Ili kuipa hadhi Elimu, Wakuu wa Idara na Taasisi wawe na elimu kuzidi wafanyakazi walio chini yao.

Trust None

JF-Expert Member
Feb 12, 2018
1,260
4,415
Unapoongoza watu ambao wanakuzidi elimu kuna changamoto yake, unakuwa hujiamini, unakuwa mwoga na hatimaye kushindwa kufanya maamzi sahihi.

Ifike mahala wafanyakazi waliojiendeleza kielimu wapewe ukuu wa idara.

Mfano:
1- Walimu Wakuu wa shule za musingi wawe na elimu ya degree, wenye degree wakiisha ndipo wapewe wenye diploma. Kuna walimu wengi wa Grade A waliojiendeleza lakini ukuu wa shule wanapewa wa Cheti huku wa degree wakiachwa.

2- Wakuu wa Shule za Sekondari wawe na elimu ya masters, hawa wakiisha basi wapewe wenye degree lakini wawe na uzoefu wa kazi angalau zaidi ya miaka kumi.

3- Wakuu wa mahosipitali na vituo vya afya wawe na elimu ya juu kuliko wafanyakazi wengine katika kituo husika.

NB. Hili pia litumike katika idara zote ili Kuipa hadhi elimu.
 
Mkuu unazungumzia Elimu ipi?
Umesema na Taasisi nyingine za Afya,Madini,Misitu,Nk,nk
Unajua Serikalini Elimu ya Degree ni Kubwa mno na ndio inayotambulika ktk Kufanya kazi!
Hizo nyingine ni Ziada,Na Mara nyingi haziendani na Kila Wanachokifanya...
Masters
Nyingi zinakuwa ni za Management tuu!
Mfano Ukute Mtu kasomea Bachelor degree ya Pharmacy,Halafu Masters ya Pharmacy?
Nashauri Masters iwe ya Uongozi kama tayari ana Technical skills ya kazi yake!
Nyingine ni short courses tuu!
Sababu huyu Mtu anakwenda Ku manage resources yaani watu,Vitu nk!
 
Awamu tano elimu imeshuka sana hadhi ajira hamna , unasoma na kujiendeleza mishahara haipandi, wasomi wamekuwa ni watu wa majalalani .
Wasomi wanadaiwa na bodi ya mikopo fedha kibao hafu wanaendesha bajaji na boda boda sijui watalipa vipi deni.
Wasomi wanazungusha kalanga, na machungwa na parachichi.
 
Awamu tano elimu imeshuka sana hadhi ajira hamna , unasoma na kujiendeleza mishahara haipandi, wasomi wamekuwa ni watu wa majalalani .
Wasomi wanadaiwa na bodi ya mikopo fedha kibao hafu wanaendesha bajaji na boda boda sijui watalipa vipi deni.
Wasomi wanazungusha kalanga, na machungwa na parachichi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Awamu hii inabidi hili liangaliwe upya
 
Back
Top Bottom