Nicholaus Kilunga
JF-Expert Member
- Feb 15, 2014
- 1,188
- 570
No way,ili kuikoa CUF na mgogoro mbaya na wa kutengenezwa na maadui wa CUF wa nje na ndani,basi katibu mkuu wa chama hicho Maalim Seifu ni lazima akubali kujishusha na kukubali kumtambua Profesa Lipumba kama mwenyekiti wa CUF na akubali kufanya nae kazi na kundi lake lote,hii ndo namna pekee ya kuikomoa CCM na serikali yake inayodaiwa kuwa ipo nyuma ya huu mgogoro hasa ikiegemea upande wa Profesa Lipumba.
Umma wote wa watanzania wa ndani na nje ya nchi unafahamu ni kwa namna gani maamuzi ya Lipumba kujiuzuru nafasi yake ya uenyekiti na maneno aliyoyaongea kuhusu mgombea urais wa UKAWA mh Edward Lowassa,umma pia unafahamu namna Lipumba kwa sasa anavyobebwa na serikali kupitia taasisi zake ikiwemo ofisi ya msajiri wa vyama vya siasa na polisi kukalia kimya matendo ya wafuasi wake wanaodaiwa kuasisi vurugu na mivurugano inayoendelea ndani ya CUF,lakini kwa sasa hakuna namna,ni lazima Seif na timu yake ambayo kimsingi ipo kikatiba,akubali kukaa meza moja na Lipumbana kundi lake,hii ndo namna ya pekee kumkomoa Lipumba na wale wanaozaniwa kuwa nyuma yake wakimtumia,hyo ndo namna pekee ya kuiunganisha CUF kwa sasa,la sivyo akiendelea kupingana na Lipumba CUF itazidi kumeguka na hili ndilo wanalolitaka CCM na serikali yake,hiki ndicho huenda alichotumwa kukifanya Lipumba.
Ukiona mtu msomi wa kiwango chake anakubali kuisigina katiba ya chama chake aliyoapa kuilinda na kuitetea,ukiona anamsifu Jecha kwa kufuta matokeo ya uchaguzi mkuu Zanzibar ambayo yalidaiwa kumpa ushindi mkubwa Seif ujue hapo kuna jambo kubwa lipo nyuma linakuja,waswahili wanasema ukiona mtoto wa Simba anachezacheza porini kwa furaha ,jua mama yake hayupo mbali,hii tusipoidhibiti haitaishia kwa CUF pekee,bali itakuja kwenye vyama vyote,na walengwa wa mkakati huu ni wana UKAWA na UKAWA yenyewe,ndio maana nazidi kusisitiza hapa njia pekee ya kumkomoa Lipumba na CCM ni kwa Seif kujishusha na kumtambua Lipumba na kufanya nae kazi bila kujari kama ni kweli Lipumba anaweza kuwa anatumikishwa na kutumika ama ni dhamira yake ndiyo imemrudisha CUF,kwa njia hii tu pekee atakuwa ameiponya na kuiokoa CUF.