Ili Kujua Mtoto Wake Sio Shoga, Amlazimisha Afanye Mapenzi na Kahaba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ili Kujua Mtoto Wake Sio Shoga, Amlazimisha Afanye Mapenzi na Kahaba

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by NGULI, Dec 24, 2009.

 1. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #1
  Dec 24, 2009
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  [​IMG]
  Thursday, December 24, 2009 4:39 AM
  Baba mmoja nchini Australia ambaye alikuwa akitilia shaka urijali wa mtoto wake mwenye umri wa miaka 14 ameingia matatani baada ya kumlazimisha mtoto wake afanye mapenzi na kahaba aliyemkodishia.Baba mmoja wa nchini Australia ameingia matatani baada ya kumlazimisha mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka 14 afanye mapenzi na kahaba kwakuwa alikuwa akifikiria mtoto wake ni shoga.

  Polisi wa Australia walisema kuwa baba huyo kutoka katika mji wa Rockhampton katika jimbo la Queensland, alimleta kahaba kwenye sherehe ya kifamilia ya nyama choma na kisha kuandaa chumba kwenye hoteli iliyopo karibu na nyumba yake ili kutesti urijali wa mtoto wake.

  Kwa mujibu wa gazeti la The Morning Bulletin, baba huyo alimpeleka mwanae kwenye chumba hicho na kisha alimlipa kahaba huyo dola 50 afanye mapenzi na mwanae.

  Baba huyo alisubiria nje ya chumba cha hoteli hiyo baada ya kumwambia mtoto wake huyo kuwa anataka ushahidi wa kondomu iliyotumika kuthibitisha wamefanya mapenzi.

  Baba huyo alifunguliwa kesi na kufikishwa mahakamani lakini mahakama ilisema kuwa hakuna ushahidi wa kutosha kumtia hatiani baba huyo kwa tukio hilo ambalo limehesabika ni la ubakaji.

  Mahakama ilipewa ushahidi wa mama wa mtoto huyo ambaye alisema kuwa alimhoji mwanae kilichotokea ndani ya chumba cha hoteli.

  "Awali hakutaka kuniambia chochote lakini baadae aliniambia kuwa baba yake alimchukua na kumpeleka hotelini ambako alitakiwa kufanya mapenzi na kahaba", mama wa mtoto huyo alinukuliwa na gazeti la Morning Bulletin.

  "Hakuendelea kuelezea badala yake alianza kulia".

  Waendesha mashtaka wa polisi waliiambia mahakama kuwa walipata taarifa za tukio hilo baada ya baba huyo kupiga simu kwenye kitengo cha watoto akiulizia kwanini hawajachukua hatua yoyote wakati alishatoa taarifa kuwa mtoto wake wa kiume anamnyanyasa kijinsia mdogo wake wa kiume.

  Baba huyo alimwambia afisa wa polisi aliyepokea simu hiyo kuwa alijaribu kutatua tatizo hilo kwa kumpeleka mtoto wake kwa kahaba.

  Kitendo hicho kilimponza baba huyo aliyejikuta akifunguliwa mashtaka ya kufanya kitendo kilichopelekea kubakwa kwa mtoto wake.

  Juhudi za polisi kumtafuta kahaba anayedaiwa kufanya mapenzi na mtoto huyo bado hazijafanikiwa

  source: nifahamishe.com
   
 2. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #2
  Dec 24, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  merry x-mass mpwaaaaz!:d
   
 3. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #3
  Dec 24, 2009
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  The same to u. Xspin amelewa hapa.
   
 4. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #4
  Dec 24, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Vp Nguli jaribio lilifanikiwa? Dogo aliweza lakini kubinjuka?
   
 5. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #5
  Dec 24, 2009
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Ha ha ha ha, hili swala la ushoga linashika hatamu.
   
 6. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #6
  Dec 24, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Sasa huyo mtoto anaacha kuwafuata machangudoa?
   
 7. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #7
  Dec 24, 2009
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  du huyu baba is a real realist
   
 8. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #8
  Dec 24, 2009
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Dogo kaharibu..
  Angekuwa anamshtua Mshua vipi leo unitesti?
   
 9. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #9
  Dec 24, 2009
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  teh teh teh...wazazi wengine 'finyu'...
   
 10. B

  Babuji Senior Member

  #10
  Dec 24, 2009
  Joined: Nov 27, 2008
  Messages: 198
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mhh kweli si mchezo mdingi anatest kama mtoto wake si rizki au la
   
 11. Ulate

  Ulate Member

  #11
  Dec 24, 2009
  Joined: Dec 20, 2007
  Messages: 66
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mzee hapo alichemsha.kuna mashoga wanamlala mtu vilevile
   
Loading...