Ile Jumamosi ya mwisho wa mwezi ya usafi bado ipo?

Mseti athuman

JF-Expert Member
Jul 19, 2016
203
150
Habari wanaJf,
Ile Jumamosi ya mwisho wa mwezi ya usafi bado ipo?
Jaman mbona siku hizi hatuoni usafi na Tv hazirushi
 
daaah nimeingia restaurant moja hapa kupiga supu nimeambiwa hakuna mauzo mpaka saa nne saa hii usafi agizo la raisi
 
mzunguko unasimama kwa muda, ila wenye magari ya abiria wao mwendo mdungo
 
Watu hawafagii mpk wamuone na mkuu wa Nchi kashika Fagio......watanzania tuna kaasili ketu ka uchafu.
 
Habari wanaJf,
Ile Jumamosi ya mwisho wa mwezi ya usafi bado ipo?
Jaman mbona siku hizi hatuoni usafi na Tv hazirushi
Hakuna hata moja ambalo wamefanikisha,

Makonda kila analogusa anakuta moto, kagusa sukari hakurudi tena, kajaribu wamachinga hata hakumbuki keshasahau, walimu kupanda bure ukimkumbusha tunaambiwa mchochezi, ya unga na ujangili ukimwambia unaweza kuozea jela, kaanza kubomoa majumba ya watu ngoja tuone episode hii.
 
Watu wanafunga maduka na migahawa yao wakihofia kukamatwa, wanasubiri saa nne ifike wafungue ili waendelee na biashara zao. Hakuna anaye fanya usafi.
 
Hapo ndio utambue kuwa viongozi wetu wengi ni wanafiki, nia yao haikuwa kufanya maeneo husika yawe masafi, lengo lao kubwa ilikuwa ni kuonekana na bwana mkubwa kuwa na wao wanaendana na kasi yake.

Pale bwana mkubwa alipoamua kukusanya takataka mbele ya kamera na wao wakafuata mkumbo na kuanza kufanya usafi mbele ya kamera, ili kujipendekeza na kupata fursa ya kujikuza kisiasa. Kwa sasa wameona bwana mkubwa haliongelei tena suala hili na wao wameamua kuliacha.

Wajinga wachache waliacha shughuli zao na kutumiwa kisiasa kuokota takataka kwa hizi jumamosi chache za mwisho wa mwezi bila kujua kuwa wanaongozwa na wanafiki kufanya zoezi lisilo na maana yoyote, mji hauwezi kusafishwa kwa kuokota takataka mara moja kwa mwezi wakati takataka zinazalishwa kila siku,kwa majiji makubwa ni kwa kila saa kama sio dakika. Leo hii nimezunguka Dar ni chafu takataka zimejaa mitaroni (nafikiri ni kwa sababu ya ile mvua iliyopita katikati ya wiki) na hakuna zoezi lolote la usafi linaloendelea.

Kwa aina ya uongozi tulionao sasa bwana mkubwa akiamua kutembea uchi, si ajabu kuona wale waliochini yake wakimpigia makofi na kusema amependeza na wengine kuthubutu hata kuvua nguo zao na kumfuata.
894007.jpg
 
  • Thanks
Reactions: Ok9
Back
Top Bottom