Ilemela, Mwanza: Afisa Biashara wa Manispaa alalamikiwa na Wafanyabiashara Wadogo

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,802
11,961
Salaam Wakuu,

Afisa Biashara Manispaa ya Ilemela, amelalamikiwa na Wafanyabiashara wadogo kwamba anafanya kazi kwa kukomoa na hasikilizi Matatizo yao.

Wafanyabiashara wadogo Manispaa ya Ilemela wameomba Serikali iwasikilize kilio chao kuliko kuwafungia biashara.

Hapa chini ni nukuu ya Maneno ya Mfanyabiashara mdogo kati ya wengi.

"Jamii forums" tusaidieni kutupazia sauti.

Tazama wafanyabiashara wadogo tunavyo nyanyasika ndani ya Wilaya ya Ilemela Mkoa wa Mwanza. Mimi natumia kitambulisho cha ujasiliamali na nimeanza biashara majuzi tu, ajabu afisa biashara alipita akiwa na mgambo pasipo hata kunipa elimu akafika nakunitisha nakufunga biashara yangu.

Kwa mtindo huu nchi yetu inawaua wafanyabiashara wadogo.

Hatutafika hata kidogo..Tupazieni sauti tunaomba, Huyu ni afisa biashara wa manispaa ya Ilemela". Mwisho Wa kunukuu.

Tumemtafuta Afisa biashara wa Manispaa ya Ilemela bila Mafanikio. Hivyo ni vyema akatolea ufafanuzi hili tatizo ili liishe.

 
Tazama wafanyabiashara wadogo tunavyo nyanyasika ndani ya Wilaya ya Ilemela Mkoa wa Mwanza.Mimi natumia kitambulisho cha ujasiliamali na nimeanza biashara majuzi tu, ajabu afisa biashara alipita akiwa na mgambo pasipo hata kunipa elimu akafika nakunitisha nakufunga biashara yangu...
 
Bongo ni shida, ila shida hio mimi naona ipo kwenye Tozo lukuki, ukifungua biashara kuna Service Levy, Kuna taka bei isiyo rafiki, mara fire kila ukiangalia ni kushikina mashati watu wanataka pesa hata kabla wewe binafsi haujapata kitu.

Lakini issue ya kutumia kitambulisho cha machinga kwenye duka naona ni ku-abuse the system, sababu kulingana na kitambulisho hicho nadhani mauzo (sio faida mauzo) inabidi yasizidi milioni nne kwa mwaka sasa hapo utaona hata mtu anayeuza soda crate moja kwa siku anavuka hio (ingawa huenda faida isiwe kubwa)

Pia haiingii akilini mtu anaweza kulipa pango elfu 50 mpaka laki kwa mwezi alafu aseme ana kibali cha machinga...

Anyway the whole system is a mess.... na huu ubabe ubabe hautakiwi nchi yetu sote tunakuwa kama wakimbizi...

Things are No Longer at Ease.....
 
Back
Top Bottom