Ili kumaliza migogoro ya wakulima na wafugaji naishauri serikali ifundishe ZERO GRAZING kwa wakulima

Chris Lukosi

Verified Member
Aug 23, 2012
4,584
2,000
Nndugu zanguni,

Kama mjuavyo kila kukicha lazima usikie migogoro baina ya wakulima na wafugaji nchini, migogoro ambayo hupelekea vifo vingi tu.

Nimekaa na nimeona nitoe ushauri wangu kwa serikali ku introduce zero grazing kwa wafugaji ili kuondoa kabisa hii kero. Serikali iwapatie maeneo wafugaji, maeneo ambayo watayatumia kwa kufugia mifugo yao na kulima nafaka.

Utaratibu huu nimeuona Botswana , South Africa na hata huku UK ni mfumo mzuri wa ufugaji tena untawasaidia wakulima kupata kipato kikubwa kwani mifugo yao itaongezeka na kuwa na afya nzuri tofauti na utaratibu wao wa sasa wa kuhama hama jambo ambalo linaifanya mifugo ichoke na pia kusababisha migogoro


Kila mfugaji akiishapewa eneo lake afundishwe namna zero grazing inavyofanyika (naamini kuna maafisa kilimo wengintu wa kutoa somo) eneo linagawanywa mara nne waqkati ngo'mbe wanakula nyasi kusini, kaskazini mahindi yanapandwa kaskazini majani mapya yanaotwa na magharibi mazao mengine amabayo baada ya kuvunwa mabaki yake yanakuwa chakula cha mifugo yanapandwa

Hii itamsaidia mfugaji kubadili maisha na kusettle sehemu moja na pia itamfanya apatane na nduguye mkulima
Na pia itamsaidia kutumia faida zote za mifugo kuanzia samadi hadi ngozi kwani wanapohamahama wanakuwa wanapoteza mbolea bure tu. Na pia itasaidia hata wao wenyewe wakihitaji mikopo kutoka serikalini au mabenki kwani sasa watakuwa na address kamili na itakuwa rahisi kufanya tathmini ya raslimali walizonazo

Mbona pale SUA na UYOLE mifugo imewezekana? hiyo elimu kwa nini wasiipeleke kwa jamii?

Huu ni ushauri wangu kwa mtazamo wangu tu ...
 

time theory

JF-Expert Member
Nov 22, 2013
767
1,000
Wazo lako no zuli na nina liunga mkono,lakini tatizo lipo kwa wapeleka hiyo elimu.......wamelalala fofofo.

Matatizo yanayotokea sasa hata wahusika wenyewe wamesha shauri namna nyingi tu za kumaliza hilo tatizo lakini msimamizi ......amelala fofofo.
 

Tuko

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
11,181
2,000
Ni wazo zuri japo jina ulilotumia sio sahihi. Unachoongelea hapa ni controlled rotational grazing. Zero grazing ni ile ya ng'ombe kufungiwa na mfugaji kwenda kukata majani na kumletea.
Pendekezo lako litafanya kazi sio kwa serikali kuwafundisha tu wafugaji, bali kuwawezesha pia. Wasaidiwe katika kuanzisha improved pasture lands, improved grass quality, availability of drinking water, improved cattle breeds nk...
Serikali inatakiwa itenge bajeti na iwezeshe uendelezwaji wa ranch za wakulima, at least ekari 1,000,000 kila mwaka. Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali, gharama za mwanzo za kuendeleza eneo la machungio tz ni takribani tsh laki 5, kwa hiyo kwa ekari milioni moja (ambazo kitaalamu zinaweza kusustain ng'ombe laki 5) ni 500bn kitu ambacho serikali haishindwi. Tz ina ng'ombe kati ya milioni 19 na 21 kwa sasa na zaidi ya 90% wapo katika matunzo holela. Serikali ikiamua kuanzisha programme ya miaka mitano na ikatenga jumla ya hela kama trillions 10 kwa miaka hiyo, hakika tz itakuwa mbali sana kwenye ufugaji na uchumi wa nchi utaendeshwa kwa kilimo...
 

eddy

JF-Expert Member
Dec 26, 2007
13,719
2,000
lukosi, mie sijui tatizo ni nini hasa? david matayo ameishi na kufanya kazi huko kama mtaalamu wa kilimo lakini kashindwa kabisa hata kushauri nini kifanyike!

lakini najiuliza hata simba wa hifadhi ya Cruger wana afya ukilinganisha na hawa wa serengeti waliojaa ukurutu na trakoma.
 

umla

JF-Expert Member
Oct 20, 2012
1,166
1,250
Zero grazing is desirable for only few number of animal,unakuta mtu ana ng'ombe mia tano then unamwambia afanye zero grazing is it sound.
 

Lokissa

JF-Expert Member
Nov 20, 2010
7,447
2,000
mmasai, msukumuma nk uchumi wao ni ngombe
ngombe hizo zinaliiingizia pia taifa fedha za kigeni
Tanzania hatuagizi nyama nje..
wanasomesha kwatoto wao kwa kuuza hao ngome
leo hii uje na wazo la zero grazing aisee haya maajabu ya kufunga mwaka 2013
 

Mdau

JF-Expert Member
Mar 29, 2008
1,792
1,500
Kweli,ianzie kwenye TEMBO lakini.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom