Ile ahadi ya Mbunge wa Kibamba kutoka kwa Mh Rais ndo imeyeyuka?

Kwasenga

Member
Feb 24, 2021
50
52
Nakumbuka wakati Mh Hayati Rais JPM (R.I.P) kipindi hicho anafungua stand ya Mbezi Lous alimuahidi Mh Mbunge wa Kibamba kuwa kutoka na sababu ya kwamba jimbo hili ndo linaongoza kwa kuwa na kiwango kidogo cha lami yaani chi ya 5%., basi aliagiza timu iundwe na Tanroads pamoja na mbunge wapitie barabara zote kisha utekelezaji uanze.

Sasa ninavyojua Mh rais wa sasa alisema wao ni kitu kimoja na aliyekuwepo, je, hii ahadi itatekelezeka? Make naona hata barabara ya kuingia stand ilivyokuwa na kasi ya kujengwa imesitishwa na hata gharama zilizoingia naona zitaharibikia humo make mpaka waanze upya.

Je, mbunge wa Kibamba ana jibu lolote juu ya ile research aliyoiagiza Mh rais?

Lkn pia kumbuka wilaya mbili za Kigamboni na Ubungo ni wilaya ambazo hazikupata mradi wa DMDP, sasa kwa nini serikali isione kuwa wilaya hizi ziko hoi sana kwenye barabara zao?

Kwa kuwa JF ni babalao, namuomba mbunge aje aelezee kuhusu hii ishu ya barabara.
 
Back
Top Bottom