Ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya 2015-2020 yatekelezwa kwa kishindo sekta ya usafirishaji na uchukuzi nchini

juctn Mt

Member
Jan 12, 2019
38
37
Nikiwa napitia ilani ya uchaguzi ya chama pendwa pendwa cha CCM ya mwaka 2015-2020 hususani katika sekita yetu hii ya usafiri na uchukuzi kuanzia page no 46 -64 .Hakika serikali hii ya awamu ya tano imewatendea haki wananchi wake Kwa kutekeleza zaidi ya asilimia 99.9% Katika sekita hii ya usafiri na uchukuzi.

Awamu hii ya tano serikali imejenga na kukarabati Barabara nyinyi Sana tofauti na awamu za nyuma Kama ilani yenyewe ilivyo eleza na Barabara nyinyi Sana zimekamilika na zingine zipo hatua ya mwisho. Japo kuwa mikakati ilikuwa ni kujenga na panua Barabara zinazounganisha mikoa, Lakini hata za Ndani ya mikoa na wilaya Barabara nyingi zimekarabatiwa. Natumaini makomredi mlioko mikoani mnaona Hali ilivyo nzuri katika Barabara za wilaya na mikoani.

Lakini pia kupitia hii sekita yetu ya usafiri na uchukuzi serikali imejenga na kukarabati madaraja mengi na vivuko vingi Sana kanda ya ziwa wilaya za sengerema, ukerewe, n.k Mara na kigoma nadhani saivi mnasafiri Kwa kuvuka maji bila tatizo.

Aidha Serikali hii imepambana kufufua shirika la Reli nadhani Sisi sote ni mashahidi tutakumbuka kabisa shirika hili la Reli lilikuwa linaenda kufa kifo cha Mende kabisa Lakini Kwa juhudi ya JPM kapambana Sana kuliinua ikiwemo na kulibadili jina kutoka TRL kuwa TRC na mpaka sasa usafiri wa Reli upo imara katika hili wanangu wa kigoma,Tabora,Sumbawanga na Kilimanjaro ni mashahidi. Hata paha Dsm Treni yetu ya mkoa inapiga kazi kweli kweli .tusisahau pia serikali Bado inaendelea na ujenzi wa reli ya kisasa.

Lakini pia kuna Bandari nyingi na viwanja vya ndenge vimejengwa na vingine Vipo katika ujenzi si mnaikumbuka Terminal 3 hapo uwanja wa Ndege wa kimataifa wa mwl Julius Nyerere Dsm. bila kusahau uwanja wa msalato unaanza kujengwa soon, Mwanza Air port inapanuliwa huko zipo nyingi Sana msisahau na hizo Ndege nyingi tu na zingine Bado zitakuja .

Ilani ya uchaguzi ya 2015-2020 katika sekita hii ya usafiri na uchukuzi imetekelezwa Kwa kishindo .

*2020 JPM TENA*
TUTACHAGUA MAFANIKIO
IMG_20200106_200352.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijutii Kura yangu 2015. CCM Daima. Mbeya Mjini, Hai, Iringa Mjini, Kibamba, Ubungo rudini nyumbani l, kumenoga
 
Watanzania ni watu wajinga sana SASA hayo yote ni WEMA wa CCM kuyafanya au ni wajibu wao kutokana na KODI zetu ??? Yaani unafikiria serikali kujenga barabara ni ihsani ?? ELIMU....ELIMU ....ELIMU...

SERIKALI INATAKIWA ISIFIWE INAPOTENGENEZA AJIRA KWA WINGI NA KUBORESHA MAISHA YA WATU SIO KWA KUJENGA BARABARA, RELI, AIRPORT, MADARAJA NA KUNUNUA NDEGE.

WATANZANIA TUSIWE WAJINGA KIASI HICHO.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom