Uchaguzi 2020 Ili kuondoa utata kuwe na mawakala wa vyama vyote vinavyoshiriki uchaguzi katika vituo vyote na wapewe 'nakala' za matokeo

Trust None

JF-Expert Member
Feb 12, 2018
1,260
4,415
Pamoja na kwamba Magufuli amepiga kampeni kwa miaka mitano na miezi hii miwili ya NEC lakini ukifuatilia vizuri kampeni zake, utagundua kuwa ana hofu zaidi ya kushindwa kupata kura za kumuwezesha kushinda uchaguzi ikiwa na maana kwamba asilimia kubwa anaamini anaweza kushindwa. Hii inajidhihirisha kutokana na kauli, kutekeleza ahadi papo kwa hapo na vitisho kwa raia wakati wa kampeni.

Kwa upande mwingine, Tundu Lissu ana hofu kidogo ya kushinda uchaguzi ikiwa na maana kwamba asilimia kubwa anaamini atashinda uraisi. Ni kutokana na kauli na misimamo yake na kukubalika kwake kwa kipindi hiki kifupi cha kampeni takribani mwezi mmoja tu tofauti na Magufuli aliyepiga kampeni tangu 2015

ILI KUONDOA UTATA HUU, 'NEC' WAHESABU KURA KWA UWAZI 'LIVE KUPITIA TVs NA REDIO'

Pia kuwe na mawakala wa vyama vyote vinavyoshiriki uchaguzi katika vituo vyote na wapewe 'nakala' za matokeo.

Screenshot_20201001-130928.png
 
Uko Tanzania kweli wewe?

Magufuli sio mshindani ndio maana hakubali kushindwa. Baada ya kufanya siasa za kikatili huku akiamini kaua upinzani, anayoyaona yanamfedhesha sana maana aliamini anapendwa sana na kaua upinzani. Hivyo ameingiwa na hofu kubwa maana hana uhakika anakubalika kiasi gani, na kwake kushindwa ni bonge la aibu ambayo hayuko tayari kwa hali hiyo.
 
Over confidence ni mbaya JPM alidhani kujenga madalaja ya juu flyover nakununua ndege inatosha kushinda uchaguzi kwamba atapata walk over win, hajui wa Tz ni wabobezi katika unafiki asipo angalia hata 25% uenda hasipata nawanao hamasisha watu kumchukia wako ndani ya CCm

.
 
Hata kama ni wewe ungeweweseka, umekataza mikutano ndani ya miaka mitano, ukawanunua hata wale wenye msimamo kwa kutegemea kwamba umebomoa upinzani kazi imeisha .

Sasa kinachomuumiza kichwa zaidi ni hiki hapa, je hawa watu wameelewana lini na wamekutana wapiii?
 
Baada ya kutangazwa washindi How are we going to convince washirika wa maendeleo kushirikiana na sisi ndo swali la maana kwa sasa...
 
Nimemuuliza aliyeandika!
Mnadai kuwa kwa kipindi cha miaka mitano magufuli amefanya mambo makubwa sana.Kama amefanya mambo makubwa sana inakuwaje yeye leo hii ahitaji wananchi kuliko wananchi wanavyomuhitaji yeye?Unaelewa kuwa kitendo cha magufuli cha kuomba kura kwa kupiga magoti ni kwamba anawahitaji wananchi kuliko wananchi wanavyomuhitaji yeye?

Yaani uwafanyie wananchi mambo makubwa sana halafu ukawaombe tena kuwatumikia kwa kupiga magoti?Inaleta sense?Kama amewafanyia wananchi mambo makubwa sana ni nani anatakiwa kumuhitaji mwenzake kwa kupiga magoti?

Kama amewafanyia wananchi mambo makubwa sana hao wananchi ndiyo wanapaswa kumpigia Magufuli magoti kumuomba aendelee kuwa Rais wao ili aendelee kuwafanyia mambo makubwa,ila hapa inakuwa ni kinyume chake yaani Magufuli ndiye anapiga magoti!Kama Magufuli amewafanyia watu mambo makubwa sana basi atulie hayo mambo makubwa yamnadi na siyo yeye ajinadi mwenyewe tena kwa kupiga magoti.

Hii inamaanisha nini?Hii ina maana Magufuli anajua kabisa hakuna la maana alilofanya na anachofanya sasa hivi ni anataka achukue madaraka kwa njia ya kulaghai wananchi(Magoti).Huwezi kufanyia watu mambo makubwa halafu badala ya hao watu wakuhitaji wewe kuliko wewe unavyowahitaji wao iwe kinyume chake yaani eti wewe uwahitaji wao kuliko wao wanavyokuhitaji wewe.

Magufuli ni tapeli asiekuwa na aibu aliekosa kibali cha wananchi na ni heri ajitoe kwenye kinyang'anyiro hiki apishe wenye kibali cha wananchi wachukue dola
JamiiForums312469786.jpg
 
Over confidence ni mbaya JPM alidhani kujenga madaraja ya juu flyover nakununua ndege inatosha kushinda uchaguzi kwamba atapata walk over win, hajui wa Tz ni wabobezi katika unafiki asipo angalia hata 25% uenda hasipata nawanao hamasisha watu kumchukia wako ndani ya CCm

.
 
Over confidence ni mbaya JPM alidhani kujenga madalaja ya juu flyover nakununua ndege inatosha kushinda uchaguzi kwamba atapata walk over win, hajui wa Tz ni wabobezi katika unafiki asipo angalia hata 25% uenda hasipata nawanao hamasisha watu kumchukia wako ndani ya CCm

.
Hapana mkuu siyo wabobezi wa unafiki, wanafiki ni wale wanaomzunguka ambao wanaofaidika na yeye. Kiuhalisia kabisa binadamu yeyote kwake kipaumbele ni maisha bora yeye na familia yake kwanza.

Kama hana uhakika na kula yake, tibiwa yake, kuhudumia familia yake daily hata ulete daladala za helikopta is nothing... Halafu kumbuka asilimia 75 au 80 ya watanzania wanaishi vijijini, habari za fly over, sijui stigilazi goji, sijui bombardia kwake haoni direct connection.
 
Magufuli sio mshindani ndio maana hakubali kushindwa. Baada ya kufanya siasa za kikatili huku akiamini kaua upinzani, anayoyaona yanamfedhesha sana maana aliamini anapendwa sana na kaua upinzani. Hivyo ameingiwa na hofu kubwa maana hana uhakika anakubalika kiasi gani, na kwake kushindwa ni bonge la aibu ambayo hayuko tayari kwa hali hiyo.
Endeleeni kuwadanganya wakina Sky Eclat , wabeba mabox wote pamoja na beberu Amsterdam. Mkipata hata 20% mkatambike!. Lakini nyinyi tumewazoea kwa u-turn kwanza mlisema hamtashiriki uchanguzi mpaka ipatikane Katiba Mpya mara tena hao wameingia kwenye kinyang'anyiro bila Katiba Mpya.

Juzi Msaliti Lissu akapigwa stop for 7 days na Kamati ya Maadili ya Uchaguzi mkasema mtaendelea na kampeni hamkubali adhabu hiyo jana Kamati Kuu ya Chadema wenye saccos wameikubali adhabu na watakata rufaa lakini nyinyi wafuata bendera ya msaliti Lissu mlisema mtaendelea na kampeni leo Jumapili naona mmeufyata mkia! Hahahaha..
 
Over confidence ni mbaya JPM alidhani kujenga madalaja ya juu flyover nakununua ndege inatosha kushinda uchaguzi kwamba atapata walk over win, hajui wa Tz ni wabobezi katika unafiki asipo angalia hata 25% uenda hasipata nawanao hamasisha watu kumchukia wako ndani ya CCm

.
Rais Magufuli atashinda zaidi ya 80%!
 
Mnadai kuwa kwa kipindi cha miaka mitano magufuli amefanya mambo makubwa sana.Kama amefanya mambo makubwa sana inakuwaje yeye ahitaji wananchi kuliko wananchi wanavyomuhitaji yeye?Unaelewa kuwa kitendo cha magufuli cha kuomba kura kwa kupiga magoti ni kwamba anawahitaji wananchi kuliko wananchi wanavyomuhitaji yeye?....
Kwani hicho nacho unaona ni hoja? Si hicho amecheza hadi muziki!!
 
Hivi mtu kabisa umekaa unawaza kwamba Magu anahofu ya kushindwa?

Lisu haungwi mkono na tasisi yeyote ya vyombo vya usalama sababu ya umbumbumbu wake wa kushindwa kujua awateke vipi.

Kaenda zanzibar kasema eti chadema haina maslahi na zanzibar. Hii kauli ina utata sana tasisi kama jeshi wanamuona huyu ni muhuni tu.

Kisha Amsterdam anapambana kufa kupona Lisu awe rais. Hiki kitu taasisi kama ya usalama wa taifa wanamuona Lisu kama kibaraka flani.

Yani Lisu sijui hata kama ana washauri
 
Back
Top Bottom