Ili kuepuka usumbufu na gharama zisizo za lazima Fanya yafuatayo kabla ya kwenda makao makuu ya Uhamiaji Kurasini Dar

MartinCoder

JF-Expert Member
Feb 20, 2018
703
1,000
Ili kuepuka usumbufu na gharama zisizo za lazima Fanya yafuatayo kabla ya kwenda makao makuu ya Uhamiaji Kurasini Dar


1.Toa kopi ya vyeti/vitambulisho vyako kabisa kama kuna uhitaji wa kufanya hivo :make steshenari za maeneo yale wengi wana bei za kukomoana (mfano kuna steshenari bei ya kopi sh 500 kwa page Moja) -wenye mipesa waache watoe pale kopi

2. Nenda na Passport size zako kabisa kama kuna umuhim wa kufanya hivo ili kuepuka bei ambayo hutoiweza.

3.Usiende na begi Kama huna gari binafsi ya kwenda nayo -Hakuna anaye ruhusiwa kupita getini na begi, isipokuwa mikoba tu kwa akina mama /mabinti

i.e beba nyaraka kwenye bahasha au small hand bag. Ukienda na begi utaambiwa na walinzi kuwa tafuta mtu /sehemu huko nje uweke. Kuna steshenari au cafeteria nje wanatoza 1000 kukuwekea begi ingawa usalama wao siuamini.

Ikiwa utakuwa na vitu vya thamani kwenye begi kama laptop cjui kama ukimuachia mtu pale utakaa kwa amani( kwa utapeli wa Dar ....). Ukiwa na gari binafsi hutapata shida begi utafungia kwenye gari lako

4.Usiende umevaa suruari oversize make pale getini kwenye ukaguzi unavua mpaka mkanda wa suruari. So kama suruari yako inavuka pindi unapovua mkanda usithubutu kwenda na hilo bwanga Lako.

Baadhi ya walinzi mkanda hawakwambii vua. Mi Mara ya kwanza skuvua mkanda ,mara ya pili nliambiwa nivue mkanda. Isipokuwa mkanda wako uwe haujatengenezwa na aina yoyote ya chuma.

5.Kama una-Apply passport jaza fomu online ili uiprinti na kwenda nayo kabisa kuepuka usumbufu wa kujazia pale ikiwemo kupoteza muda.


NB:Sina lengo la kuharibu biashara za watu wa steshenari maeneo Yale ila nakupa tahadhari wewe mwenzangu namimi ambaye buku kwako ni Kama msimbazi

Mengine wataleta wengine
 

bowlibo

JF-Expert Member
Dec 10, 2011
3,184
2,000
Waache ubahili, wanunue scanner sampuli niliziona ubalozi wa Japan. Unascaniwa mzimamzima unapopita korido, hawaachi kitu wale
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom