Ile principle ya divide and rule kwa ngozi nyeusi imefanikiwa sana

the glassroof

JF-Expert Member
Apr 25, 2017
256
500
Mpaka hapa tulipofikia bado kuna watu wanaendelea kugawanyika kwenye masuala ya kitaifa.

Ripoti ya pili imesomwa juzi, watu wakabeza vya kutosha. Haya leo wahusika wamekuja tena mamlaka ya juu kabisa, bado vijembe vinaendelea kurushwa. Wakati wawekezaji wamekili kukaa meza moja nasi tuyamilize

Siamini kama utimamu wetu tunautendea haki katika kuargue

Nina mashaka na uzalendo kama si uraia wetu

Nashukuru pia hayati baba wa taifa kutuachia lugha ya taifa kiswahili ambacho wazungu hawahangaiki nacho, maana wangekuwa wanakijua wakawa wanafatilia tunavyojadili rasilimali zetu wangetushangaa sana

Wangejipa matumaini ya kushinda kwa asilimia zote kozi tayari wapo watanzania(sina hakika kama ni wazawa) wako nyuma yao

Na tungekuwa tunajua kiingereza vizuri kama wenzetu wakenya hapo ndo tungewarahisishia zaidi kuujua upumbavu wetu kwa kina kabisa, maana wangejipakulia taarifa zetu kadili wawezavyo

Hiki hiki kiingereza chetu cha hovyo lakini bado baadhi wanakitumia kuwasaidia wawekezaji kupotosha ripoti za uchunguzi, kana kwamba wao ndo wenye machungu kuliko hata wazungu wenyewe

Nafikiri wangejua kama watanzania wenyewe hawaipendi nchi yao wala wasingehangaika hata kuleta wazungu wafanye kazi kwenye makampuni yao.

Badala yake wangetuacha tufanye wazawa wenyewe ili tuwasaidie kupora mali zetu wenyewe. Na kwa mantiki hiyo hata tukitaka kuwashitaki watushangae vizuri maana wezi ni sisi wenyewe 100%

Na hata wasipate tabu kutafuta waumini wao ni rahisi sana, waangalie tu kwenye mitandao yetu ya kijamii, watu wao wako open kabisa.

Labda tatizo kiswahili chetu ndo hawakijui, iko haja wazungu wawekeze sana kwenye kiswahili. Kwa maana watamjua mswahili vizuri na kamwe hawatojutia kumfahamu.

Kweli mwl nyerere aliona mbali sana, na alitufahamu vizuri sana. Akaamua kutufichia aibu yetu kwa kututengezea lugha yetu wenyewe, yaani tubaki kama kisiwa. Ila yeye alijifunza kizungu ili atuwakilishe vyema.

Kwa hili naiona mantiki ya kukiendeleza kiswahili na ikibidi kizungu kifutwe kabisa kuficha upumbavu wetu, na atakae ruhusiwa kusoma kiingereza basi awe amethibitishwa uzalendo wake ili asiliangamize taifa kwa kuwa kibaraka wa mzungu.

Ni hayo tu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom