Ili kuendeleza soka inabidi tufanye yafuatayo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ili kuendeleza soka inabidi tufanye yafuatayo

Discussion in 'Sports' started by Rutashubanyuma, Oct 11, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Oct 11, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,787
  Trophy Points: 280
  Tabia ya kuleta makocha wakigeni yaelekea siyo muarobaini wa kutufanya tutambe kwenye viwanja vya soka duniani lakini hatua hizi zaweza kutusoge za mbele ya hapa tulipo:-

  a) Kutambua ya kuwa vilabu ndiyo msingi wa maendeleo ya soka usiwe na wa domo tu bali uanze na kutoa ruzuku kwa vilabu kutoka serikalini ili vitoe chachu ya mchezo huu. Aidha vilabu vimekuwa vikiendesha kazi zake kutokana na ridhaa ya wafadhili ambao wengi wao huja na malengo yao binafsi ambayo siyo lazima yaoane na mahitaji ya vilabu husika. Ruzuku hizi zitapunguza au kuondoa kabisa tegemezi za vilabu kutoka kwa wafadhili ambao hutoa mchango mkubwa wa kudumaza soka letu badala ya kuliendeleza.

  Kwa kuanzia vilabu vya darajala premier, kila kilabu kipewe shilingi bilioni moja kila mwaka na daraja la kwanza shilingi milioni mia mbili hamsini kila mwaka kwa kila kilabu. Daraja la pili shilingi milioni mia kwa mwaka kwa kila kilabu. Daraja la tatu shilingi milioni hamsini kwa kila kilabu na kwa mwaka. Masharti ya kuendelea kuzipata fedha hizi ni kuwa kila timu itabidi kupeleka hesabu zao zilizokaguliwa kwa CAG kila mwaka kuhakikisha fedha hizo zimetumika vyema kwa malengo yaliyokusudiwa......

  b) Wachezaji wa timu ya taifa kulipwa mshahara wa kila mwezi kama nchi nyinginezo duniani. Mfano, Afrika ya Kusini mchezaji hulipwa dola za kimarekani elfu nne kila mwezi. Hii itawaongezea wachezaji wa Taifa Stars ari ya kuichezea timu ya taifa badala ya mfumo uliopo hivi sasa.

  Kwa kuanza kila mchezaji alipwe mshahara wa dola 2,000 kwa mwezi mbali ya posho wakati wa mazoezi au mechi au mshahra wake wa kilabuni kwake atokako.........


  Toa maoni yako ya kuboresha soka tuyapeleke kwa wahusika
   
 2. NG'OTIMBEBEDZU

  NG'OTIMBEBEDZU JF-Expert Member

  #2
  Oct 11, 2010
  Joined: Aug 11, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Makosa yapo sehemu kibao, na mengine yanatokana na kutaka sifa bila ya kufanya chochote cha maana. TFF imeshindwa kabisa kulinda timu za mikoani mpaka tunajikuta tuna ligi dhaifu na isiyokuwa na ushindani.

  Kanuni za usajili wa wachezaji zinaumiza sana vilabu vidogo kiasi kwamba wachezaji wa timu ndogo wanachukuliwa kirahisi mno na timu kubwa na kusababisha timu hizi kuwa na utitiri wa wachezaji wa mazoezi zaidi kuliko wa kucheza mechi.

  Ligi yetu haieleweki kama ni ya kulipwa au ya ridhaa,maana kuna timu ambazo zinaendeshwa ktk mfumo wa kiprofessional lakini zinacheza ligi ya ridhaa,hapo unakuta chances za kumfanya mchezaji kuwa endelevu ni kidogo mno kwa vile anasajiliwa kiprofessional,anacheza rihaa na mkataba unakuwa feki kwa vile mchezaji mwenewe anakuwa hana uhakika wa tiba nzuri akiumia kwa vile hata bima yake ni ya kimtindomtindo tu.

  Usimba Uyanga ni athari kubwa sana kwa vile umegawa soka letu pande 2,mpaka kwenye timu ya Taifa. Udhaifu wa technical director wa TFF nao ni kiwazo kwa vile ni kama hana fikra mpya za kuboresha ligi ikawa ya ushindani zaidi.

  Huu ni mtazamo wangu tu,sijui wewe unasemaje?
   
Loading...