Ile style aliyofanya yule mjane kumfikia Rais isirudiwe tena

ebaeban

JF-Expert Member
Jan 15, 2012
2,205
2,692
Kile kitendo alichofanya yule mjane wa kutoka Tanga hadi kumfikia rais ni kitendo cha hatari sana kwa rais na kisirudiwe tena na mtu yoyote awe mjane au laa.

Watu wenye nia mbaya wanaweza kutumia mwanya huo na kumfikia rais ili watekeleze ya kwao, kumbukeni yaliyompata Rajiv GANDHI wa India , yule mama wa kubeba shada la maua alifanya usanii unaofanana kabisa na aliofanya huyo mjane ambae ameshindwa mahakamani vibaya sana mtakumbuka kilichomtokea yule waziri mkuu wa India.

Nasema mchezo wa aina hiyo usirudiwe tena iwe ni fundisho, pia walinzi wa rais waliovaa kiraia waliokuwepo siku ile ya maadhimisho ya siku ya sheria duniani ambapo yule mjane alijitokeza na bango lake wafukuzwe kazi mala moja, au wapewe extra drill ya week moja pale Lugalo ili siku ingine wakumbuke kutimiza wajibu wao ipasavyo.

Tushukuru yule mama alitoa bango angekuwa na vitu vingine lengo lake lingetimia kwa asilimia 100

Nasema tena ile style aliyotumia yule mama mjane hadi kumfikia rais isirudiwe tenaaaaaaaa ni hatari.
 
Back
Top Bottom