Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,694
- 40,720
Mkaguzi mkuu wa serikali alitoa ripoti yake ya uchunguzi wa umma ya mwaka 2006. Kuhusu akaunti ya EPA aliweza kuonesha (hii ilikuwa mwaka 2006) kuwa shs bilioni 90 zilikuwa zimeibiwa na zile 44 Bilioni zinahitaji uchunguzi zaidi...
Maswali:
- Kama mkaguzi mkuu wa serikali aliwez akuonesha kuwa bilioni 90 zimeshaibiwa kwanini Ballali aliendelea kuwa Gavana wa Benki Kuu
- Kwanini wahusika wote hawakukamatwa mara moja?
- Kwanini Jeshi la Polisi lenye dhamana ya kuhakikisha "usalama wa raia na mali zao" hawakuingia Benki Kuu na kuwatia pingu wahusika wote?
- Kwanini serikali ilianzisha uchunguzi mwingine wa EPA nzima badala ya uchunguzi wa hizo 44 tu kwani zile tisini tayari zilioneshwa kuwa zimeibiwa
- Kwanini licha ya serikalii kujua uhalifu umefanyika hakukuwa na juhudi zozote za wazi za kuipangua Benki Kuu kiasi kwamba hata sasa hakuna mtu aliyefukuzwa zaidi ya kuhamishwa na kupelekwa vitengo vingine?
- Ni mpaka kiasi gani cha fedha kiibwe ndipo tujue tuna matatizo?
Katika ripoti hiyo "nyingine" ambayo wengi hawakupata kuiona na leo ninaitoa hapa kwa mara ya kwanza kuna mambo mengi yaliyotajwa kuhusu makampuni mbalimbali ya serikali lakini katika makampuni hayo yote (kama ilivyo kwa BoT) hakuna hatua kali na za fundisho kuchukuliwa?
Tafadhali jisomee ripotii hiyo wewe mweenyewe na uamua kama tukisema kuna wazembe, wezi, na wadanganyao katika serikali yetu tutakuwa tunawatukana... au tunasema ukweli ambao wao ndio mashahidi wa kwanza?