Ili kuvutia uwekezaji mkubwa,umiliki wa ardhi uongezewe miaka kutoka 99,kwenda 199 mpaka 999

iparamasa

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
13,437
14,924
Sheria ya Ardhi inasema ardhi ni mali ya umma na Rais mdhamini katika umiliki huo

Sheria inasema kwamba,kwa ardhi iliyopewa hati,muda wa ukomo wa kumiliki ardhi hiyo ni miaka 99(tisini na tisa) na mmiliki wa eneo anaweza kuongezewa muda wa umiliki baada ya ule wa awali wa miaka 99 kuisha.

Pia kuna umiliki wa miaka 33 na 66

Nadhani wakati muda huu unawekwa,uwekezaji katika sekta ya Kilimo, ujenzi,viwanda na biashara haukuwa mkubwa kiasi hiki kama tunavyoshuhudia sasa

Kwa sasa tunashuhudia uwekezaji wa mamia ya mabilioni katika majengo mrefu kabisa yenye manufaa kiuchumi

Nilikuwa nawaza tu,hivi kweli uwekezaji wa bilioni mia moja,bilioni mia mbili au matrilioni kama alivyowekeza Dangote unaupatia miaka 99?

Nina maoni kwamba ili tupate wawekezaji katika maghorofa kwa ajili ya makazi ambao watashusha hata bei, na pia mabenki kuwaamini zaidi kuwakopesha,ni vizuri kuongeza muda wa umiliki hasa kwa maeneo maalum ya mijini

Hii itapunguza kasi ya miji yetu kutanuka horizontally,badala yake miji itakuwa inatanuka kwa kwenda juu kwa kutengeneza flats ambazo tutauziwa kwa unit title kwa bei rahisi.

Kwa kasi ya ukuaji wa majiji na ongezeko la idadi ya watu,sasa hivi ardhi itakwisha na ndani ya miaka kumi mapori yote yatakuwa makazi ya watu,hasa yale yaliyo pembeni ya majiji kama Dar,Arusha,Mwanza.

Tukumbuke Mungu aliumba Dunia Mara moja tu na hatarudia tena,lakini sisi kila siku tunazaana

Pia nilikuwa napendekeza kwamba hata muda wa chini kabisa kumiliki ardhi kwa kutumia hati iwe miaka 66, hii miaka 33 haiendani na hali halisi ya gharama za ujenzi,nyumba ya kawaida kabisa nzuri haipungui milioni mia moja,unaijenga kwa karibu miaka kumi,wakati mwingine unamalizia ukiwa ndani humo humo,kama hati ni ya miaka 33,basi mamilioni uliyotumia yatakuwa na faida kwa miaka 23 tu baada ya hapo unaanza kumshawishi Rais akuongezee muda wa umiliki tena,akiamua atakuongezea,akiona ulimpingapinga kwenye kampeni anakataa,hivyo kwa mujibu wa sheria,eneo hilo linarudi kumilikiwa na rais,na wewe anaweza kutimuliwa muda wowote au kuvunjiwa jengo.

Pia nilikuwa na mawazo kwamba maeneo baadhi ya mjini yawe na umiliki usio na kikomo lakini yawe na masharti ya malipo maalum(serikali ikiyahitaji kwa matumizi yake inalipa fidia) Hii sehemu nyingine wanaita FREEHOLD,mfumo wetu ni wa LEASEHOLD,leasehold ni upangaji katika ardhi,serikali inakupangisha(japo inakupa hati)na unakuwa unailipa kodi kila mwaka.

Ubunifu huu wa Freehold utaongeza mapato hasa kwa wawekezaji wakubwa,serikali anaweza kuweka tozo maalum,kubwa kidogo kwa watakaohitaji hati za namna hii. Hata katika soko,mtu anayemiliki ardhi yenye hati isiyo na ukomo akiamua kuuza atauza kwa bei nzuri au kukopeshwa benki kuliko mwenye ka hati ka miaka 33,hapa naongelea mkopo mkubwa wa kujenga apartment za kubeba maelfu ya watu. Ubunifu wa hati hizi ni sawa na ubunifu wa namba za magari zenye majina binafsi,lakini kwenye ardhi,lengo ni kuvutia uwekezaji mkubwa,na anayeomba hati hii asipewe bila kuonyesha anataka kufanya nini.

Ni wakati sasa kuondokana na mawazo ya kale ya kijamaa, hii ya hati zisizo ukomo zinaweza kuelekezwa kwenye sekta za Kilimo,mfano mawese kigoma,upandaji miti kibiashara,na mengine mengi

Pia mamlaka ya Rais kufuta hati miliki yanaweza kuangaliwa kwa jicho la kiuwekezaji na kibiashara,kwa kuwa kuna siku tutapata Rais ambaye kila akiamka anafuta hati hivyo kuleta mkanganyiko kwa mabenki yanayokopesha pamoja na dunia ya uwekezaji

Leasehold vs Freehold

Maoni yangu tu!!
 
Mimi huwa nashangaa,kwanza Mimi ni mtanzania,nimenunua kaeneo kangu nikakapima,halafu napewa hati eti inasema ntakaa hapo miaka 33,hiyo miaka ikiisha niende wapi?maana hiyo miaka ikiisha,ntakuwa sina hata haki ya fidia maana muda wangu wa kukaa hapo umekwisha.

Ni kama nchi hii tumepangishwa tu,maana mpangaji ndio hupangiwa muda wa kuishi mahali
 
Mimi huwa nashangaa,kwanza Mimi ni mtanzania,nimenunua kaeneo kangu nikakapima,halafu napewa hati eti inasema ntakaa hapo miaka 33,hiyo miaka ikiisha niende wapi?maana hiyo miaka ikiisha,ntakuwa sina hata haki ya fidia maana muda wangu wa kukaa hapo umekwisha.

Ni kama nchi hii tumepangishwa tu,maana mpangaji ndio hupangiwa muda wa kuishi mahali
Mkuu,ndio maana nikatoa maoni kwamba hata muda wa chini kabisa kumiliki kwa njia ya hati iwe miaka 66,

Na kwa maeneo maalum ya uwekezaji mfano posta, kariakoo,masaki,oyster bay muda uwe mrefu zaidi

Itengenezwe zone maalum ambapo umiliki utakuwa zaidi ya miaka 99!

Kupata muwekezaji wa kujenga ghorofa arobaini kwenda juu halafu umpe miaka 99 ni kichekesho

Lizaboni na vikaragosi wake huwezi kuwaona kwenye huu uzi
 
Mkuu,ndio maana nikatoa maoni kwamba hata muda wa chini kabisa kumiliki kwa njia ya hati iwe miaka 66,

Na kwa maeneo maalum ya uwekezaji mfano posta, kariakoo,masaki,oyster bay muda uwe mrefu zaidi

Itengenezwe zone maalum ambapo umiliki utakuwa zaidi ya miaka 99!

Kupata muwekezaji wa kujenga ghorofa arobaini kwenda juu halafu umpe miaka 99 ni kichekesho

Lizaboni na vikaragosi wake huwezi kuwaona kwenye huu uzi
Lizaboni unaitwa huku
 
Back
Top Bottom