Ili kulinogesha penzi lenu, fanyeni haya sikukuu ya idd | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ili kulinogesha penzi lenu, fanyeni haya sikukuu ya idd

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by MziziMkavu, Aug 19, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Aug 19, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  MziziMkavu na Mpenzi wake.

  NI kweli kabisa kwamba, kwa wapenzi wanaopendana kwa dhati kila siku ni sikukuu kwao. Hata hivyo, sina budi kuwakumbushia baadhi ya mambo ambayo ni vyema mkafanyiana katika sikukuu hii ya Idd inayokuja, lengo likiwa ni lilelile la kulinogesha penzi lenu.
  Jifungieni chumbani
  Hili si kwa wale walio nje ya ndoa, nawazungumzia wale ambao wamehalalishwa kufanya mapenzi, nawazungumzia wanandoa na siyo nyie mnaodanganyana na kuvunja amri ya sita.
  Kwa wanandoa, yawezekana siku hiyo mkawa hamjisikii kutoka kwenda popote, basi tulieni chumbani kwenu. Cha kufanya siwezi kuwafundisha ila mahaba ya siku hiyo si vibaya yakawa tofauti na ya siku zote.
  Naelewa wengi mlikuwa mkipeana mambo kwa kujibanabana kutokana na kuwepo kwenye mwezi mtukufu. Tumieni siku hizo kumaliza kiu yenu.
  Kama chumbani kwenu mtakuwa mmepakinahi, tafuteni hoteli iliyotulia muende mkapumzike kwa raha zenu.
  Kununuliana zawadi
  Siku zote zawadi ni chachandu katika penzi. Kumbuka kwamba katika suala la uhusiano, zawadi ni zawadi bila kujali ukubwa wake. Hii itategemea tu na uwezo wako.
  Kwa maana hiyo basi ni vizuri ukamwandalia zawadi nzuri mwenza wako ambayo itamfanya aione siku hiyo ni muhimu kwenu.

  Kadi maalum
  Hili kwa wengine itakuwa ni kama kuwakumbushia. Usisahau kabisa kumwandalia mpenzi wako kadi ya kumtakia Idd njema.
  Urasmi katika hili ni wa kuzingatiwa, angalia kadi yenye rangi za kimahaba na ujumbe ulio muruwa.

  Tokeni muende kokote
  Yawezekana katika kipindi chote cha uhusiano wenu hamjawahi hata siku moja kutoka pamoja kwenda kwenye ukumbi wa starehe ama sehemu yoyote tulivu.
  Kwa sikukuu hii inayokuja si vibaya ukafanya hivyo na kama mna utaratibu wa kufanya hivyo kila wikiendi, safari hii mnaweza kupanga kwenda sehemu tofauti ikiwezekana hata kutoka nje ya mji mnaoishi.
  Kuna mengi ya kufanya mnapotoka ‘out’, mojawapo ni kubadilishana mawazo juu ya maisha yenu, kuombana msamaha pale ambapo mlitokea kutofautiana. Yaani ni kipindi cha kulikarabati penzi lenu na hata pale mtakapokuwa mnarudi inakuwa ni kama vile mnafungua ukurasa mpya.

  ‘Surprise’
  Surprise zipo za aina nyingi, kwa mfano inawezekana hujamuambia mpenzi wako chochote kuhusu sikukuu lakini siku hiyo unaweza kumshitukiza kwa zawadi, kumvisha pete ya uchumba, kumtoa ‘out’ na mambo mengine ambayo yatamfurahisha utakopomfanyia kwa kum-surprise.

  Ni siku za furaha
  Ninachotaka kusisitiza hapa ni kwamba, hakuna kitu kibaya kama wapenzi katika siku hizi kununiana ama kuudhiana. Hizi ni siku za furaha hivyo basi, hakikisha unafanya kila uwezalo kumfanya mwenza wako awe na uso wa tabasamu muda wote.
  Jamani ni hayo tu, niwatakie sikukuu njema. ILI KULINOGESHA PENZI LENU, FANYENI HAYA SIKUKUU YA IDD | VITUKO VYA MTAA
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Aug 19, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,601
  Likes Received: 82,165
  Trophy Points: 280
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 3. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #3
  Aug 19, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  ngoja nifanyie majaribio now.
   
 4. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #4
  Aug 19, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Duh, mie leo nimethibitiwa, hakuna kutoka mama Ngina kaniweka kwapani na hapa nimewekewa mikanda ya series................... LOL
   
 5. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #5
  Aug 19, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,673
  Trophy Points: 280
  Na ambao hatujaoa je????
   
Loading...