Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 1,813
- 4,545
Salaam wakuu, natumai nyote mpo salama.
Ni wazi kwamba miaka ya hivi karibuni kumekuwa na shida kubwa sana kwa watu mbalimbali kupata ajira serikalini licha ya kuwa na vigezo ya kuajiriwa. Viongozi na wadau mbalimbali wamekuwa wakitoa wito kwa vijana na watu kujiajiri lakini kiuhalisia jambo hili limekuwa gumu kutekelezeka kwa wengi kutokana na vijana kukosa mitaji itakayowawezesha kujiajiri.
Kwa maoni yangu naona ipo haja ya kuwekwa kwa ukomo wa ajira kwa watu waliojiriwa serikalini ili kupisha wengine ambao hawajapata nafasi kuingia. Mathalani, kama mwalimu amepata nafasi ya ajira basi miaka mitano ya kwanza atathmiwe utendaji wake ulivyo kama uko vizuri aongezewe miaka mitano mingine kumalizia muda wake kama ilivyo kwenye Urais.
Kuwekwa ukomo wa Watumishi wa Serikali kutatoa nafasi waliopo makazini kukusanya pesa na kujipanga na kuwa na nafasi nzuri ya kujiajiri wanapoenda mitaani. Mfumo uliopo sasa unawapa nafasi watu wachache kudumu makazini huku wengine wakitaabika licha ya kuwa na vigezo.
Zaidi ya hayo, Jambo hili litaongeza ushindani makazini na kuwafanya watu kuheshimu kazi na mishahara yao pamoja na kuwa na akili ya kufikiria miradi sahihi ya kufanya pindi muda wao wa kukaa kazini ukiisha.