Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,470
- 911,173
Matokeo ya URAISI hujumlishwa na kufahamika majimboni sasa kwa kulinda ufisadi wa CCM, NEC huyazuia majimbo ya uchaguzi kutotangaza matokeo ambayo tayari yanajulikana na kutoa mianya mikubwa ya uchakachuaji wa matokeo ya URAISI
Tangia mfumo wa vyama vingi urejeshwe mwaka 1992 na kuanza kutumika mwaka 1995 yamekuwepo malalamiko ya kimsingi ya wagombea URAISI wa upinzani kuwa kura zao ziliibiwa.
Mwaka 1995, Augustine Mrema alilalamika Mkapa alimwibia kura kupitia tume ya uchaguzi NEC.
Mwaka 2010, Dr. Slaa alilalamika JK alimwibi kura kupitia tume ya uchaguzi NEC.
Mwaka 2015, Lowassa aliilalamikia NEC kutangaza matokeo feki na kuitaka iache mara moja kutangaza matokeo hayo. NEC ilikaidi na hata ilipopelekewa kitabu cha malalamiko ya UKAWA hadi leo imeyakalia.
Katika jimbo la uchaguzi la TANDAHIMBA NEC ilitangaza matokeo feki yaliyoonyesha Magufuli alishinda jimbo hilo wakati alibwagwa vibaya na Lowassa. Kilichosaidia ni nakala halisi ya matokeo hayo kilipozagaa mitandaoni ndipo NEC ikaona haya na ikayabadilisha.
Swali ambalo hadi leo NEC hawako tayari kulijibu hivi matokeo feki ya TANDAHIMBA waliyatoa wapi?
Upo uvumi uliozagaa maeneo mengi CCM huajiri wataalamu wa kughushi fomu za urais zitokazo majimboni ya uchaguzi na kuyabadilisha matokeo huku sahihi za wahusika kughushiwa na baada ya unyama huu dhidi ya sisi wapigakura fomu tajwa hukimbizwa NEC ambayo hutangazwa kuwa ndiyo matokeo halisi.
Kuondoa dhana hiyo ni lazima UKAWA waishinikize NEC ikubali hakuna sababu yoyote ya maana matokeo yanajulikana majimboni kupewa usalama wa taifa kwenda mahotelinj na kuyachakachua kabla ya kwenda NEC kutangazwa.
Kazi ya NEC iwe ni kuyajumlisha matokeo ya majimboni na kutangaza matokeo ya kitaifa siyo kuwa ni mshika dau wa matokeo ya urais majimboni.
Pili, tume ya uchaguzi ishinikizwe iwe na mawakala wake yenyewe majimboni na iache mara moja kuwatumia mawakala wa serikali za mitaa ambao hurubuniwa na CCM kwa kuahidiwa vyeo au kuporwa vyeo ili watangaze matokeo feki.
Yapo mapendekezo ya NEC mezani mwa Rais Magufuli juu ya NEC kujitegemea kwa kuacha kuwatumia mawakala wa serikali za mitaa lakini huyu Rais kayakalia kwa sababu anajua fika bila uwakala wa serikali za mitaa hawezi kushinda uchaguzi ujao.