Ili kundoa usumbufu kwa serikali na CCM, Wizara ya elimu iagizwe kuondoa topiki zinazomfanya mwanafunzi kuwa mchambuzi,masomo ya kuchagua A au B muhim

chiembe

JF-Expert Member
May 16, 2015
11,983
20,631
Nimetafakari sana na kugundua kumbe ccm hii shida tunayoipata tumeitengeneza wenyewe tangu enzi za mwalimu Nyerere

Kipindi cha mzee Nyerere,masomo mengi ya kuhoji mifumo yalifundishwa, na haya ndio shida kubwa kwetu

Awamu ya mzee Mwinyi na Mkapa,Benki ya Dunia na mashirika ya kimataifa yalimwaga pesa katika mitaala ili kuyafuta masomo haya,kwa kweli vitabu vilikuwa vinatoka kila leo na vilifuta yale mambo ya hovyo ya enzi za Mwalimu yaliyohamasisha kuhoji na kujenga hoja

Ila sasa bado tatizo lipo,mitaala lazima ipekenyuliwe upya, wachungaji na viongozi wa dini wapewe nguvu ya kuindorse siasa na wanasiasa, imani ichukue nafasi ya watu kujadili matendo ya wanasiasa na siasa, kila mkutano,viongozi wa dini waitwe waje wapandikize mambo yao ambayo yatasaidia watu wasifikiri ila wasubiri muujiza

Bongo fleva zipigwe kwa nguvu zote ili kwenye mikutano watu wacheze tu, wale wanaodili na kilimo wasijiulize kwa nn mazao yamepungua, wakiuliza waambiwe mapenzi ya Mungu, au achague A au B

Ntaendelea
 
Jina lako limenihamisha mawazo na kunitoa kwenye reli ndugu mleta mada!
 
Back
Top Bottom