Ilhan Omar: Trump ni mwendawazimu na mtu aliyechanganyikiwa

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
5,214
2,000
Ilhan Omar: Trump ni mwendawazimu na mtu aliyechanganyikiwa
Mei 25, 2019 06:56 UTC
Mbunge wa Kongresi ya Marekani, Ilhan Omar amemtaja Rais Donald Trump wa nchi hiyo kuwa ni mwendawazimu, mtu asiye wa kawaida, aliyechanganyikiwa na mwenye huzuni.
Mbunge huyo wa Baraza la Wawakilishi la Marekani amesema hayo katika ujumbe wake kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter na kufafanua kuwa, bwabwaja anazotoa Trump hadharani mara kwa mara zinaonyesha kuwa ana matatizo ya kiakili.
Akizungumza Alkhamisi, Trump alijipiga kifua na kusema kuwa yeye ni mtu razini na mwenye busara na hekima nyingi. Hata hivyo Ilhan Omar akijibu kauli hiyo ya Trump amesema mtu ambaye ana uelewa wa hali ya juu kama anavyojinadi Trump hajitangazi na kujipiga kifua hadharani kila mara.
Huko nyuma, mwakilishi huyo wa Kongresi ya Marekani alimtaja Trump kuwa ni dikteta na kusisitiza kuwa, kuna udharura wa kusailiwa na kutimuliwa kiongozi huyo.
Kadhalika Spika wa Kongresi ya Marekani Nancy Pelosi ametumia kinaya kujibu matamshi hayo ya majisifu ya Trump kwa kusema, "Mtu mwenye busara nyingi akianza kufanya kazi kama rais wa nchi, nitafurahi kufanya kazi naye katika sekta za miundombinu, biashara na mambo mengine."
Hii ni si mara ya kwanza kwa Trump kujisifu na kujiita mtu mwenye busara na hekima akihutubia wafuasi wake.
4bsg666ce335511efk2_800C450.jpg
 
mulwanaka

JF-Expert Member
Feb 19, 2017
4,274
2,000
Tembea uone, njoo huku Tanzania ndio utajua Kuna punguani anayeitwa Zuzu.
Kwa uzuzu wake tumepoteza mamilioni ya dola ambayo tungeyapata kwenye korosho, Sasa korosho zinaozea ghalani
Duh wewe unaona korosho tu kaharibu kila sekita ya uchumi kaua private sector Elimu ajira za umma nk
 
BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
109,520
2,000
Hahahahaha ile misemo yao ya kizwazwa “mtaisoma namba” na “mtapata tabu sana” hawaitumii tena tu. Maisha yamewapiga kwenye uchumi unaokuwa kwa “asilimia 7 au zaidi”

Lakin nilichofurahi ni kuwa namba tunazisoma wote mpaka hao hao mafisiem
 
Wyatt Mathewson

JF-Expert Member
Dec 22, 2017
10,992
2,000
Ilhan Omar: Trump ni mwendawazimu na mtu aliyechanganyikiwa
Mei 25, 2019 06:56 UTC
Mbunge wa Kongresi ya Marekani, Ilhan Omar amemtaja Rais Donald Trump wa nchi hiyo kuwa ni mwendawazimu, mtu asiye wa kawaida, aliyechanganyikiwa na mwenye huzuni.
Mbunge huyo wa Baraza la Wawakilishi la Marekani amesema hayo katika ujumbe wake kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter na kufafanua kuwa, bwabwaja anazotoa Trump hadharani mara kwa mara zinaonyesha kuwa ana matatizo ya kiakili.
Akizungumza Alkhamisi, Trump alijipiga kifua na kusema kuwa yeye ni mtu razini na mwenye busara na hekima nyingi. Hata hivyo Ilhan Omar akijibu kauli hiyo ya Trump amesema mtu ambaye ana uelewa wa hali ya juu kama anavyojinadi Trump hajitangazi na kujipiga kifua hadharani kila mara.
Huko nyuma, mwakilishi huyo wa Kongresi ya Marekani alimtaja Trump kuwa ni dikteta na kusisitiza kuwa, kuna udharura wa kusailiwa na kutimuliwa kiongozi huyo.
Kadhalika Spika wa Kongresi ya Marekani Nancy Pelosi ametumia kinaya kujibu matamshi hayo ya majisifu ya Trump kwa kusema, "Mtu mwenye busara nyingi akianza kufanya kazi kama rais wa nchi, nitafurahi kufanya kazi naye katika sekta za miundombinu, biashara na mambo mengine."
Hii ni si mara ya kwanza kwa Trump kujisifu na kujiita mtu mwenye busara na hekima akihutubia wafuasi wake. View attachment 1107331
Huyu dada ana matatizo yake binafsi ya ajabu sana....anaongea as if alishampima ubongo....mpumbavu sana huyu dada..ashatukana watu kibao America...hana siasa za kistaarabu kabisa!
 
FRANC THE GREAT

JF-Expert Member
May 27, 2016
4,350
2,000
Ashukuru Tu Kwamba Anayasema Hayo Akiwa Ndani Ya Nchi Yenye Uhuru Wa Kutoa Maoni AKA 'Freedom Of Speech'. Angekuwa Tu Hata Hapo Kwa Ndugu Putin Alafu Akazungumza Hayo Dhidi Ya Kiongozi Wa Juu Wa Nchi, Sijui Kama Kesho Yake Angeonekana Mtaani!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom