Ile kesi ya mauaji ya mkurugenzi wa Manyoni imeishia wapi?

Witmak255

JF-Expert Member
Feb 5, 2019
3,264
5,403
Wakazi wa manyoni na wajuzi wenye taarifa za uhakika mtujuze Kuhusu huyu DED, kesi yake imefikia wapi?
Na je alitenguliwa au bado Yuko kwenye Ofisi za umma?

Tangu mauaji yalipotekea huko manyoni baada ya DED na msafara wake kuvamia kanisa na kutekeleza uovu wao, taarifa hazikuwa wazi sana na hata zilipotoka kwa kuchelewa zilikinzana, sio magazeti, TV Wala radio hakuna sehemu yeyote utakapokuta habari ya kina kuhusu kesi hii ya mauaji inayomkabili DED.

Huyu DED inasemekana ni ndugu wa damu na namba one, hebu Wana jf wajuzi tujuzeni huyu mkurugenzi bado yuko ofisini?
Na vipi kesi ilishafutwa?
 
Watanzania kama kawaida yetu tumeshasahau na life goes on!!,kuna mifano mingi tu wapi ripoti kuhusu kuzama kwa kile kivuko pale Mwanza!whats about yule mfanyabiashara mkubwa pale moja ya mikoa ya kanda ya ziwa aliyeuliwa na mwili wake kupatikana kwenye kiroba?

vipi kuhusu yule kiongozi wa chadema aliyeuliwa kinyama pale moja ya mikoa again ya ziwa?nini kimetokea kwa muuaji wa yule mwandishi wa habari pale Iringa(naona hata mwenyekiti wa kijiji ,mjengwa ameshasahau!!)viroba vya maiti pale ufwekweni wa coco?maiti ndani ya mto Ruvu?dada yetu Akwilina mbona kimya?

kichapo cha walemavu walipojaribu kuandamana kati ya jiji la makonda kuna aliyewajibika?Lissu anapigwa risasi na watu wasiojulikana ,kamanda wa jeshi naye anashambuliwa ila yeye anapelekwa SA kwa matibabu na washambuliaji wake wanauliwa katika majibizano ya risasi na polisi(break) its on and on and on.....
 
Km atakuwa kazini basi hakuna haja ya mahakama wala bunge halina maana tna.km wanatunga sheria ambayo haitekelekezeki kuna haja gani ya bunge
 
Back
Top Bottom