Ili kutenda haki na kutobambikia watu kesi, Mzee Kamara Kusupa apendekeza polisi wapunguziwe majukumu

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,007
9,873
Mara ya kwanza niliposikia msamiati wa “mzungupori” sikuelewa, nilidhani msemaji anamtania mzungu mshamba anayetoka Ulaya kijijini.

1. Lakini baadaye nilipomuona mlengwa, nikaelewa kumbe walimaanisha chotara? Baba mzungu na mama Mtanzania, Rangi ya kizungu ila nywele za kipilipili.
2. Nilipotoka Gerezani mwaka 2007 niliandika muswada niliokusudia uwe kitabu, “The Imprisonment of the Poor in a Poor state: Arrest Trial and sentence”
3. Haya ni masimulizi ya wafungwa na mahabusu zaidi ya 100 waliohiari kunieleza ukweli kuhusu kesi zao na walikuwa radhi ziandikwe.
4. Stori za Gerezani ni matukio, kesi, upelelezi, uendeshaji wa mashitaka na hukumu. Kule watu wanasema kwa uhuru na uwazi mambo waliyoyafanya.
5. Hata mtu akijitahidi kuficha alilolifanya, bado hujulikana kwamba aidha alifanya ama hakufanya (alisingiziwa).
6. Gerezani mtu anaweza kusema kesi ambayo fulani alihukumiwa kunyongwa niliyemuua marehemu ni mimi.
7. Nikiwa Jela nilijua jinsi upelelezi unavyoweza kurekebisha ushahidi, aidha kuupika ushahidi usio kweli ukapata nguvu hadi ukaonekana kweli, ama ushahidi wa kweli ukadhoofishwa hadi mkosaji (aliyefanya kweli) akaachiliwa huru.
8. Nilipata pia wasaa wa kujua rushwa inavyotembea kushoto na kulia kwenye Mahakama zetu, nikajua kwanini wakosaji wa kweli rufaa zao hufanikiwa na aliyeonelewa kwenye mahakama ya awali inavyopata ugumu kutendewa HAKI hata na Mahakama za juu.
9. Nilitunga kitabu “Maisha yangu gerezani, simulizi la siku 1,888 za mateso” lengo likiwa kuonyesha mfumo wetu wa Magereza ulivyo na dosari nyingi. KWASABABU ulioanzishiwa na wakoloni.
10. Nia yangu Magereza yafanyiwe “reforms” ili kukidhi mazingira ya uhuru wa Mtanzania na utamaduni wa Mtanzania.
11. Eneo jingine nililogusa ni haki jinai “criminal justice” nimeuzungumzia upelelezi na uendeshaji wa kesi za jinai.
12. Nilipendekeza Asasi zetu za uchunguzi ziunganishwe, CID, TAKUKURU, TISS, Tume ya uchunguzi iliyobadilishwa kuwa Tume ya utawala bora na Tume ya kuchunguza mwenendo wa viongozi ziundiwe “Tanzania Bureau of Investigation” (TIB) ambayo kwa ndani itakuwa na mgawanyo wa Idara zitakazokuwa na majukumu yake.
13. Hakuna sababu ya msingi Tanzania kuwa na Taasisi nyingi zinazofanya kazi moja ya “Investigation”
14. Nilipendekeza majukumu ya Polisi yapunguzwe, maana hadi sasa Polisi anafanya kazi nne, kwanza inakamata, pili inashitaki, tatu inapeleleza kosa, yaani inakusanya ushahidi, nne inaendesha kesi kupitia PP wanao – “prosecute.”
15. Chini ya uhalisia huu ni vigumu anayeshitakiwa kujinasua, hasa anayesingiziwa. Wanaosingiziwa huwa hawaoni uhalali wa kuhonga na kumaliza mashauri yao kwa kutumia nguvu ya fedha.
16. Hapa ndipo wahalifu wazoefu hutumia mwanya wa hayo manne kujinasua kirahisi kuliko wasiofanya matukio.
17. Nilipendekeza Polisi ibaki na majukumu mawili tu, kumkamata mkosaji na kumshitaki. Jukumu la upelelezi liondoshwe Polisi, lipelekwe kwenye Asasi huru ya “Tanzania Investigation Bureau”
18. Polisi isiendesha kesi, jukumu hilo lipelekwe Ofisi ya DPP ili walau kupunguza utamaduni wa kupanga matokeo.
19. “Ma- prosecutor” walio Polisi wahamishiwe kwa DPP na wawajibike kwa DPP badala ya kuwajibika kwa wakubwa wa Polisi OCD, RCO, RPC na wengineo.
20. Eneo jingine nililogusa ni Mahakama, nikasema huu ni mfumo wa kigeni tulioanzishiwa na mkoloni, unahitaji mageuzi “reforms” kwasababu umekuwa ukibadilika kutoka kwenye ubora kwenda kwenye ubaya hadi ubaya zaidi.
21. Nilipendekeza majukumu ya Hakimu yapunguzwe, maana hadi sasa Hakimu ama Jaji anayesikiliza kesi anafanya kazi nne kubwa na nzito.
22. Kwanza Hakimu anasikiliza, pili Hakimu ni mwandishi, analazimika kuandika anachosikiliza, tatu Hakimu ni mtafasiri wa lugha maana analazimika kuandika katika English yale anayoyasikiliza katika Kiswahili.
23. Nimetoa mfano hai wa “proceedings” na “judgement” zenye English mbovu, utakuta Hakimu ameandika “my little Father, Young mother ama small father” Ndipo nikapendekeza Hakimu apunguziwe kazi, abaki na mbili tu kusikiliza na kuandika Hukumu
24. Nilipendekeza Hakimu awe na makarani wawili wa kuandika kinachosemwa Mahakamani, karani mmoja aandike kwa Kiswahili na karani mwingine aliye mtaalamu “translation” aandike katika lugha ya English.
25. Hakimu akipenda aweza kuwa na “notebook” ya kuandika tu points anazoona zitafaa kukumbukwa wakati aandikapo hukumu.
26. Hakimu anapofanya kazi zote, kusikiliza, kutafsiri na kuandika, anachoka upesi, hali inayosababisha usikilizaji kesi uchukue muda mrefu.
27. Tukitaka Tanzania ya HAKI lazima tukubali kuugharamia vilivyo huu mfumo wetu wa “justice.”
28. Kuna mengi yasiyosemwa hadharani, Hakimu anaweza kuutengeneza mwenendo wa kesi, akaupa sura anayoitaka yeye.
29. Ndio maana wakati mwingine inapotokea mtoa rushwa kumkabili Hakimu, huulizwa “mbona hamkunijia mapema?”
30. Hakimu aliyedhamiria kumsaidia mshitakiwa, hujenga mazingira ya kmwachia kupitia “proceedings”
31. Hakimu akidhamiria kufunga, hata mshitakiwa angekuwa hana hatia kama Yesu, bado ataonekana anayo hatia na atahukumiwa.
32. Kwa uzoefu wangu mwanasiasa yeyote ambaye dola inamwona msumbufu, akishitakiwa kwa “criminal” lazima ataonekana ana kesi ya kujibu, hatimaye atatiwa hatiani na kuhukumiwa japo kwa ushahidi wa kulazimisha (ushahidi wa kutengenezwa).
33. Kwenye kesi yangu cc. No 641/2000 Hakimu aliitisha mithili ya mcheza mpira anavyoita apewe pasi, kwanza alianza kuandika kwamba tarehe 14. Julai, 2000 nimeshitakiwa na kukana shitaka na kupelekwa rumande, wakati sikuwako Mahakamani.
34. Ilipofika Jumatatu ya tarehe 17/07/2000 nilikwenda Mahakamani kwa lengo la kuchukua Pasi yangu ili nisafiri kwenda Amsterdam. Askari wa Mahakama “Orderly” alinijia akaniambia “there are some development, twende ofsini kwa Hakimu, tukapita kwenye ukumbi wa Mahakama. Hakimu aliponiona aliashiria nipandishwe kizimbani, kisha akasema “ehee!”
35. Mwendesha mashitaka akasema upande wa mashitaka umeamua kuongeza mshitakiwa wa pili, akanisomea shitaka la kula njama.
36. Nikiwa nimeduwaa sijui la kufanya, Hakimu alitaka nijibu kama ni kweli au si kweli! Nikajibu sio kweli. Baadaye nikaulizwa kama ninaye mdhamini, kwakuwa sikujiandaa kushitakiwa sikuwa na mdhamini, nilienda mahabusu (Keko).
37. Baadaye nikiwa Gerezani Ukonga nililetewa “proceedings” zilizoonyesha nilishitakiwa tarehe 14/7/2000 nikasomewa tena shitaka hilo hilo tarehe 17/7/2000, aliyekuwa akiniandalia rufaa, aliuza “what happened between 14/7/2000 and 17/7/2000?” Je ulitoroka chini ya ulinzi?
38. Lakini mambo hayakuishia hapo. Majalada ya kesi zangu yalifichwa ili kukwamisha rufaa, hadi nikamaliza kifungo.
39. Nilipotoka Jela ilikuwa bahati Jaji Mkuu Agostino Ramadhan (marehemu) alisoma makala yangu iliyohusu wafungwa wa kunyongwa. Alinipigia simu akaniomba tuonane Ofsini kwake.
40. Nilipofika tulizungumza kirefu, hatimaye aliniuliza kesi iliyonipeleka Jela, nikamwelezea yote sikuficha, aliniuliza tena kama nilikata rufaa? Nilimjibu rufaa yangu CC.App. no 02 0f 2002.
41. Tatizo majalada yamefichwa ili kunikomoa, Jaji mkuu alimwita msaidizi wake aliyeitwa Mugeta, akanikabidhi kwake, akaniambia ikitokea kuna lililomshinda, usisite kunijia tena, tukaachana.
42. Mugeta aliwapigia wahusika wakayatoa majalada walikoyaficha, ndipo rufaa yangu ikaendelea nikiwa nimemaliza kifungo. Kufikia mwaka 2014 Mahakama kuu iliniachia huru nilionekana kufungwa kimakosa.
43. Naam niliwekwa huru baada ya kumaliza kifungo!
44. Nimejifunza mengi nilipofuatilia rufaa, nilibaini makarani wa Mahakama wanaweza kucheza na jalada, wanaweza kucheza na kilichomo ndani ya jalada wakaathiri matokeo.
45. Heri ya mahakam zetu asilia zilizosikiliza mashauri chini ya mti. HAKI ilitendeka hakuna aliyenyongwa akiwa hajaua. Hakuna aliyeonekana m’bakaji akiwa hajabaka, wala hakuna mkosaji aliyeonekana hakukosa.
46. Mfumo wa kigeni umetuzalia mapooza na matangopori! Tuna kibarua kizito cha kuisimamisha HAKI nchini Tanzania, ili Mungu aweze kwenda na Taifa letu.
 
Inasikitisha sana
 
Kwenye mahakama zetu kuna wapolaji wanaovaa majoho, huku yakiwa ni mashetani kumzidi hata ibirisi mwenyewe
 
Nakumbuka jina Kasupa Kamara. Who was he. A famous one!
Mmoja wa waasisi wa vyama baada ya kuruhusiwa vyama vingi.
Cha ajabu pamoja na madhila yote aliyopitia chini ya policcm na system alikuwa shabiki mkubwa wa Mwendazake
 
Back
Top Bottom