Shujaa Mwendazake
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 3,734
- 6,292
"Ile hela ntakutumia kwenye FIKOSHI, utaipokea Buzurugwa, Ahsante."
Hivi ni vibonzo vilivyosambaa mitandaoni hivi sasa, Yawezekana ikawa ni kweli huu utaratibu wa kutumiana pesa manually ama kianalojia ukarejea upya. AMA inawezekana watu wanajaribu kufikisha ujumbe kwa njia hii ya kuwa tunarudi nyumaMama amejinasibu kuwa ni msomaji mkubwa wa Mitandao. Na tunajua kwa mamlaka aliyopewa anaweza kureverse hii tozo inayoleta kelele
Nakumbuka enzi zile tunatumiana pesa kupitia mabasi kama Scaninavian Express kwa sababu ya gharama na ugumu wa kutuma fedha kwa kutumia taasisi za kutuma fedha kama Western Union kuwa na gharama kubwa na wengi wetu si watumiaji wazuri wa huduma za kibenki. Ujio wa mitandao ya simu pamoja na huduma ya kutuma pesa kwa simu zikarahisisha utumaji wa pesa kwenye ncha za vidole vyetu. Nakumbuka gharama zilikuwa nafuu sana kututamanisha tutume kwa mfano ilikuwa Airtel to Airtel ilikuwa ni bure. Sasa kumekucha, gharama za simu nazo zimekuwa ni kama Western Union, Sasa twenede wap wakati wengi wetu huku vijijini si watumiaji wa huduma za kibenki?
Serikali na Bunge vyote vimepewa mamlaka na wananchi, Kiuhalisia nimemshangaa Abbas Tarimba akihimiza wananchi kulipa hii kodi. Lakini Tarimba na kina Zungu hawajajaribu kukaa na kuangalia upande wa wananchi nao wataathirika vip?. Bado wengi wanajiuliza kulikoni kodi kwenye Vileo ikapunguzwa na wakati ni Anasa. Achilia mbali sigara na starehe za kila aina. Kwa nini zisiongezewe kodi hizi.
Mama Samia hizi kodi zilishapingwa tangu pale Mbunge Zungu alipoleta kiherehere chake cha kuitaka, yaani Mbunge anapendekeza mpiga kura wake aongezewe utitiri wa kodi na tozo lakini anashindwa kulalamika ukubwa wa kodi hiyo ama anashindwa hata kudai ripoti ya B.OT ama anashindwa kukomalia matumizi mabaya ya fedha hizi mfano toka ripoti ya CAG. Mama umezibariki na umezisaini baada ya kuidhinishwa na bunge. Ni kweli hujasikia kilio chetu? Nii kweli uliomba tusiwe wanyonge, ulimaanisha au ulitania?
Mama ulisema unaachia fedha mtaani watu wafarijike, Is it TRUE?. Hakika Mgema akisifiwa Tembo hulitia maji. Tumeanza kuamini siku 100 za mwanzo ilikuwa ni Spinning na kuondoa legacy ili kupata endorsement. Tumekuendorse sasa unaturudisha ujima.
Ni wakati sasa wa Mama kutuokoa na janga hili la kuanza kutuma Pesa kianalojia kutoka Mkoa to Mkoa. Haya makato mengine ni gharama ya pesa ya kula ya familia zetu.
SAMIA SULUHU HASSAN HAWEZI KUKWEPA HIZI LAWAMA, MAMA AMEAMUA KUTURUDISHA KIANALOJIA