Ileje: Meneja wa kituo cha kuuza mafuta avamiwa na kuporwa Tsh milioni 25

Ila huyo jambazi mpuuzi kweli Kwann asingeinngia boda Ya Malawi kulee atembee upande ule Hadi anapoteaa
 
Mkuu wa Wilaya ya Ileje ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya hiyo, Anna Gidarya, aliiambia Nipashe kwa simu kuwa tukio hilo lilitokea juzi saa 4:00 asubuhi.

Alisema majambazi hao walimvamia meneja wa kituo hicho aliyejulikana kwa jina moja la Matha ambaye alikuwa kwenye bajaji na kumwamuru kutoa mkoba aliokuwa amewekea fedha alizokuwa akizipeleka benki na kumpora.

Alisema majambazi hao ambao walikuwa kwenye pikipiki ambayo haikuwa na namba za usajili, walimvamia meneja huyo maeneo ya Isongole kitongoji cha Chumbageni ‘B’ jirani na daraja na baada ya kumpora walitokomea kusikojulikana.

Mkuu huyo wa wilaya alisema kufuatia tukio hilo msako mkali wa Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na wananchi ulianza mara moja baada ya tukio hilo na kufanikiwa kumkamata na kumuua mmoja kati ya watuhumiwa hao wa ujambazi waliohusika katika uporaji huo.

Mtu huyo aliyefahamika kwa jina la Emili Yeka Mqakayamba (39), alikamatwa na wananchi katika kijiji cha Sange.

Gidarya alisema kuwa mtuhumiwa huyo aliomba lifti katika gari aina ya Fuso kutokana wananchi na Jeshi la Polisi kujipanga na kuweka vizuizi katika njia mbalimbali za kuingia na kutoka Ileje baada ya kulisimamisha gari hilo dereva aliwaeleza viongozi wa kata kuwa kuna mtu wamempakia na wanamtilia shaka ndani ya gari lao.

Alisema baadaye mtu huyo alitolewa katika gari hilo na kumpeleka katika ofisi ya mtendaji wa kijiji kwa ajili ya kumuhoji na kumfanyia upekuzi, na kwamba alidai alitoka kwa mganga na alipoulizwa ni kijiji gani alitoka, alishindwa kukitaja na kuwaomba atoe vielelezo vyake ndani ya begi lake.

Mkuu wa Wilaya alisema walipomruhusu ghafla alitoa bunduki aina ya Ak 47 na kuwaelekezea mtendaji na mgambo waliokuwa wanamuhoji, lakini mmoja kati ya mgambo hao alimrukia na kuishika bunduki hiyo na katika purukushani risasi mbili zilifyatuka ndani ya ofisi.

Alisema baada ya purukushani, wananchi wakazi wa Kijiji cha Sange walisogea eneo la tukio na kuanza kumshambulia jambazi hadi kufa.

Aliongeza kuwa walipopekuliwa katika begi lake alikutwa na Sh.1,200,000 na silaha nyingine aina ya bastora (chaines) iliyokuwa na risasi tano kati ya nane zilizostahili kuwapo ndani ya silaha na haijajulikana risasi tatu zingine zilitumika wapi.

Chanzo: Nipashe

Masikitiko:
Jesh la Polisi liloweza kuzuia ugaidi wa laki 6 na kuwakabili kisawasawaa makomandoo limeshndwaje kuwazuia watu wawili majambazi ( pengine sio Makomandoo) wakafanya uharifu wa kupora million 25??
Kuna polisi walidhibiti makomando, mkuu naomba source ya hii habari niitafute
 
Wananchi bwana eti wakazikuta tsh 1,200,00/=hizo 23,800,000/= zilenda wapi japo walikua wawili
 
50C59397-11A2-40FC-B811-61E646962EE4.jpeg
 
Tumpongeze mgambo japo tunatakiwa tumwitwe jeshi la akiba siyo mgambo kuhusu hela hao wamezifukia sehemu
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom