Ili kuleta tija ya vyama vingi vyama vifanye haya

mmmuhumba

JF-Expert Member
Nov 8, 2017
491
476
Tanzania ni nchi yenye vyama vingi vya kisiasa, tokea tuache mfumo wa chama kimoja mwaka 1992 na 1995 rasmi katika uchaguzi hadi leo 2022, vyama vingi vya kisiasa vimesajiliwa.

Lengo la vyama vingi ni kuchochea misingi ya demokrasia na utawala bora. Kumekuwepo na malalamiko mengi ya kisiasa na vyama vingi vikipoteza mvuto na ushindani katika siasa.

Kuna kitu cha kujifunza, vyama vya upinzani ndio jicho la chama tawala na serikali, bila upinzani hakuna serikali bora na hakuna siasa bora sio tu kwa nchi yetu bali nchi zote duniani.

Ili vyama vya siasa vilete tija hapa nchini na mataifa mengine nashauri vifanye haya:

Wajiwekeze katika kutoa huduma za jamii na uchumi. Vyama vya siasa vina ruzuku, wafadhili na vina uwezo wa kupata rasilimali fedha, mipango na rasilimalii watu, kupitia hivi wangejiwekeza katika miradi midogo midogo itayogusa maslahi ya watu kama afya, vyuo vya ufundi vijijini, yawezesha vijana na makundi maalum, vyombo vya habari na biashara.

Kwa kufanya hivi vitaweza kujitengenezea tija na kufikia umma kimaslahi badala ya kuendelea kutoa ahadi za maendeleo pasipo kuonyesha wao ni taasisi, zinaweza kujitegemea kujenga jamii bora.

Maneno matupu hayajengi ni lazima uwekezaji wa vitu na vitendo uonekane.
Wajikite katika kutatua changamoto zilizopo katika maeneo yao. Kuanzia ngazi ya kijiji hadi taifa, viongozi wa vyama vya kisiasa ni wananchi na wanafursa kubwa ya kushiriki katika changamoto za jamii.

Isiwe ni mambo ya kufanyika wakati wa kampeni kuelekea uchaguzi. Kwa misingi hii ya kizamani, vyama vitaendelea kupambana na serikali badala ya changamoto za jamii na kufanya jamii iwaone, kama kuunda taasisi zitazo shauri na kusaidia jamii na wizara kama elimu, afya, kilimo na sheria

Waendeshe vyama kwa kufuata katiba zao, kwa kufuata sauti ya watu kusimamisha viongozi na fikra jengefu. Katiba za vyama vya siasa zinajipambanua vyema ila yako makosa kama kuwapa watu uongozi kwa kuheshimu fedha na hadhi yake kitaifa, ung'ang'aniaji wa madaraka na uhujumu.

Wapo watu wengi wanahama vyama kwa kukosa kusimamiwa ahadi walizopewa na viongozi wao, kuambiwa mpishe fulani kwa kuwa anafedha ya kufanya kampeni, hii itaendelea kuwatesa na kuwajaza chuki wanaoathiriwa na mfumo huu.

Tuache kufanya siasa za nchi isitawalike ni mbaya inadhuru maisha ya wengi. Moja ya mkakati wa kisiasa ili kushika dola ni kufanya nchi isitawalike kwa kushikilia jambo lenye kuweza kuamsha hisia za watu au kuanzisha jambo lenye kuamsha hisia za watu juu ya utawala au vyama.

Ni sawa jambo linatija lakini kwa mbinu ya kufanya nchi isitawalike, inafanya nchi kuingia katika machafuko, mdololo wa uchumi, matumizi ya vyombo vya dola na watu kuchukiana kwa utofauti wa vyama. Tunapoangamiza watu tunaotaka kuwa tawala ni tatizo, lazima tuje kivingine watu waguswe ila isiwe chanzo cha machafuko, kwani watu upata kesi kwa kushambuliana na visasi.

Tukubali ukweli demokrasia ina mipaka. Kila jambo lina mipaka yake, baada ya uchaguzi tuipe muda serikali kutekeleza mipango yake, vyama vya siasa viwe ni sehemu ya utawala, kwa kukosoa, kutekeleza shughuli za serikali na viangalie wanayotaka kuyafanya yasiingilie maslahi ya serikali kiuvurugaji kiutendaji. Lazima vyama vya siasa vitambue makosa na uozo wa serikali iliyo madarakani, kwao ndio uwanja wa kusimamia, watazame haya kwa jicho kuu na kama serikali imekusudia kuleta maendeleo itasimamia vyema kuepuka upinzani kutoka kwa vyama vya upinzani na wananchi wenyewe.

Vyama vijiimarishe kwa kugusa maslahi ya vijana na watu wa tabaka la kati na chini. Vyama vya kisiasa vinadolola kugusa maslahi ya vijana na matabaka ya kundi ambalo ndio litalobeba maono ya chama na kujenga misingi ya kesho ya chama. Kugusa maslahi ya vijana ni kugusa ingini ya Taifa. Vyama vya siasa vinaongozwa na watu wenye rika kubwa na mikutanoni wanaojitokeza wengi ni wazee na watu wazima.

Lazima viji tathmini kuona kweli vinaweza kujenga taifa bora kama vinashindwa kuwajenga vijana kifikra kuunga mkono siasa zao. Ikumbukwe viongozi wazee wana ukomo mfupi kukitawala chama ni lazima warithishe itikadi zao kwa vijana na waguse maslahi ya vijana kwa kuwafungua macho kuziona fursa, kutumia vyama kuwaunganisha waingie katika mifumo rasmi ya uzalishaji mali na kuwafanya waweze kuaminiana.

Vyama vya siasa viwekeza kuanzia vijijini. Utajifunza vyama vyetu vinakimbilia sana kujijenga mijini ili vijijini vinaonekana wakati wa kuelekea uchaguzi. Tujikumbushe, vyama vikubwa vya kisiasa vimeanzishwa kutoka vijijini kwenda mijini na ndio vilivyoweza kuleta uhuru na mapinduzi. Ni lazima tujenge kwanza shina na tufate matawi. Afrika vipo vyama kila kichochoro wamefika na watu wamevipokea kivyovyote kama timu za mpira.

Vijipange kimkakati na kimbinu kuelekea uchaguzi. Nchi zetu za Afrika, wanasiasa wanapaswa kuwa na watu wenye kuweza kumudu tafiti, kushawishi watu, kujenga hoja na kubuni mbinu za kuleta ushindi na kuzuia wanavyoona wapi watashindwa. Hii itasaidia kuepuka malalamiko ya uchaguzi kutokuwa huru na haki, kuchukiana viongozi wa kisaisa baada ya uchaguzi wakati wote wanapaswa sasa kujenga nchi moja.

Vyama vitambue uzalendo wa chama sio gharama ya kadi bali mtu kukipenda chama. Watizame mifumo ya kisasa isiharibu hali ya wanachama wake na pia wajikite katika kuona namna gani watavuna wanachama na sio namna gani watakijenga chama kiuchumi, ni lazima chama chochote kipate watu ndio kipate mali na fedha.

Uvumilivu wa kisiasa na kiteknolojia ni jibu la utawala bora. Sasa hivi Afrika nchi nyingi zinaingia katika mifumo ya kieletroniki, vyama vya kisiasa vijiwekeze kwa nguvu ni mfumo bora na utakuja kubadili mfumo wa upigaji kura. Wanasiasa wa wakubaliane na matokeo na wajipange upya, wasiwe watu wenye kuwaza kuibiwa kura na hii inafanya nchi, chama kinaposhika dola, upinzani kuendelea na siasa ya chuki inayoleta ugomvi kati yake na chama tawala.

Ndugu zangu viongozi wa vyama vya kisiasa Tanzania na Afrika, ni lazima tutambue sisi wote tunataka kujenga nchi moja, tuwe watu wenye mikakati na kujipanga vyema badala ya kujiingiza katika migogoro inayokwamisha nchi na kuchafua amani iliyopo.

Wito wangu kwa vyama vya upinzani, vitambue bila wao hakuna jicho na mzani wa kupima ubora wa serikali iliyopo, ni lazima watengeneze propaganda za pale iliposhindwa serikali ila watu waone umahili wao.

Wito wangu kwa vyama tawala, vitambue kushika dola, kutumia nguvu na akili chache wakati wa uchaguzi ni uamuzi wao wenyewe, endapo watashindwa kuleta maendeleo katika Taifa, ni wao wenye watakao kuwa wanajitengenezea ukomo wa kutawala.
 
Iyo Ruzuku unayosema unajua ni sh, ngapi? Uoatikanaji wake? Kazi yake?
Asante ndugu ichumu lya, Chama ni taasisi kinao uwezo wa kutafuta rasilimali fedha rasilimali mipango na rasilimali watu. Wajiwekeze kugusa maslahi ya wanachama wao na wananchi. Hilo ndio kubwa kulielewa hii rudhuku ni ziada tu, kubwa ni chama kimeingia katika siasa ni lazima kijijenge chenyewe.
Ruzuku ni fedha inayotolewa na serikali kwa chama kwa ajili ya kusaidia chama kuendesha shughuli zake za chama na huwa kuna sifa ikiwepo kupata asilimia afikiwa ya kura ikiwemo kushinda ubunge, udiwani. Kwahiyo ruzuku kwenye vyama ni ziada kikubwa ni chama kimejipangaje.
 
Asante ndugu ichumu lya, Chama ni taasisi kinao uwezo wa kutafuta rasilimali fedha rasilimali mipango na rasilimali watu. Wajiwekeze kugusa maslahi ya wanachama wao na wananchi. Hilo ndio kubwa kulielewa hii rudhuku ni ziada tu, kubwa ni chama kimeingia katika siasa ni lazima kijijenge chenyewe.
Mimi nimeuliza tu nijibu kwanza alafu tusogee mbele maana naona unataka chama kifanye kazi ya serikali inayokusanya kodi. Lengo la chama sio biashara chama cha siasa asa chama kikuu cha Upinzani ni kioo cha chama Tawala kinatakiwa kuwa na sera mbadala kuchallenge chama tawala
 
Mimi nimeuliza tu nijibu kwanza alafu tusogee mbele maana naona unataka chama kifanye kazi ya serikali inayokusanya kodi. Lengo la chama sio biashara chama cha siasa asa chama kikuu cha Upinzani ni kioo cha chama Tawala kinatakiwa kuwa na sera mbadala kuchallenge chama tawala
Ruzuku inategemea asilimia ya chama kilivyopata katika uchaguzi mkuu.
Vyama vya kisiasa vinawezesha miradi, kuchangia ujenzi, kutoa vifaa tiba,na vya kielimu, kutoa mafunzo ya ujasiriliamali mpaka kwenye majanga vinajitoa na mengi mengi yanayogusa maslahi ya umma, huku ndio kuweka uhai wake katika nchi yoyote. Vyama vinaofisi vina miradi na wafadhiri.
Swali?
1. Ipi ni faida ya wewe kuwa mwanachama wa chama husika?
2. Chama kinawezaje kugusa maslahi ya wanachama wake na wananchi?
3. Lipi ni lengo la chama husika katika hiyo nchi?
 
Back
Top Bottom