ibesa mau
JF-Expert Member
- Sep 17, 2015
- 2,109
- 1,697
Wakati China vijiji vinakusanya bilion 20 kwa mwezi , hapa tanzania kijiji cha Ilela katika halmashauri ya mbinga vijijini inasemekana ndio kijiji bora hapa nchini kwa sababu kinakusanya zaidi ya milioni 18 kwa mwezi toka kwenye vyanzo vyake vya mapato ambavyo ni pamoja na majengo mbalimbali yaliyopo mbinga mjini pamoja na jengo la ghorofa mbili ambalo lipo katikati ya mji wa mbinga. Wanamiliki vibanda vyenye milango zaidi ya mia mbili ambavyo wafanyabiashara mbalimbali katika mji wa mbinga wamekodishiwa . Kwa hakika na kwa jinsi vijiji vyetu vya tanzania vilivyo duni hiki kijiji ni mfano wa kuigwa . Ukiwa mwenyekiti wa kijiji hapa wewe ni sawa na meneja wa benki, na ukiwa afisa mtendaji wa kijiji hiki wewe unaishi kama afisa wa tamisemi .