Ili Kuepuka Masimango ya Mkewe, Ateka Benki ili Atupwe Jela | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ili Kuepuka Masimango ya Mkewe, Ateka Benki ili Atupwe Jela

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by MziziMkavu, Sep 12, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Sep 12, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Friday, September 11, 2009 4:24 AM
  Jamaa mmoja wa nchini Marekani ili kukwepa manyanyaso na masimango ya mke wake aliamua kuiteka benki na kuwasubiria polisi waje wamkamate ili atupwe jela. Anthony Miller, 39, alimwambia jaji wa mahakama ya kitongoji cha lancaster, Pennsylvania, Marekani kwamba mke wake alikuwa akimnyanyasa sana kiasi cha kwamba mwaka 2007 aliamua kuiteka benki ya Ephrata Bank na buduki ili afungwe jela aweze kuepukana na manyanyaso yake.

  “Alikuwa akininyanyasa na kunisimanga kwa maneno sana” Miller alimwambia jaji Louis Farina. “Niliogopa kumwacha kwasababu alitishia kujiua iwapo nitamwacha”.

  Miller baada ya kuiteka benki alikuwa na shauku kubwa ya kukamatwa na polisi kiasi cha kwamba aliwasubiria polisi kwa dakika kadhaa baada ya kumlazimisha mfanyakazi wa mhasibu wa benki asalimishe pesa zilizokuwepo.

  “Umeishawaita polisi?” Miller alimuuliza mhasibu huyo kwa mujibu wa gazeti la Lancaster.

  Mhasibu huyo hatimaye aliweza kuwataarifu polisi kwa kubonyeza alarm ya benki. Polisi walimkamata Miller wakati akitoka kwenye benki hiyo baada ya kuchoka kuwasubiri.

  Miller alipofanyiwa mahojiano na polisi baada kukamatwa aliwaambia kuwa yuko tayari kwenda jela.

  Jaji Marina alimwambia Miller kuwa amefanya kosa kubwa la jinai pamoja na kwamba bunduki aliyokuwa nayo haikuwa na risasi na wala hakuwa na nia ya kumdhuru mtu.

  Jaji Marina alimhukumu Miller kwenda jela miaka sita lakini wakili wa Miller alitaka Miller ambaye alikuwa tayari ameishakaa jela miezi 31 aachiwe huru.

  Jaji Marina alimgeukia Miller na kumwambia kuwa inabidi wapate uhakika kuwa hatarudia tena kuteka benki.

  Na kama habari nzuri kwa Miller, ndoa yake na mkewe ilivunjika rasmi mwaka jana.
  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=3054918&&Cat=2
   
Loading...