Ili Kujenga CHADEMA ya kushindana na CCM ya sasa, Tafuteni uongozi mpya, Waondoeni Mwenyekiti Mbowe, Makamu Mwenyekiti Lissu na Katibu Mnyika

Mbona siku hizi hamongelei RUZUKU ya CHADEMA kwamba Mh. Mbowe anaila tu.
SACCOS inanuka Madeni👇👇👇

IMG_20220412_211645.jpg
 
Wewe jamaa huijui chadema umekurupuka hiki ni chama Cha wachaga walikiasisi wakati wanakunywa mbege baada ya kujua kuwa hawewezi kupewa urais kwa sababu za ukabila wao

USSR

Haichekeshi.
 
Mimi ni mpenda Maendeleo ya Tanzania, na kwa sababu sasa Ccm inaisimamia vizuri Serikali, na Serikali inasimamia vizuri Utekelezaji wa miradi ya Maendeleo ninasuport Serikali ya Awamu ya sita
kama unasapot ishaur serikal c chama wakat we huna chama.Pilipil hauli wawashwa nin?Hao uwaonao hawafai ndiyo walikivusha chama chao ktk wakati mgumu ule wabunge wahama,madiwani nk.Hakikufa unadhan kitakufa sasa? Think twice
 
Hii ni point kubwa sana wakati wao wanalia CCM kubaki madarakani Kwa Muda mrefu wanasahau kwamba Viongozi wao wako madarakani Kwa Muda mrefu Kwa kisingizio kwamba wanaogopa Mamluki wasipandikizwe kwenye chama,

Ndo hivo hivo hata CCM wataendelea kuwa madarakani Kwa kisingizio cha kuogopa Mamluki kupandikizwa kwenye nchi Kwa Mgongo wa Upinzani!

Wananchi wanataka mabadiliko chanya siyo hasi , wakipata chama makini CCM inaondoka ila sasa bado wana hisi na CDM bado sana,

ACT hao ndo wachanga Kabisa ..

Acheni janja janja fanyeni taratibu wananchi wawaamini,

Mwenye kiti tu kuitwa Mwenyekiti hataki kuachia Miaka 25 sasa je akiitwa Mheshimiwa Rais si atakaa miaka 40?

We don’t believe you and we don’t trust you

Jenga misingi muaminike

Britanicca

Cdm wajenge misingi waaminike na wananchi au vyombo vya dola? Maana sasa hivi sio wananchi wanaamua nani akae madarakani, bali vyombo cya dola ndio vinaamua nani akae madarakani. Uzuri wananchi nao wameshaamka wengi hawana muda wa kwenda kupoteza muda kwenye box la kura. Machafuko tu ndio yatawatoa CCM.
 
Nimemsoma jamaa nikaona 0 tu.Amexahau hawa ndyo walipambana kukiimarisha chama chao wakati mgumu wabunge na madiwani wengi waliunga mkono juhudi wakati wa mazingira magumu ya siasa.Kama walipita salama enzi leo kunani?
Unasema walikiimarisha chama? mbona chama kimekufa Mkuu, kwa sasa imebaki jina tu, hivi ile CHADEMA ya Dr WS ndio utalinganisha na hii? badilisheni uongozi
 
Ni ukweli mchungu kwa kwa Makamanda wa Chadema, na hakuna Kamanda atakayekubali kuwa Chadema ya sasa imekwisha, haina uwezo wa kuleta upinzani kwa Chama tawala ambacho kimepata Makamu Mwenyekiti mpya.

Kila movement ambayo CHADEMA mnafanya kwa sasa inafeli vibaya saana, Join the chain imefeli vibaya saana, Chadema ya sasa inazidiwa hata na ACT ya bwana yule. CHADEMA ya kweli ilikuwa ile ya Dr Wilbroad Slaa tu, baada ya hapo CHADEMA imekuwa ikijongea kaburini kidogo kidogo na msipo anza upya baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 Chama chenu hakitakuwa na utofauti na kile chama cha yule jamaa wa kugawa ubwabwa kwenye mikutano ya kampeni.

Mheshimiwa Freeman Mbowe, kama Mwenyekiti wa CHADEMA kwa sasa ni muda wake wa kupumzika, amekifanyia mambo makubwa CHADEMA na atakumbukwa kwa mchango wake katika siasa za upinzani, lakini Mheshimiwa Mbowe kwa sasa hana jipya la kuweza kuwaambia Watanzania wakakiunga mkono CHADEMA, hakuna Mtanzania atakayeunga mkono siasa za matukio, Vijana wengi sasa ni wasomi wanaotaka sera na sio matukio, Mbowe alikifaa Chama kipindi hicho cha siasa za harakati. CHADEMA mnahitaji Mwenyekiti mpya na hii itakuwa njia bora ya kuonyesha mna demokrasia ya kweli, Mkipata mwenyekiti mpya atajenga CHADEMA ili kuja kushindana na CCM miaka 15- 20 ijayo.

Ndugu John Mnyika , kama katibu wa CHADEMA , najua makamanda wote mnajua ukweli kuwa Mnyika mnamlazimisha tu kuendelea kuwa Katibu wa Chama lakini yeye muda mrefu amekuwa anataka kupumzika, Mnyika si mtu wa siasa za kiharakati wala si muumini wa siasa za matukio. Mnyika yule wa kujenga hoja akili yake sasa iko mapumzikoni mwili tu umebaki CHADEMA, Mnyika hawezi kukisaidia CHADEMA kwa sasa. Mnyika ameamua kukaa kimya, ni bora mkamuacha apumzike tafuteni Katibu mpya wa kuweza angalau kufikia uwezo wa Komredi Chongolo

Ngugu Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti wa Chama, huyu ni Muumini wa siasa za kiharakati na siasa za matukio ambazo kwa sasa hazina nafasi katika Tanzania inayoendesha Siasa za kistarabu, siasa za utu na kuheshimiana, CCM wamepata Makamu Mwenyekiti hodari na nguli wa siasa za Tanzania, CHADEMA mnahitaji kupata Makamu Mwenyekiti ambaye ana weza fikia hata robo ya uwezo wa Kinana, najua ni ngumu kumpata mtu mwenye uzoefu na uwezo wa Komredi Kinana. Muacheni Ndugu Lissu aendelee na ajira yake UN, kwa aliyopitia ndugu yetu Lissu anahitaji muda mwingi wa kupumzika na kumtumikia Mwenyezi Mungu.

Siasa za kwenye mitandao huko the space na twitter hazitawasaidia kwa sasa.

Kuanza upya haijawahi kuwa vibaya, hata yule ndugu yenu wa ACT alikubali kuanza upya.

MUNGU IBARIKI TANZANIA , MUNGU MBARIKI RAIS WETU SAMIA SULUHU HASSAN.
baada ya jamaa kutoka jela hizi mada za kumuondoa kwenye uenyekiti zimeanza tena😁😁😁😁
 
CCM toka kipindi kile..ni chama kinachotegemea dola. Mtaani hakuna mtu ana hamu na CCM. Watu wamekichoka.
 
Bado Mbowe ni mtu muhimi sana CHADEMA! Kinachopaswa ni kuangalia maslahi ya chma siyo kuangalia mtu.
 
Cdm wajenge misingi waaminike na wananchi au vyombo vya dola? Maana sasa hivi sio wananchi wanaamua nani akae madarakani, bali vyombo cya dola ndio vinaamua nani akae madarakani. Uzuri wananchi nao wameshaamka wengi hawana muda wa kwenda kupoteza muda kwenye box la kura. Machafuko tu ndio yatawatoa CCM.
Hiiii.....

Si dhalimu ameshaondoka?

Sasa hii hofu yote ya nini?
 
Ni ukweli mchungu kwa kwa Makamanda wa Chadema, na hakuna Kamanda atakayekubali kuwa Chadema ya sasa imekwisha, haina uwezo wa kuleta upinzani kwa Chama tawala ambacho kimepata Makamu Mwenyekiti mpya.

Kila movement ambayo CHADEMA mnafanya kwa sasa inafeli vibaya saana, Join the chain imefeli vibaya saana, Chadema ya sasa inazidiwa hata na ACT ya bwana yule. CHADEMA ya kweli ilikuwa ile ya Dr Wilbroad Slaa tu, baada ya hapo CHADEMA imekuwa ikijongea kaburini kidogo kidogo na msipo anza upya baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 Chama chenu hakitakuwa na utofauti na kile chama cha yule jamaa wa kugawa ubwabwa kwenye mikutano ya kampeni.

Mheshimiwa Freeman Mbowe, kama Mwenyekiti wa CHADEMA kwa sasa ni muda wake wa kupumzika, amekifanyia mambo makubwa CHADEMA na atakumbukwa kwa mchango wake katika siasa za upinzani, lakini Mheshimiwa Mbowe kwa sasa hana jipya la kuweza kuwaambia Watanzania wakakiunga mkono CHADEMA, hakuna Mtanzania atakayeunga mkono siasa za matukio, Vijana wengi sasa ni wasomi wanaotaka sera na sio matukio, Mbowe alikifaa Chama kipindi hicho cha siasa za harakati. CHADEMA mnahitaji Mwenyekiti mpya na hii itakuwa njia bora ya kuonyesha mna demokrasia ya kweli, Mkipata mwenyekiti mpya atajenga CHADEMA ili kuja kushindana na CCM miaka 15- 20 ijayo.

Ndugu John Mnyika , kama katibu wa CHADEMA , najua makamanda wote mnajua ukweli kuwa Mnyika mnamlazimisha tu kuendelea kuwa Katibu wa Chama lakini yeye muda mrefu amekuwa anataka kupumzika, Mnyika si mtu wa siasa za kiharakati wala si muumini wa siasa za matukio. Mnyika yule wa kujenga hoja akili yake sasa iko mapumzikoni mwili tu umebaki CHADEMA, Mnyika hawezi kukisaidia CHADEMA kwa sasa. Mnyika ameamua kukaa kimya, ni bora mkamuacha apumzike tafuteni Katibu mpya wa kuweza angalau kufikia uwezo wa Komredi Chongolo

Ngugu Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti wa Chama, huyu ni Muumini wa siasa za kiharakati na siasa za matukio ambazo kwa sasa hazina nafasi katika Tanzania inayoendesha Siasa za kistarabu, siasa za utu na kuheshimiana, CCM wamepata Makamu Mwenyekiti hodari na nguli wa siasa za Tanzania, CHADEMA mnahitaji kupata Makamu Mwenyekiti ambaye ana weza fikia hata robo ya uwezo wa Kinana, najua ni ngumu kumpata mtu mwenye uzoefu na uwezo wa Komredi Kinana. Muacheni Ndugu Lissu aendelee na ajira yake UN, kwa aliyopitia ndugu yetu Lissu anahitaji muda mwingi wa kupumzika na kumtumikia Mwenyezi Mungu.

Siasa za kwenye mitandao huko the space na twitter hazitawasaidia kwa sasa.

Kuanza upya haijawahi kuwa vibaya, hata yule ndugu yenu wa ACT alikubali kuanza upya.

MUNGU IBARIKI TANZANIA , MUNGU MBARIKI RAIS WETU SAMIA SULUHU HASSAN.
Sasa wewe ndio wkt wa kushukuru huu ili chama unaochoamini kiweze kufanikiwa zaidi. Na hawa waendelee kufeli. Mbon unataka kuwasaidia?
 
Napendekeza wewe ugombee uenyekiti.
 
Back
Top Bottom