Keynez
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 2,397
- 3,884
Najua hii mada inaweza kuwashtua wengi, ila nipe muda kidogo nitakuelewesha.
Juzi juzi, nilileta mada iliyokuwa inaongelea ni jinsi gani taifa letu sasa linafuata mkondo wa Kifashisti. Nilijaribu kuelezea kwa uwezo wangu huku nikiambatanisha video kadhaa kutoka kwa Profesa mbobevu wa mambo ya Historia na Siasa.
Baada ya kutafakari na kusoma zaidi kuhusu suala hili, nimegundua haya mambo yametokea sana katika historia. Na kwa sababu yameshatokea na yanajirudia, ni budi kujifunza kutoka katika historia.
CCM Mpya kama chama cha kifashisti, kitakuwa na sifa kuu tatu.
Kwanza, kitakuwa kinahubiri sana Utaifa na Uzalendo kama moshi wa kufunika maovu na udhaifu wao.
Pili, kitawakumbatia matajiri na wafanyabiashara wakubwa. Hili nalo limeshafanyika kwa kiwango kikubwa.
Tatu, litaminya uhuru wa maoni na mawazo mbadala kuhusu mustakabali wa nchi. Sifa ya kwanza itatumika sana kufanikisha sifa hii ya tatu. Kila mwenye maoni tofauti na ya watawala atakuwa anashutumiwa kuwa siyo mzalendo, ni mhaini, kibaraka, nk. Tuendako ni kubaya zaidi ya sasa.
Hizi ndiyo zitakuwa 'hallmarks' za CCM Mpya. Nini sasa kifanyike?
Nyakati, ambazo watawala wameshindwa kuzizuia ndizo ambazo zimeilazimisha CCM Mpya kwenda kwenye mlengo huu wa kifashisti. Muda na mazingira ya kisiasa na kijamii yamewalazimu na kuwasukuma huko. Ilikuwa ama chama kife au wakumbatie siasa za kipropaganda, mkono wa chuma na kuwaweka karibu matajiri (kwa kuwarubuni au kwa vitisho).
Uamuzi huu hata hivyo utafanya wasiweze tena kudai wao ni chama cha kijamaa. Unaweza kusema walishautupa Ujamaa toka kitambo, ila mazingira haya mapya yatafuta hadaa zote za Ujamaa katika siasa zao.
Ndiyo maana umeshasikia wameanza kuahidiana mautajiri na ubilionea na ni kweli tutegemee kuchipuka 'wazalendo' mabilionea ambao chanzo kikuu cha utajiri wao kitakuwa ni mahusiano ya kisiasa waliyonayo.
Katika ulingo wa kisiasa, mazingira haya yanaacha 'vacuum' inayohitaji kujazwa. Kuna sauti ambazo zitataka watu wa kuwasemea. Sauti hizo inabidi zihubiri yale ambayo Ujamaa ulijaribu kuyapigania.
Kwa muda sana nimekiona chama cha ACT Wazalendo kama chama cha kimkakati. Naona uwezekano ACT kama chama ambacho kiliandaliwa kuja kuziba mwanya huu kabla 'genuine oppositional figure' hajafanya hivyo.
Niliwahi kusema, uamuzi wa Tundu Lissu katika kampeni za Uchaguzi wa 2020 kumrudia Nyerere na yale aliyohubiri miaka ya 1960's ulikuwa ni uamuzi muhimu sana katika kampeni zile.
Laiti kama uchaguzi ungekuwa wa huru na wa haki, uamuzi ule inawezekana ungekuwa moja ya sababu za matokeo chanya kwa CHADEMA. Lakini wote tunajua nini kilifanyika!
Katika historia, mapambano kati ya Wasoshalisti na Wafashisti huwa ni makali sana. Naona kama tunaelekea huko huko.
Ila hilo litatokea iwapo tu kama kutakuwa na upinzani wa kweli wa kukabiliana na Ufashisti. Mamluki watambulike mapema na watengwe. Pia tafakuri ya nguvu inabidi ifanyike ili mbinu sahihi zitambulike na zitumike.
Kwa mtazamo wangu, Siasa ni Sayansi na Sanaa pia. Ukijipanga vizuri, ukajua mbinu za mpinzani wako na madhaifu yake, na pia ukayatambua ya kwako, unajiweka kwenye nafasi nzuri ya kupambana. Kwenye hili, historia ni msaada muhimu.