ILEJE: DC aamuru Afisa Habari wa wilaya kuwekwa ndani kwa kosa la kutowaalika Waandishi kwenye vikao maalum vya Serikali

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,410
2,000
Mkuu wa Wilaya ya Ileje Joseph Mkude ameamuru Afisa Habari wa Ileje Daniel Mwambene awekwe ndani kwa kosa la kutowaalika Waandishi wa Habari katika Vikao muhimu vya serikali pia amempa maagizo Mkurugenzi wa Ileje Haji Mnasi kubadili mfumo wa kuwaita Waandishi wa Habari.

Akiongea na Mwandishi wetu Mkude amesema ameshangazwa na kitendo cha Waandishi wa Habari kutokuwepo katika Vikao muhimu kama kilichofanyika leo cha DCC.

"Afisa Habari ni mratibu wa Waandishi wa Habari sio mwana habari leo wananchi wanakosa habari muhimu kama hizi sababu ya uzembe wa mtu mmoja serikali inafanya mambo kwa uwazi yeye anakuja kutoa taarifa za vikao baada ya wiki nimeamua kumuweka ndani ili iwe fundisho hatutaki mzaha" amesema Mkuu wa Wilaya.
 
Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
871
1,000
Mkuu wa Wilaya ya Ileje Joseph Mkude ameamuru Afisa Habari wa Ileje Daniel Mwambene awekwe ndani kwa kosa la kutowaalika Waandishi wa Habari katika Vikao muhimu vya serikali pia amempa maagizo Mkurugenzi wa Ileje Haji Mnasi kubadili mfumo wa kuwaita Waandishi wa Habari

Mkude amesema ameshangazwa na kitendo cha Waandishi wa Habari kutokuwepo katika Vikao muhimu kama kilichofanyika leo cha DCC.

"Afisa Habari ni mratibu wa Waandishi wa Habari sio mwana habari leo wananchi wanakosa habari muhimu kama hizi sababu ya uzembe wa mtu mmoja serikali inafanya mambo kwa uwazi yeye anakuja kutoa taarifa za vikao baada ya wiki nimeamua kumuweka ndani ili iwe fundisho hatutaki mzaha" amesema Mkuu wa Wilaya.
 
USSR

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
5,253
2,000
Kosa kubwa sana maana wananchi wanataka kusikia habari.
 
macho_mdiliko

JF-Expert Member
Mar 10, 2008
13,322
2,000
Huyu DC anatuaminisha kosa la kutoalika waandishi wa habari LINAHATARISHA USALAMA WA TAIFA?
Kosa kubwa hapo DC analoliona ni ''kosa'' la usanii wake wa kwenye makamera kutomfikia bosi wake. Kwa kifupi hawa ni wale ma-DC ambao wameshamjulia bosi wao kuwa anapenda usanii wa kuonekana kwenye makamera na kila mteule anayeonekana kwenye makamera anaitwa mchapa kazi.
 
wa hapahapa

JF-Expert Member
Aug 22, 2012
7,139
2,000
Kosa kubwa hapo DC analoliona ni ''kosa'' la usanii wake wa kwenye makamera kutomfikia bosi wake. Kwa kifupi hawa ni wale ma-DC ambao wameshamjulia bosi wao kuwa anapenda usanii wa kuonekana kwenye makamera na kila mteule anayeonekana kwenye makamera anaitwa mchapa kazi.

Kwa Nini huyo dc asitumie njia nyingine labda kumuonya, au kumkumbusha wajibu wake...

Hao Wana ishu nyingine tofauti na hiyo.... Labda wanagombania Bibi...
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom