Ili kuharakisha maendeleo kwanini wilaya zisipewe mamlaka zikiwa na wakuu wa wilaya wa kuchaguliwa?

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
15,658
20,889
Sun Tzu aliwahi kusema, "Kuongoza jeshi kubwa hakuna tofauti na kuongoza jeshi dogo, unachotakiwa ni kuligawa jeshi lako."

Kwa kawaida kitu ambacho kipo centralized sana huwa ni kazi sana kukisimamia kwa ufanisi. Urasimu na ukwamishaji huwa mwingi sana. Na hata mifano inaonyesha kuwa ni kazi kwa nchi kuendelea kama ikiwa centralized kama hii yetu. Na uzuri ni kuwa ili kudecentralize nchi si mpaka iwe na mfumo wa majimbo. Nchi nyingi za Ulaya ziko decentralized.

Ingekuwa vema sana tungefanya decentralization hii nchi. Kuwe na mkuu wa wilaya anayechaguliwa na wananchi, ambaye atakuwa ndiye kiongozi wa wilaya. Kunakuwa pia na baraza la wilaya ambalo linaact kama bunge la wilaya. Hii serikali inakuwa na mamlaka ya kupanga bajeti yake, miradi yake, nk. Pesa inakuwa inapata kutokana na mapato yake na gawio kutoka serikali kuu, gawio ambalo linazingatia vigezo kadha wa kadha.

Jambo kama hili litaharakisha maendeleo, uwajibikaji na ushiriki wa wananchi katika kupanga mipango yao ya maendeleo. Mkuu wa wilaya atawajibika sababu anajua wananchi wanaweza kumtoa muda wowote.

Kwa nionavyo hii system yetu ambayo ipo highly centralized itakuwa ni ngumu sana kwetu kupata maendeleo. Unaonaje, kudecentralize madaraka kunaweza harakisha maendeleo?
 
Back
Top Bottom