teledam
JF-Expert Member
- Mar 6, 2017
- 927
- 1,239
Hadi wakati huu taifa letu lina wahitimu wengi ambao walitegemea kuajiriwa baada ya kuhitimu mafunzo yao ya elimu aidha ya vyuo vikuu ama ambao kwa bahati mbaya ni wahitimu wa elimu ya juu ya sekondari yaani kidato cha sita na wameshindwa kusonga mbele kwa kufeli ama kwa kukosa mkopo wa kuwawezesha kusonga mbele zaidi.
Aidha kundi hili ambalo kimsingi ndilo jicho la taifa limekuwa ni changamoto siyo tu kwa jamii bali kwa taifa kiujumla. Licha ya kuwa kundi hili limekuwa likiongezeka mwezi hadi mwezi,mwaka hadi mwaka bila ya jamii ama taifa kuupatia ufumbuzi wa kudumu watakwimu hapa wanaweza kuthibitisha hili, ikumbukwe kwamba kwa vyovyote hasara ni kwa jamii yetu tu lazima tuchukue tahadhari kwa kuwa na mipango kwa nguvukazi ya taifa letu ambao ni vijana kwa sehemu kubwa,vijana ni hazina kama wataandaliwa ipasavyo.
Kiufupi tu ili kupata "skilled individuals" naonelea kwamba aidha tuboreshe elimu ya juu ya sekondari kwa sasa ama tubuni na kuboresha vyuo kwa taaluma mbalimbali vya elimu kwa vitendo kama VETA n.k kwani tutapata wataalam katika kada zote kulingana na taaluma zao na kwa kiasi fulani kupunguza kasi ya ongezeko la akina bashite na wawindaji wa ajira mtaani ambapo kwa namna moja ama nyingine tutafanikiwa kukuza uchumi wa taifa letu.
Wahitimu wengi wamejikuta wakikata tamaa kwa sababu pengine ya matarajio ya wengi kwamba wakihitimu masomo wataajiriwa na kujipatia kipato cha kuendesha maisha yao ya kila siku na ndivyo mfumo wetu wa elimu ulivyo. Yaani unaandaliwa kuwa mwajiriwa badala ya chanzo cha ajira, kwa mfano mtu amepambana na pcb,au hkl advance akifeli hapo labda aishie kuwa mwalimu wa tuishieni za mtaani ama akafanye mishe zingine ambazo nyingi hazihusiani hata na taaluma yake. Hapa tunapoteza muda na nguvu kazi kwa wakati mmoja,eti mtu unajikuta baada ya miaka 14 yote ya kubukua vidudu hadi kidato chasita ukifeli tu unashindwa hata na fundi cherehani ama fundi mwashi aliyeishia la saba kiufupi inabidi uanze upya kwa kuwa unakuwa huna ujuzi wowote hii inakera na kukatisha tamaa kwa kweli msione watu wanabebeshwa maunga ama kuuza dawa za kulevya wengi wao hawapendi ila inabidi kupoza family na ndugu na jamaa waliowasubiri na kuwategemea kama msaada mbeleni kwa muda mrefu bila mafanikio.
Kama tupo serious na tunataka kujenga taifa ambalo siyo tegemezi katika nyanja yoyote lazima tuwe tayari kuufumua ama kuuboresha mfumo wetu wa elimu hii italeta tija kwa jamii na taifa kwa ujumla,unafikiri kwanini hadi leo hatuna kiwanda hata cha kutengeneza baiskeli wakati wenzetu wameunda hadi ndege,rockets na vingine vingi ambavyo kwa namna moja ama nyingine vinachangia sana katika uchumi na maendeleo ya mataifa mengi hapa duniani.
Hapa kwetu usishangae mtu mwenye astashahada ya umeme VETA akawa bora kuliko mwenye hata shahada ya umeme huu ndo ukweli mchungu hili halina ubishi na bado tunaona tupo sawa wizara husika ndo kwanza kama haina habari kabisa ipo busy kuzuia wanafunzi wajawazito wasirudi shule,kweli? Hebu fikiria mama yako angenyimwa haki ya kupata elimu kwa sababu tu amekubeba tumboni nina hakika ungeliuchukia kuanzia unyayo hadi unywele wa mtawala aliyeamua hivyo. Sina nia ya kuchochea hisia zozote kwa matamko yanayotolewa ila uhalisia ni kwamba kila mtu ana nafasi yake katika taifa lolote.
Ushauri kwa wizara yetu ya elimu; Waziri N/waziri na makatibu musikubali tu kukaa katika nyumba za serikali na kutafuna mishahara ambayo ni kodi za hawa hawa wavuja jasho bila kuwaza kwamba kuwa na mfumo bora huenda hata hayo makazi na mishara ingenona na kuwa bora zaidi kwa kuwa kila taifa ili liendelee kwa karne hii ni lazima uwekeze katika elimu bora,do something for the betterment of the community and your legacy will forever live.
Kuna gap kubwa sana kati ya taifa letu na mataifa mengi duniani kuanzia kiuchumi teknolojia n.k,hivyo ili kuziba pengo hili hatuna budi kuwa na mifumo bora na rafiki ya elimu kwa manufaa ya taifa letu,la sivyo itatuchukua karne nyingine kuja kustuka badala yake tutaendelea kuibiwa rasili mali zetu tena kwa kutoa wenyewe bila kushurutishwa.
Nawasilisha.