Ili kukabiliana na upungufu wa mask (barakoa) wizara ya afya itoe muongozo wa mask za namna hii kama ikionekana zinaweza kufaa

Conwel Ngani

Senior Member
Sep 16, 2018
134
149
Kitendo cha mabeberu kuanza kuibiana mask inaonekana kuna upungufu mkubwa sana wa mask duniani kwa namna hiyo napenda kuwasilisha mawazo yangu kwa wizara ya afya kuangalia mask za namna hii na kutoa muongozo kwa matumizi ya kawaida ya mitaani na majumbani kama ikioneka zinaweza kufaa HASA KUZUIA MATE YANATOKA WAKATI WA KUONGEA.

Wizara iangalie ni kitambaa cha namna gani kinaweza kutumika na kitumike katika layers ngapi ili pia kuweza kuruhusu mvaaji kupumua vizuri.

KWANINI MASK ZA NAMNA HII?

1. Gharama, mask za namn hii gharama yake ni ndogo, bila kujali aina ya kitambaa, gharama za vifaa haitaweza kuzidi shilingi 300 kwa mask moja hivyo naamini kila mtanzania ataweza kumudu. Hata kama zitashonwa na fundi cherehani gharama haiwezi kuzidi 1000 maana ni kazi ya dk 10 tu.

2. Zinaweza kufuliwa mara kwa mara na mtumiaji husika

3. Mask special (surgical mask) waachiwe wahudumu wa afya na wale walioathirika maana ni adimu.

4. Zinaweza kupatikana kirahisi, tuna mafundi cherehani wengi mitaani wamejaa. Kama zitashonwa na mafundi cherehani basi wizara ishauri namna bora mvaaji kuzisafisha kabla hajavaa maana kama fundi cherehani husika kaathirika itakuwa hatari. Kama watatumika mafundi cherehani naamini wizara itatoa muongozo bora kwa kushirikiana na wakuu wa wilaya na serikali za mitaa ili kuondokana na hiyo risk.

5. Mafunzo yaweza kutolewa kwenye mitandao ya kijamii ili kila mtu ajitengenezee mwenyewe nyumbani kwake kwa kutumia sindano ya mkono. Ila watu wa maduka ya vitambaa wapewe muongozo wa kukata kwa vipande vidogo vidogo na kuwe na bei elekezi ni matumaini yangu haitazidi 200 kwa kipande. Hapa pia wizara itoe muongozo wa namna ya kuzisafisha kabla ya matumizi.

6. Viwanda vya nguo vinaweza kuruhusiwa na kupewa muongozo wa namna bora ya kuziandaa.

7. Zinaweza kutengenezwa kwa saizi mbalimbali

Nimejaribu kushona moja pichani kuonyesha nana inavyoweza kumkaa mvaaji.

Pamoja katika mapambano ya Corona

Conwel Ngani
Ekwueme Fashion and Interior Design

Bukoba
DSC01650.JPG
View attachment 1418533 Screenshot_20200414-064036~2.png DSC01651.JPG

UPDATE:
ASANTE SERIKALI KWA KUSIKIA HILI, KUMBE NA NYIE MLIKUWA KWENYE MCHAKATO.
Wananchi kufundishwa kutengeneza barakoa - JamiiForums
 
Ya nini kuhangaika na yote hayo?

Tumia kanga au kitenge inatosha. Tafuta 'rubberband' kusaidia ikae vizuri, kazi imekwisha. Na ikiwezekana, tumia matone machache ya pombe juu yake, coronavirus haponi. Ndio, pombe ina'eveporate' haraka, beba kichupa kidogo kulowanisha sehemu ya mdomo na pua tu.

Hapana, hutalewa, hii unatumia kwa mda mfupi wakati ukiwa kwenye maeneo hatarishi.

Kesho nawasilisha ombi la 'patent' juu ya uvumbuzi huu.

Utakuja hapa ubishe, lakini ukweli ni kwamba vinaweza kuwa bora kuliko hizo barakoa.
 
Ya nini kuhangaika na yote hayo?

Tumia kanga au kitenge inatosha.

Utakuja hapa ubishe, lakini ukweli ni kwamba vinaweza kuwa bora kuliko hizo barakoa.
Mawazo yako ni mazuri, ila kuna ambae ataona kitenge na shuka la pamba na mzigo maana yupo atakaye shauri tutumie shuka la cotton
 
Ya nini kuhangaika na yote hayo?

Tumia kanga au kitenge inatosha.
Tafuta 'rubberband' kusaidia ikae vizuri, kazi imekwisha. Na ikiwezekana, tumia matone machache ya pombe juu yake, coronavirus haponi. Ndio, pombe ina'eveporate' haraka, beba kichupa kidogo kulowanisha sehemu ya mdomo na pua tu.

Hapana, hutalewa, hii unatumia kwa mda mfupi wakati ukiwa kwenye maeneo hatarishi.

Kesho nawasilisha ombi la 'patent' juu ya uvumbuzi huu.

Utakuja hapa ubishe, lakini ukweli ni kwamba vinaweza kuwa bora kuliko hizo barakoa.
Kuna watu kutembea wanapepesuka road
 
Bora umeongeza nyama kidogo
 
Back
Top Bottom