Bila bila
JF-Expert Member
- Dec 20, 2016
- 21,474
- 37,745
Ni Jambo la kawaida Kwa mzalendo kufanya Yale yaliyo juu ya uwezo wake. CAG ametoa ripoti kwamba fedha katika mashirika na Taasisi mbalimbali za serikali zimeliwa na wakubwa. Ni dhahiri fedha hizo zilizoliwa zimewaongezea maendeleo binafsi viongozi wetu. Sisi tulio tayari kuona viongozi wetu wanaishi maisha mazuri tunaomba Mheshimiwa Mwigulu kama kawaida yako, shusha Mswada mpya wa fedha kwenye Bunge hili la bajeti ili kufikia July 2023 tuanze kutozwa Tozo kubwa kidogo ili kufidia fedha iliyochukuliwa na waheshimiwa Kwa manufaa Yao na ya Nchi. Sisi hatuko tayari kuona viongozi wetu au wake zào wakitumia magari ya low class. Tunataka wageni hasa Wakenya wanapotutembelea waone jinsi nchi yetu ilivyobarikiwa viongozi Wenye akili kubwa ya utafutaji.