Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,468
- 113,583
Wanabodi,
Nimeanza kusikia sauti zikihimiza kutumika kwa busara ili kuepusha shari inayoweza kutokea hapo September Mosi kwenye maandamano na mikutano ya UKUTA nchi nzima,
Sasa ili hiyo busara itumike, kitu cha kwanza kabla hiyo busara haijatumika, shurti la kwanza ni hiyo busara iwepo! .
Jee katika hali halisi ya pande kuu zinazohusika na mgogoro huu, jee hii busara inayozungumzwa kutumika, ipo?!.
Jee tangazo la kupiga marufuku maandamano na mikutano ya hadhara nchi nzima hadi 2020 lilitumia busara? .
Jee wahusika wakuu wa maandamano na mikutano ya hadhara nchi nzima kuhamasisha UKUTA wametumia busara kubuni jina la UKUTA? .
Maadam katiba imetoa haki ya kuandamana na haki ya kukusanyika na kufanya mikutano ya hadhara kwa kibali, Jee kuitumia haki hii ya Kikatiba kunahitaji busara? .
Vitendo kwa kauli na matendo ya viongozi na Jeshi letu la polisi, lugha zinazotumika kuonyesha watayadhibiti maandamano na mikutano hiyo kwa nguvu zote, kumeosha uwepo wa busara? .
Hayo na mengine mengi yameonyesha uwepo wa busara?.
My Take.
Kwa maoni yangu tangu tamko la kupiga marufuku mikutano ya kisiasa, halikutolewa kwa busara na kila likisisitizwa zinatumika lugha za ukakasi zaidi kuashiria shari kuliko heri, hapa busara iko wapi? .
Chadema na viongozi wake kwa kauli na matendo wameonyesha kukaidi utii wa mamlaka halali kwa kauli za jeuri ya katiba bila kuonesha kiwango chochote cha busara, hivyo Chadema nao kuanzia viongozi wao, wazee wao hadi wanachama, washabiki na wafuasi wao hawajaonyesha busara yoyote, hivyo hiyo busara ya kutumika Chadema itoke wapi? .
Viongozi wa Serikali na Jeshi la Polisi nao hawajaonyesha busara yoyote tangu day one. Hivyo hiyo busara ya kuyadhibiti maandamano na mikutano ya UKUTA nchi nzima wataitoa wapi? .
Kama suluhisho la kudumu la mgogoro wowote ni matumizi ya busara, inapotokea hiyo busara haipo, busara inayozungumzwa kutumika kuepusha shari hiyo tarehe 1 September ipo? kama haipo, itoke wapi? .
Jee kweli busara ndio suluhisho? au suluhisho ni kufuatwa kwa katiba, sheria, taratibu na kanuni, ukiwemo utii wa sheria bila shuruti na hata kama amri zenyewe ni batili na kinyume cha katiba? .
Pasco