Justice minister
JF-Expert Member
- Sep 1, 2016
- 1,173
- 823
Kuna wimbi kubwa la raia wa kigeni wanaokimbilia nchini na kwa kuwa sheria za uhamiaji zinaonekana kupwaya wahamiaji hao wamekuwa wakijichanganya na wazawa na baada ya muda hujipachika utanzania na kupata haki zote zinazomstahili mtanzania.
Kwanza raia yeyote wa kigeni hawezi kuingia nchi nyingine bila kujua wapi atapata hifadhi, hapa utaona kwamba wapangishaji wa nyumba wanahusika kwa kiasi kikubwa kuwahifadhi wahamiaji haramu bila wao kujua. Hapo serikali inapaswa kuhakikisha mtu yeyote anayetaka kujenga nyumba na kupangisha anapewa kibali kwanza kutoka ofisi ya serikali ya mtaa na kuhakikisha anatoa kila anayetaka kupanga nyumba yake anafika kwanza ofisi ya serikali na kuacha nyaraka zinazomtambulisha alikotokea. Haiwezekani mtu ahamie sehemu nyingine bila watu kujua alikotoka na sababu ilikuwa nini.
Raia yeyote atakayewakwepa askari wa uhamiaji mipakani atakuja kukumbana na watu wa serikali za mitaa na kudhibitiwa. Ukipita mitaani warundi wanyarwanda, waganda, wakongo, wamalawi, wasomali, wasumbiji na raia wa nchi zinaizunguka Tanzania wanaishi kama wazawa, hii ni hatari kwa usalama wa nchi.
Cc: Mwigulu Nchemba