"Ilani" ya uchaguzi haiwezi kuwa dira ya nchi

Shoctopus

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
3,434
1,985
Asalam-alaikhoom Wana-JF!

ANGALIZO kwa Mods na msomaji:
Mods wana tabia ya kupotezea threads zangu mapema sana. Huu si uungwana jamani! Tuvumiliane!

Kwanza kabisa lazima nikiri kwamba kutokana na yaliyotokea kabla ya Uchaguzi MKUU uliopita mimi sikupiga kura kwasababu ninajua maana ya KURA na naiheshimu sana KURA yangu!

KWANZA kwa kawaida lengo na madhumuni ya ILANI YA CHAMA kuelekea uchaguzi hasa Uchaguzi MKUU ni kushinda UCHAGUZI na si vinginevyo! Kwahiyo ILANI ni mikakati, mipango au mbinu mbalimbali za kupata KURA, sio mbinu au mipango ya kuendesha SERIKALI au NCHI.

Kwahiyo tunapopiga KURA tunachgua WATU au CHAMA, hatuchagui Dola au Serikali. Kwahiyo ILANI YA CHAMA haiwezi kamwe kuwa mwongozo wa Dola au Serikali!

NCHI haiwezi kamwe kuendeshwa na ILANI YA CHAMA hata kama kwa kutumia nguvu za polisi na vyombo vya Dola. Kufanya hivyo ni makosa makubwa sana!

Uchaguzi MKUU kwa mgombea asiyejua maana ya KURA; na mwananchi na/au mpigakura asiyejua maana ya KURA vilevile; kwao hawa wawili Uchaguzi ni tukio la siku moja tu, baada ya hapo ni 'business as usual'.

KWANZA, tukianza na MGOMBEA UCHAGUZI asiyejua maana ya KURA, hasa kwenye Uchaguzi MKUU; huyu atatumia kila mbinu aijuayo pamoja na AHADI za UONGO kujipatia "NDIYO" ya mpigakura asiyejua maana ya KURA yake.

Lengo la mgombea asiyejua maana ya KURA ni kupata madaraka kwanza halafu ndipo aanze KUFIKIRI kuhusu nini anachotakiwa kufanya. Kwahiyo AHADI za aina hii ya mgombea KURA lazima ziwe za UONGO MTUPU! Ndiyo maana akiyapata MADARAKA huyatumia kwa manufaa yake binafsi kwanza, halafu huwakumbuka wapigakura wake kuelekea uchaguzi mwingine!
Na kwa hali hiyo mtu huyo 'akishalewa' madaraka mpigakura anakuwa si BINADAMU. Kwake mpigakura ni DARAJA tu la kujipatia MADARAKA!

Mtu huyu huwa hataki kusikia neno 'HAKI' au Haki za Binadamu. Anachotaka yeye ni 'Amani' tu; ili afanye anavyotaka yeye kwa faida yake na CHAMA chake! Na ili aweze kufanya atakavyo hataki kusikia neno 'katiba' au katiba mpya!

PILI kwa mpigakura asiyejua maana ya KURA; Uchaguzi MKUU ni tukio la siku moja tu. Huyu hajui au hajali umuhimu wa KURA yake kwa maisha yake binafsi au TAIFA lake!

Aina hii ya mpigakura asiyejua maana ya KURA ni rahisi kushawishika kutoa KURA yake kwa mgombea atakaempa zawadi au AHADI za UONGO!

Kwahiyo sisi sote Watanzania kama NCHI MAKINI, tuna sababu nyingi za kujiuliza:

Kwamba:

1. Je! Ni sahihi au sio sahihi kwamba Serikali au vyombo vya Dola vifanye kazi zao kupitia ILANI YA CHAMA badala ya KATIBA NA SHERIA ZA NCHI?

2. Je! Ni kweli tuko radhi NCHI yetu iendeshwe kwa ILANI YA CHAMA chochote cha SIASA?

3. WALIPAKODI wote wa Tanzania wameridhia lini kwamba kodi zao zitumike serikalini kutekeleza ILANI YA UCHAGUZI ya CHAMA chochote cha SIASA?

4. Je! Kuendesha SERIKALI au Dola kwa mujibu wa ILANI YA CHAMA ni halali na siyo kukiuka KATIBA?

Mwisho nitoe mifano michache:

1. Kama kuna wagombea wasiojuajua maana ya KURA lakini hao hao ndio wanateua TUME YA UCHAGUZI; Uchaguzi huo ni halali?

2. Kama kuna makundi ya wapigakura wasiojua maana ya KURA kwamfano wamachinga, bodaboda, wanawake, wazee, wanafunzi, bila kusahau wafanyakazi, wakulima, wavuvi, nakadhalika; ambao kama wote hawajui maana ya KURA tungesema hao ndio huiweka CCM madarakani au CHAMA chochote cha SIASA kwa KURA zao?

Tujiulize pia maswali kadhaa kuhusu jinsi gani chama cha siasa kinavyoweza:

a. Kuandaa wagombea na wapigakura wanaojua maana ya KURA?

b. Kuandaa ILANI YA UCHAGUZI
isiyo na UONGO MTUPU kwa madhumuni ya kupata KURA tu?

Chama cha SIASA kinawwezaje kufanya hayo na kupigiwa KURA kupitia TUME YA UCHAGUZI isiyo HURU na mazingira ambayo hayakiruhusu chama hicho kufanya mikutano ya hadhara, au kujinadi kupitia vyombo HURU vya HABARI?

Na kama Bunge ni sauti na chombo pekee cha uwakilishi wa WANANCHI, hilo linawezekana vipi kama wawakilishi hao walikuwa wagombea Uchaguzi MKUU wasiojua maana ya KURA; wakatumia ILANI YA CHAMA iliyojaa UONGO na kupigiwa KURA na watu wasiojua maana ya KURA?

Na inawezekana vipi Bunge la aina hii liikosoe au liiwajibishe Serikali inayotekeleza ILANI YA CHAMA kilicholiunda Bunge lenyewe?

ILANI YA CHAMA chochote cha SIASA haiwezi kamwe kuendesha TAIFA au SERIKALI. Kwasababu asili (nature) ya ILANI YA UCHAGUZI hapa bongoland inatokana na MADHUMUNI ya mgombea na/au CHAMA chake, ambayo ni kupata KURA tu! Na hii ndiyo sababu CCM haitaki wagombea binafsi!

SERIKALI huendeshwa kwa Katiba na Sheria full stop! Sio mtu binafsi aanze kusema eti fulani ametoa fedha ili barabara 'x' ijengwe; au ametoa bilioni kadhaa ili ndege kumi zinunuliwe! Hii ni dharau na ukiukwaji mkubwa wa KATIBA ya NCHI na SHERIA ZETU.

Lakini utakapofika muda wa kampeni na ILANI za Uchaguzi MKUU ujao, utasikia:

... "Tuchagueni sisi kwasababu tumewajengeeni ma-flyover, tumewaleteeni maji safi, dawa hospitalini nakadhalika! Na kwamba tutaondoa kero zenu, kero za muungano, tutaongeza ajira, tutatoa 50 milioni kwa kila kijiji nakadhalika!
Na ile kubwa zaidi: 'tutapambana na rushwa ktk polisi, mahakamani, serikalini nk'

Wakishpata madaraka kitu cha kwanza ni kubuni kodi na tozo mpya! Kujiongezea mawizara kibao na posho nono za safari na vikao, magari kemkem ya fahari na ma-flyover baharini nk.!

Sote tunajua hayo ni mambo ya kampeni za uchaguzi tu. Huwezi kuyatumia kama DIRA YA NCHI na Serikali. Lakini ndivyo tunavyotakiwa kuamini!

HAPA NDIPO TULIPOFIKISHWA WATANZANIA WENZANGU.

TUJADILI.
 
Back
Top Bottom