Ili Kupambana na 'Umasikini' Serikali ya Tanzania haiwezi 'Kutulazimisha' Watanzania wote tuutumie 'Ubini' wa 'Laizer' ambao una 'Nyota' ya Utajiri?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
43,116
2,000
Mshindi wa Jackpot ya SportPesa, Lilian Ngitoria Laizer, amekabidhiwa kitita chake kiasi cha Sh. 267,800,060 na Kampuni ya Michezo na Burudani ya SportPesa Tanzania, huku akieleza mipango yake ni kufungua biashara kubwa.

Nipashe

Kuna Mtu aliwahi kuniambia huko zamani kuwa Pesa, Elimu na Mafanikio huwa yanategemea na Historia nzima ya Koo zako zote mbili. Nimeamini!!
 

darubin ya mbao

JF-Expert Member
Aug 3, 2016
1,504
2,000
Wewe Kuanzia Babu na Bibi zako wa Koo zako zote mbili hawana Historia ya kuwa na ama Pesa na Elimu, halafu leo hii eti na Wewe 'Utusue' pia?
Umasikini na ufukara ni kama tabia unaambukizwa, ni ngumu sana kutusua kama unaishi na kukulia kwenye jamii ya watu masikini na wewe unakua maskini by default ref: poverty cycle.
 

St Lunatics

JF-Expert Member
Aug 29, 2015
6,671
2,000
Jana kuna mchina alisema $5 million dollars pocket change nilisema huyu atakuwa mdogo wake Chenge.


Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 

yuzazifu

JF-Expert Member
Oct 6, 2018
5,128
2,000
Vp kama ndoto zangu ni kuona ndoto za mwingine zinatimia?
kuona ndoto za mwingine zinatimia haikuzuii wewe kujenga ndoto zako, hiki mnachojaribu kuaminishana hapa na mtoa mada ndo kikwazo kikubwa cha vijana wengi wa kiafrica, wenzetu huangalia zaidi ndoto zao bila kujali historia za familia zao, tizama akina ronaldo, messi wametoka familia duni kabisa bt kwa kua waliwekeza katika kuzijenga ndoto zao leo hii dunia nzima inawatukuza
 

Ezekiel Mbaga

JF-Expert Member
May 28, 2018
9,355
2,000
H pia n sawa na connection tuu, unakuta mwanaume anaoa kwenye familia masikini na duni sana hapo ataanza kujenga maisha mazur kwa mkwe kwanza huku akichelewa kujenga kwake
 

kagoshima

JF-Expert Member
Dec 31, 2015
2,137
2,000
Mshindi wa Jackpot ya SportPesa, Lilian Ngitoria Laizer, amekabidhiwa kitita chake kiasi cha Sh. 267,800,060 na Kampuni ya Michezo na Burudani ya SportPesa Tanzania, huku akieleza mipango yake ni kufungua biashara kubwa.

Nipashe

Kuna Mtu aliwahi kuniambia huko zamani kuwa Pesa, Elimu na Mafanikio huwa yanategemea na Historia nzima ya Koo zako zote mbili. Nimeamini!!
Hahah we janaa we we huishi vituko
 

yuzazifu

JF-Expert Member
Oct 6, 2018
5,128
2,000
ndoto zangu ni kuona ndoto za mwingine zinatimia.
acha kuzungusha maneno mkuu haitakusaidia kitu, bill gate anakuambia "acha kujifananisha na yeyote katika dunia hii, kufanya hivo utakua umejidunisha mwenye"

historia ya familia haina athari yoyote katika kupata mafanikio yako, akina diamond, kiba na harmo wangeangalia historia za familia zao sidhani leo wangetimiza ndoto zao
 

komrade

Senior Member
Sep 26, 2019
179
250
Mkuu, asante kutuhabarisha. Wahenga walisema MWENYE BAHATI HABAHATISHI

Serikali inakulazimisha kupambana na umaskini wako kwa kutumia nyota yako, siyo nyota ya Laiser wala matakwa ya Mabeberu

Usiwaze wala isikuumize kichwa, kupanga ni kuchagua. Mambo yote 10/28. Baada ya hapo, mwendo mdundo kama kawa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom