Ili kupambana na umaskini na mfumuko wa bei serikali ifanye haya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ili kupambana na umaskini na mfumuko wa bei serikali ifanye haya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nkisumuno, Jul 16, 2012.

 1. n

  nkisumuno JF-Expert Member

  #1
  Jul 16, 2012
  Joined: May 22, 2012
  Messages: 209
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  KILIMO Kila mkoa utenge eneo la uzalishaji wa chakula, inunue matrekta, iwakusanye vijana wawe chini ya wanajeshi ambao watasimamia shughuli za kilimo baadala ya kuwapa wawekezaji katika shughuli za kilimo. serikali itafute masoko nje. Vijana waelimishwe kuhusu ubaya wa kukimbilia mjini na kufanya umachinga. Iboreshe miundo mbinu vijijini kwa kusambaza umeme vijijini, iachane na mpango wa kuzidi kuboresha miundombinu ya mijini ili vijana wavutiwe kubaki mjini. Wanajeshi wasimamie shughuli za kilimo, aidha wafungwa magerezani wasaidiane na vijana huku askari magereza wakiwa wasimamizi Serikali ikifanya haya baada ya muda mfupi tutakuwa na chakula cha kutosha pasipokutumia nguvu na pesa nyingi kwa ajili ya kutafuta wawekezaji Viongozi wetu waachane na matumizi makubwa ya rasilimali za nchi ili kufanikisha mpango huo UJASIRIA MALI NA UFUNDI Kutokana na ongezeko la vijana wanao maliza shule za sekondari kuwa wengi kujengwe au vianzishwe vituo vya ujasiriamali katika kila tarafa viwepo vituo au vyuo viwili. Wapate vifaa muhimu wataalamu kama vile usindikaji, utengenezaji wa sabuni, mishumaa, ufundi cherehan nakadhalika. hii itasaidia kuwapa uwezo vijana wa kuzalisha mali baadala ya kukaa vijiweni na kuzunguka na bidhaa mitaani. Elimu hiyo ya ujasiriamali itiliwe mkazo vijijini ambako kuna idadi kubwa ya watu wenye kipato duni na hii itasaidia vijana kubaki vijijin. Serikali iachane na tabia ya kila mara kuendelea kuomba omba, baadala yake iwawezesha watanzania kutumia fursa zilizopo katika kujiletea maendeleo. NAWASILISHA
   
Loading...