Ile operesheni tokomeza mbu Tanzania imeishia wapi? Kiwanda kilizinduliwa na Mh. Pinda pale Pwani

Chai.. ..

Ukienda kupima damu haionekani ila ukipewa dawa za malaria umeze unapona@!

Nadhani ilimuwa ni ya kuficha maradhi yasionekane tu ila sio watu wasiugue!

Sema kidogo haijambo!
Niliwahi kusikia eti Zanzibar hakuna kabisa mbu wala Malaria. Sasa sijui kama ni kweli au ni chai tu.
 
Mimi nakaa Kibaha, Pangani karibu sana na hicho kiwanda. Kipo opp. Na makao makuu ya NIDA. KIwanda hakijawahi kufanya kazi, mule Kuna walinzi tu na wafyeka majani.
 
Hicho kiwanda kinachotengeneza viuatirifu kinaitwa Tanzania Biotech Products Ltd (TBPL) na kipo chini ya Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC). Wanasema wanatengeneza viuadudu vya Griselesf na Bactivec ambavyo wanadai ndio viuatirifu na dawa pekee ya kukomesha na kuangamiza mfumo wa kuzaliana kwa mbu wanaoeneza ugonjwa wa malaria.

Naona serikali imeamua kuwakabishi mradi huo wajanja wa mjini wanaoitwa AMKA TANZANIA kitu ambacho ni kiashiria cha wazi kabisa kwamba serikali haina nia ya dhati ya kutokomeza ugonjwa huo wa malaria nchini na kama ina nia hiyo basi haina mkakati wowote madhubuti wa kufanikisha lengo lake. Hao jamaa wa AMKA TANZANIA kila siku kazi yao kubwa ni kuhamasisha mwananchi mmoja mmoja tena kwa hiari yake anunue hivyo viuatirifu na kupulizia nyumbani kwake kitu ambacho kwa mtazamo wa haraka haraka hakitaweza kufanikisha jambo hilo kwa wepesi na hasa ukizingatia mazoea yetu sisi watanzania ya kupuuzia mambo ya msingi. Hivi kweli serikali inategemea malaria itaisha nchini kwa kusubiri hiari ya mwananchi mmoja mmoja kununua viuatirifu? Maana mwananchi mmoja akinunua na jirani yake asiponunua huyo aliyenunua na kupulizia kwake ni kama kapoteza tu pesa, muda na nguvu zake.
 
Kweli Mkuu
Hicho kiwanda kinachotengeneza viuatirifu kinaitwa Tanzania Biotech Products Ltd (TBPL) na kipo chini ya Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC). Wanasema wanatengeneza viuadudu vya Griselesf na Bactivec ambavyo wanadai ndio viuatirifu na dawa pekee ya kukomesha na kuangamiza mfumo wa kuzaliana kwa mbu wanaoeneza ugonjwa wa malaria...
 
Back
Top Bottom