Ili Kujenga CHADEMA ya kushindana na CCM ya sasa, Tafuteni uongozi mpya, Waondoeni Mwenyekiti Mbowe, Makamu Mwenyekiti Lissu na Katibu Mnyika

Kujenga nchi tunahitaji upinzani Imara, sio upinzani huu wa sasa uliopotea
Upinzani ulipata kibano kikali kwa miaka yooote ya mwendazake, wengine wakaponea chupuchupu kuuwawa, wengine ni wakimbizi n.k kwa hiyo wanahitaji muda ku recover. Unapowalaumu ni kama walilala makusudi.
 
Ni ukweli mchungu kwa kwa Makamanda wa Chadema, na hakuna Kamanda atakayekubali kuwa Chadema ya sasa imekwisha, haina uwezo wa kuleta upinzani kwa Chama tawala ambacho kimepata Makamu Mwenyekiti mpya.

Kila movement ambayo CHADEMA mnafanya kwa sasa inafeli vibaya saana, Join the chain imefeli vibaya saana, Chadema ya sasa inazidiwa hata na ACT ya bwana yule. CHADEMA ya kweli ilikuwa ile ya Dr Wilbroad Slaa tu, baada ya hapo CHADEMA imekuwa ikijongea kaburini kidogo kidogo na msipo anza upya baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 Chama chenu hakitakuwa na utofauti na kile chama cha yule jamaa wa kugawa ubwabwa kwenye mikutano ya kampeni.

Mheshimiwa Freeman Mbowe, kama Mwenyekiti wa CHADEMA kwa sasa ni muda wake wa kupumzika, amekifanyia mambo makubwa CHADEMA na atakumbukwa kwa mchango wake katika siasa za upinzani, lakini Mheshimiwa Mbowe kwa sasa hana jipya la kuweza kuwaambia Watanzania wakakiunga mkono CHADEMA, hakuna Mtanzania atakayeunga mkono siasa za matukio, Vijana wengi sasa ni wasomi wanaotaka sera na sio matukio, Mbowe alikifaa Chama kipindi hicho cha siasa za harakati. CHADEMA mnahitaji Mwenyekiti mpya na hii itakuwa njia bora ya kuonyesha mna demokrasia ya kweli, Mkipata mwenyekiti mpya atajenga CHADEMA ili kuja kushindana na CCM miaka 15- 20 ijayo.

Ndugu John Mnyika , kama katibu wa CHADEMA , najua makamanda wote mnajua ukweli kuwa Mnyika mnamlazimisha tu kuendelea kuwa Katibu wa Chama lakini yeye muda mrefu amekuwa anataka kupumzika, Mnyika si mtu wa siasa za kiharakati wala si muumini wa siasa za matukio. Mnyika yule wa kujenga hoja akili yake sasa iko mapumzikoni mwili tu umebaki CHADEMA, Mnyika hawezi kukisaidia CHADEMA kwa sasa. Mnyika ameamua kukaa kimya, ni bora mkamuacha apumzike tafuteni Katibu mpya wa kuweza angalau kufikia uwezo wa Komredi Chongolo

Ngugu Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti wa Chama, huyu ni Muumini wa siasa za kiharakati na siasa za matukio ambazo kwa sasa hazina nafasi katika Tanzania inayoendesha Siasa za kistarabu, siasa za utu na kuheshimiana, CCM wamepata Makamu Mwenyekiti hodari na nguli wa siasa za Tanzania, CHADEMA mnahitaji kupata Makamu Mwenyekiti ambaye ana weza fikia hata robo ya uwezo wa Kinana, najua ni ngumu kumpata mtu mwenye uzoefu na uwezo wa Komredi Kinana. Muacheni Ndugu Lissu aendelee na ajira yake UN, kwa aliyopitia ndugu yetu Lissu anahitaji muda mwingi wa kupumzika na kumtumikia Mwenyezi Mungu.

Siasa za kwenye mitandao huko the space na twitter hazitawasaidia kwa sasa.

Kuanza upya haijawahi kuwa vibaya, hata yule ndugu yenu wa ACT alikubali kuanza upya.

MUNGU IBARIKI TANZANIA , MUNGU MBARIKI RAIS WETU SAMIA SULUHU HASSAN.
Ushauri mzuri, na sisi CCM tuwaondoe KINANAA na MAKAMBA, Tuondoe Wazee wote na Rais asiwe mwenyekiti wa CHAMA, turudishe viwanja vyote vysa mipira ambavyo ni vya wananchi tukachukua, pia maeneo ya wazi tuliyoyapoka tuyarudishe.
Baada ya hapo sasa tuwaambie CHADEMA wamuondoe Mbowe, HALIMA MDEE awe Mwenyekiti, Esther bulaya Katibu mkuu na Jesca Kishoa mhazini,
 
Ni ukweli mchungu kwa kwa Makamanda wa Chadema, na hakuna Kamanda atakayekubali kuwa Chadema ya sasa imekwisha, haina uwezo wa kuleta upinzani kwa Chama tawala ambacho kimepata Makamu Mwenyekiti mpya.

Kila movement ambayo CHADEMA mnafanya kwa sasa inafeli vibaya saana, Join the chain imefeli vibaya saana, Chadema ya sasa inazidiwa hata na ACT ya bwana yule. CHADEMA ya kweli ilikuwa ile ya Dr Wilbroad Slaa tu, baada ya hapo CHADEMA imekuwa ikijongea kaburini kidogo kidogo na msipo anza upya baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 Chama chenu hakitakuwa na utofauti na kile chama cha yule jamaa wa kugawa ubwabwa kwenye mikutano ya kampeni.

Mheshimiwa Freeman Mbowe, kama Mwenyekiti wa CHADEMA kwa sasa ni muda wake wa kupumzika, amekifanyia mambo makubwa CHADEMA na atakumbukwa kwa mchango wake katika siasa za upinzani, lakini Mheshimiwa Mbowe kwa sasa hana jipya la kuweza kuwaambia Watanzania wakakiunga mkono CHADEMA, hakuna Mtanzania atakayeunga mkono siasa za matukio, Vijana wengi sasa ni wasomi wanaotaka sera na sio matukio, Mbowe alikifaa Chama kipindi hicho cha siasa za harakati. CHADEMA mnahitaji Mwenyekiti mpya na hii itakuwa njia bora ya kuonyesha mna demokrasia ya kweli, Mkipata mwenyekiti mpya atajenga CHADEMA ili kuja kushindana na CCM miaka 15- 20 ijayo.

Ndugu John Mnyika , kama katibu wa CHADEMA , najua makamanda wote mnajua ukweli kuwa Mnyika mnamlazimisha tu kuendelea kuwa Katibu wa Chama lakini yeye muda mrefu amekuwa anataka kupumzika, Mnyika si mtu wa siasa za kiharakati wala si muumini wa siasa za matukio. Mnyika yule wa kujenga hoja akili yake sasa iko mapumzikoni mwili tu umebaki CHADEMA, Mnyika hawezi kukisaidia CHADEMA kwa sasa. Mnyika ameamua kukaa kimya, ni bora mkamuacha apumzike tafuteni Katibu mpya wa kuweza angalau kufikia uwezo wa Komredi Chongolo

Ngugu Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti wa Chama, huyu ni Muumini wa siasa za kiharakati na siasa za matukio ambazo kwa sasa hazina nafasi katika Tanzania inayoendesha Siasa za kistarabu, siasa za utu na kuheshimiana, CCM wamepata Makamu Mwenyekiti hodari na nguli wa siasa za Tanzania, CHADEMA mnahitaji kupata Makamu Mwenyekiti ambaye ana weza fikia hata robo ya uwezo wa Kinana, najua ni ngumu kumpata mtu mwenye uzoefu na uwezo wa Komredi Kinana. Muacheni Ndugu Lissu aendelee na ajira yake UN, kwa aliyopitia ndugu yetu Lissu anahitaji muda mwingi wa kupumzika na kumtumikia Mwenyezi Mungu.

Siasa za kwenye mitandao huko the space na twitter hazitawasaidia kwa sasa.

Kuanza upya haijawahi kuwa vibaya, hata yule ndugu yenu wa ACT alikubali kuanza upya.

MUNGU IBARIKI TANZANIA , MUNGU MBARIKI RAIS WETU SAMIA SULUHU HASSAN.
Aliteuliwa Kinana kuwa makamu mwenyekiti baada ya kuonekana chama chenu hakina tena watu wenye uwezo wa kujaza hiyo nafasi.
Hizo porojo za Mbowe,Lissu au Mnyika kutokufaa kuwa top leaders wa CDM haijaanza leo,walioziasisi wameshatangulia mbele ya Muumba.Nawe ni bora tu ukajiandaa kisaikolojia.CDM is there to stay and there is nothing you can do.Subiri mchakamchaka na marathon kama una pumzi.
 
Back
Top Bottom