Uchaguzi 2020 Ilani ya Uchaguzi inayofaa 2020 ni ile itakayochochea Ukuaji wa Uchumi kwa wote

MPadmire

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
3,928
3,225
Ilani ya uchaguzi itakayochochea ukuaji wa uchumi kwa wote na kuongezea serikali kodi ndio inafaa.

Vyama vya Siasa inatakiwa vije na Ilani na Mipango ambayo inampa Mtanzania Uhuru wa kuchagua ni wakati gani wa kuajiriwa na ni wakati gani wa kujiajiri. Ilani ipange kuondoa vipingamizi kwa muajiriwa anaetaka kuacha ajiri, ili akafanye Kilimo chake au biashara yake.

Pili: Ilani ije na mpango mahususi wa kuongeze idada walipa kodi (to increase tax payers base) na kuacha tabia ya kuwalimbikizia watu wachache kodi nyingi.

Tatu: Ilani ya hicho chama (watakaopenda) waje na mpango mkakati wa kutawala soko la bidhaa za EAC na SADC (kuwezesha viwanda kuuza nje). Kwa sasa Tanzania kuna mafuriko ya bidhaa za South Africa, Kenya, Uganda, etc). Nyie wenyewe nendeni madukani na supermarkets.

Nne: Nguvu kazi ya vijana itumike ipasavyo(Vijana wamesoma na hawana kazi). Kuwe na mpango mkakati wa kuwatumia kwenye Kilimo, na kutafuta masoko nje ya nchi. Angalia China ananunua mahindi USA, why not Tanzania?

Mwenye zaidi achangie kwa manufaa ya Tanzania yetu sote.

Changia kwa uzalendo. Lete hoja.
 
Waambie chadema watapigwa kipigo cha mbwa mwizi
Wapigsji miezi miwili Sasa hawana posho[SUB]
IMG_20200601_173758.jpg
[/SUB]
 
Naongeza kuwa Serikali iwekeze kwenye Sekta ya utalii kwa nguvu zaidi, kuongeza ajira, kukuza uchumi wa nchi na makusanyo TRA
 
Ccm wanachojua ni kununua ndege, kujenga flyovers, kumsifia mwenyekiti, kununua Madiwani na Wabunge wa vyama vya Upinzani kwa gharama yoyote ile, nk. eti ndiyo maendeleo.
 
Back
Top Bottom