Ilani ya Uchaguzi ya CCM ipo bubu juu ya misamaha ya kodi ijayo au iliyopita!!!!!!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ilani ya Uchaguzi ya CCM ipo bubu juu ya misamaha ya kodi ijayo au iliyopita!!!!!!!!!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Rutashubanyuma, Oct 13, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Oct 13, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,787
  Trophy Points: 280
  Nimeipitia kwa makini Ilani ya Uchaguzi ya CCM lakini nimeona ipo bubu juu ya misamaha ya kodi. Yaelekea hiyo ni sera ya kimyakimya ya CCM ambayo hawataki wapigakura waifahamu. Hili ni kukosa maadili kabisa kwa sababu iwaje kwa miaka mitano inayoishia CCM imetoa misamaha ya kodi zaidi ya Tshs trilioni sita ambayo ni zaidi ya nusu ya bajeti nzima ya serikali ya mwaka mmoja lakini isiweze kutathmini misamaha hiyo iliyopita au kuahidi kama sera hiyo itaendelezwa kwa miaka ijayo.

  Ni unafiki usio na kikomo kwa CCM kudai tusome Ilani yao wakati haina mashiko ya kitakwimu ambazo zitamsaidia mpigakura kufanya maamuzi ya busara na ukichangia hata midahalo hawataki wagombea wao tuonane nao ana kwa ana ambako tungeliwahoji juu ya haya na mengineyo.

  CHAGUA DR. SLAA...............CHAGUA CHADEMAAAAAAAAAAAAAAA
   
Loading...