Ilani ya uchaguzi ya CHADEMA kuathiri ndoa

RMC

JF-Expert Member
Nov 16, 2013
1,337
1,752
Nimeisoma ilani ya uchaguzi ya CHADEMA kurasa zote. Nimeona kasoro nyingi sana lakini katika jukwaa hili nazungumzia kasoro moja ambayo ina athari katika ndoa.

Ilani ya CHADEMA inakusudia kuweka sheria ya kutambua kitu wanachoita ubakaji ndani ya ndoa. Wanasema kuwa wakiingia madarakani watafanya kuwa ni kosa la jinai ubakaji ndani ya ndoa.

Tuangalie athari ya hii sheria. Sheria hii itamuamini mke kwa anachokisema kuliko mume hata kama mume atakuwa anasingiziwa. Fikiria ndani ya nyumba mpo wawili tu mke na mume, mnaweza mkafanya mapenzi kwa ridhaa kabisa lakini mke akaamua kumkomoa mume kwa sababu ya ugomvi wao mwingine mathalani mume amezaa nje ya ndoa au ana nyumba ndogo au mke anataka kuondoka katika ndoa lakini mume anamng;ang;ania.

Hivyo anaweza akafanya mapenzi kwa ridhaa yake na kisha asubuhi akaenda polisi kushtaki kuwa amebakwa na mumewe. Uwepo wa mbegu za mume katika uke wa mkewe unaweza ukawa ndio ushahidi ambao mke anautumia lakini kumbuka kuwa katika mazingira yao ya ndani si rahisi kutofautisha ni lini mbegu katika uke zimeingia kwa ridhaa au kwa kubakwa.

Sheria hii ikipitishwa waume wengi watafungwa tena kwa kuonewa. Athari ya pili mume akishafungwa atapoteza kazi, pensheni ya jumla na ile mwezi kwa sababu kwa wale wanaofanya serikalini wanapopatikana na hatia katika jinai yeyote hufukuzwa kazi. Jambo hili litaleta mvurugano mkubwa katika jamii ya watanzania. Lissu na CHADEMA hawalizungumzii hili na kwa kuwa wanajua watanzania wengi ni wavivu wa kusoma basi wanajua si rahisi kulielewa jambo hili ambalo lipo ndani ya ilani yao.

Ninanukuu hicho kipengele katika ilani ya CHADEMA: “Kufanyia mabadiliko sheria ya Ndoa ili kuhakikisha kuwa ubakaji ndani ya ndoa unatambulika kuwa ni kosa la jinai” {f (a) ukurasa wa 46}.

Angalizo: Taarifa hii nimenyofoa katika uzi wangu niliopost katika jukwaa la siasa wenye kichwa vha habari "Ilani ya uchaguzi CHADEMA KUATHIRI NDOA NA AJIRA"
 
Chadema bwana wanata wote wawe mafilauni, pia wataruhusu mapenzi ya jinsia moja eti haki za binadamu, hawa si wakuwapa kura!
 
  • Thanks
Reactions: RMC
Back
Top Bottom