibada kwa baadhi ya Dini na hasa dini za kale za Afrika.
 
Naunga mkono hoja
huko tunakoenda huo utamaduni wa kuzika hovyo utakoma. Adrhi hii haiongezeki na sisi tunazaliana kwa kasi kubwa sana. Tunahitaji Zaidi ardhi ya kuzalisha na kujenga kuliko ya kuwekea mizoga. Lazima ifike hatua tuzike kwa kubana matumizi ya ardhi. Ukishakufa kinachobaki ni mbolea.
 
Kuna wakati unakuja huko kote kutajaa makazi na watu...idadi yetu inapanda kwa kasi ya roketi mathalani mwaka 1960 watanzania tulikuwa Milioni ishirini tu...leo tuko milioni 57.31 tunakaribia 60...zingatia hiyo KASI yetu ya kuzaliana ni ndogo wakati Ethiopia tulikuwa idadi sawa mwaka 60 wao leo wako milioni 105...na kwa tangazo la mkuu wa nchi kwamba tuzaliane...idadi yetu itakua zaidi na zaidi miaka 50 ijayo......hivyo tupange sasa matumizi sahihi ya rasilimali zetu ikiwemo ardhi hasa maeneo ya mjini.

takwimu hizo ni kwa mujibu wa WB
Mkiishiwa maeneo ya kuzikia huko dar mje mzike Lindi huku, eneo kubwa la mkoa wa Lindi ni pori
 
Back
Top Bottom