Uchaguzi 2020 Ilani ya CHAUMMA ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani 2020 - 2025

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
1,266
2,000


CHAMA CHA UKOMBOZI WA UMMA
(CHAUMMA)

ILANI YA UCHAGUZI
(MANIFESTO)
JULY 2020


IMETOLEWA NA HAMASHAURI KUU YA TAIFA
CHAMA CHA UKOMBOZI WA UMMA
MTAA WA KIJITONYAMA, KINONDONI DAR ES SALAAM
JULY .2020
YALIYOMO
1.0 Utangulizi 1
2.0 HALI YA NCHI 2020. 3
3.0 Ajenda zetu katika uchaguzi wa 2020. 4
3.1 Ajenda za kiutawala. 4
3.1.1 Katiba mpya. 4
3.1.3 Muafaka wa kitaifa. 6
3.1.4 Kutokomeza ufisadi na rushwa. 7
3.2 Agenda katika sekta za kiuchumi 9
3.2.1 Uchumi, uwezeshaji na ajira. 9
3.2.2 Ufugaji chakula na ushirika. 11
3.2.3 Uzalishaji wa mazao. 11
3.2.4 Sekta ya Mifugo. 12
3.2.9 Mawasiliano na uchukuzi 15
3.2.10 Utaifishaji na Ubinafsishaji wa mali za watu binafsi 16
3.2.11 Uwekezaji wa kigeni 16
3.3 Huduma za jamii 17
3.3.1 Elimu na malezi ya taifa. 17
3.3.2 Afya na mazingira. 17
3.3.3 Ulinzi na usalama. 19
3.4 Makundi maalumu. 19
3.5 Vyombo vya habari na asasi zisizo za kiserikali 20
3.6 Usawa wa jinsia. 20KARIBU TANZANIA MPYA
1.0 Utangulizi
Uchaguzi mkuu utakaofanyika oktoba 2020, katika uchaguzi huu litajitokeza tamko lenye kujirudia na maana yenye kukaririwa, sababu katika hilo ni kwamba ilani ya chama na muelekeo wake wa kisiasa pamoja na tamko ni maneno ambayo ndio mwelekeo sahihi kwa ajili ya kutekeleza yale ambayo wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanayapigania kwa ajili ya kujenga Taifa Imara lenye uchumi ambao utakidhi kiu na shauku ya watanzania kuondokana na ujinga, maradhi, umaskini, kukosekana sera madhubuti za kiuchumi pamoja na kukosa elimu bora.

Sisi Chaumma tunaamini kuwa watanzania katika uchanguzi wa mwaka 2020 wanataka mabadiliko ya Mfumo wa kisiasa, uchumi na utawala mpya ambao utawapeleka katika nguzo thabiti katika kushirikiana ili kutukuza miko ya kisheria, kuhifadhi utu na kuepuka Wizi ili kuwajibisha usafi, Ni uchaguzi wa kihistoria, Utatupa watanzania fursa ya kihitoria kufanya mabadiliko ya msingi ya jinsi tunavyotaka kuongonzwa. Ni uchaguzi ambao utakaoamua muelekeo wa Tanzania yetu.Tunatowa wito kwa Watanzania kujifundisha katika njia ya uokovu na kuepuka kufuata kundi la wapotoshaji ambao wanawaita watu ili kuwachaguwa kwa misingi ya ukabila, dini, Rangi zao, ni uchaguzi wa kuandika historia kuepuka kufuata upepo uelekeapo, ni wakati wa kujiangaza na Nuru ya elimu na kuepuka kurejea makosa ambayo yamepelekea uchumi wa nchi kuwa ombaomba na tegemezi.

Watanzania tutakuwa na chaguo la wazi la kuamua iwapo tunataka Tanzania tuendelee na Mfumo na Mdororo na uongozi usio na dira na sera za ukandamizaji, ni wakati wa kufanya maamuzi bila ya woga, na kuacha kuilaumu asubuhi ya majuto (Kufanya makosa siku ya uchaguzi) tukatae kuchagua Chama Cha Mapinduzi ambacho kimeshindwa kuleta mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi, Nidhahiri kuwa Asubuhi ya uchaguzi imeota mwanga kwa mwenye macho kwasababu watu ni maadui kwa wasioyajua, Matunda ya kutojali ni majuto, na Matunda ya uoni wa mbali ni usalama, mwenye kutii uzembe na kushindwa kufanya mabadiliko ya kiutawala atapoteza haki zake kwa njia ya giza, uchaguzi ni kioo cha kufikiri na kuchukuwa hatua kutokana na vile vinavyotuzunguka ili kuchukuwa tahadhari na itoshe kukataa umaskini na kuutupilia mbali kwa kuchanguwa viongozi wa Chaumma ambao watakuwa na elimu ya kuita kwenye matendo ya kisiasa na kiuchumi yakutosha elimu yako ya kufanya maamuzi kuondokana na umaskini na kukataa kuchanguwa sera zisizo na muelekeo za chama kinachotumia nguvu ili kubaki madarakani, kuvunja katiba na sheria zinazosimamia Haki.Muelekeo wa Chama cha Ukombozi wa UMMA ni kuamsha watu waliolala usingizi kwa kukosa kuwa na makusudio ya maendeleo kwa kusimamia kodi na kutozidisha kodi kuongoza kwa uadilifu na kujihadhari dhidi ya utawala wa mabavu pasipo na Haki, kwasababu ushupavu pasipo na Haki huleta mafarakanano na kujipindisha mbali na uadilifu husababisha mapambano na umwagaji wa damu.

Katika kurasa za ilani ya uchaguzi za Chaumma utaona ni kiasi gani tumejiandaa kukutimizia hayo. Tupe ridhaa yako na kwa pamoja tujenge Tanzania mpya yenye Mamlaka kamili na neema kwa wote.

CHAUMMA NGUVU YA UKOMBOZI.

………………………………………………

HASHIM RUNGWE SPUNDA ALI O. JUMA

MWENYEKITI TAIFA KATIBU MKUU TAIFA


2.0 HALI YA NCHI 2020
Chama cha ukombozi wa Umma mnamo 4 Juni ,2013 kilisajiliwa kuwa katika orodha ya vyama vya siasa hapa Tanzania, na kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 2015 CHAUMMA kilishiriki Uchaguzi Mkuu kwa kusimamisha Wagombea katika nafasi ya Ngazi ya Uongozi Kuanzia Rais Wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mgombea katika nafasi ya Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Wabunge, Wawakilishi, na Madiwani. Katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 Mgombea katika nafasi ya Rais wa Jamuhuri Ya Muungano wa Tanzania alikuwa Ndugu HASHIM RUNGWE SPUNDA ambaye katika matokeo ya jumla ya Tume ya Uchaguzi (NEC) alipata idadi ya kura 49,256 sawa na asilimia 0.32, na Mgombea katika nafasi ya Rais wa Zanzibar alikuwa Ndugu MOHAMED MASSOUD RASHID ambapo matokeo ya uchaguzi yalifutwa isivyo halali na pasipo sheria wala Amri ya Mahakama Kuu na Matakwa ya Wananchi wa Zanzibar yalipuuzwa kwa mujibu wa Mkataba wa Kimataifa.

UN General Assembly,(1997) endorsed the Rio Declaration’s provision on access and specifically resolved that: “Access to information and broad public participation in decision – making are fundamental to sustainable development, the Copenhagen Programme of action affirmed the obligation to enable and encourage access by all to a wide range of information and recognized that an open political and economic system require access by all to knowledge, education and information. A Resolution in a 1998 Report, clarified the meaning of freedom of information under Article 19 of the ICCPR in unequivocal terms as imposing a positive obligation on states to ensure access to information, particulary with regard to information held by Government in all types of storage and retrival systems.

Katikati ya kipindi cha miaka mitano ya awamu ya Tano, wananchi walijionea wenyewe jinsi ambavyo serikali ya awamu ya Tano ilivyoshindwa kushughulikia ufisadi wa Ununuzi wa Ndege kwa sababu matumizi ya Fedha za ununuzi wa Ndege hizo hazikupitishwa katika Muswada wowote katika Bunge la Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania,pamoja na miradi mikubwa ya ujenzi pamoja na kutokuwepo uwazi wa matumizi.

Katika hali ya siasa, taifa letu limepita katika utawala mgumu kutokana na ukandamizaji wa demoskrasia pamoja na zuio lisilo la kisheria kwa vyama vya siasa kuzuiliwa kufanya mikutano ya hadhala kutafuta wanachama wapya ili kujenga ushindani sawa katika uchaguzi Mkuu katika hatua hiyo Utawala umeshindwa kabisa kubadili katiba ya nchi iwe ya kidemokrasia Zaidi na wenye uwezo wa kutetea haki za binaadamu, kiuchumi, kijamii, na haki za kisiasa za wananchi wetu.

Hivyo makundi mbalimbali na hasasi za kiraia pamoja na watetezi wa haki za kibinadamu wameathirika kwa kushindwa kutekeleza shughuli zao kwa uwazi pamoja na vitisho kutoka vyombo vya dola na usalama jambo ambalo lilipelekea mazingira magumu kwa wananchi kujengwa katika mazingira magumu kwa kuishi katika hofu na kudhalilika na pale endapo wananchi wakidai Haki hizo wanashindwa kuzipata pasipo mafanikio bila ya mafanikio ya kupata Haki zao.

Chama chetu kimebaini kuwa kiini cha matatizo tulionayo ni udhaifu wa kiuongozi na dira zisizo sahihi za kiutawala zilizomo katika katiba, sheria mbovu na taratibu dhaifu. Ili kuleta ufumbuzi wa matatizo haya chama chetu kinaweka kipaumbele ajenda zifuatazo katika uchaguzi wa Mwaka huu 2020.

3.0 Ajenda zetu katika uchaguzi wa 2020
3.1 Ajenda za kiutawala
3.1.1 Katiba mpya

Pamoja na Bunge maalumu la Katiba kupitisha Katiba pendekezwa ya mwaka 2014,Katiba inayopendekezwa ni kinyume na matakwa ya Wananchi katika Rasimu ya Katiba iliyoandaliwa na Tume ya mabadiliko ya Katiba baada ya kukamilisha kazi ya kuratibu, kukusanya, kuchambua na kutathmini maoni ya wananchi kuhusu katiba Mpya kwa mujibu wa kifungu 20 (3) cha Sheria ya mabadiliko ya Katiba ,sura ya 83 na Tangazo la Serikali Na.30 la tarehe 14 Februari, 2014.

Katiba pendekezwa imetupilia mbali matakwa ya wananchi walio wengi juu ya muundo wa suala la muundo wa serikali Tatu limechukua nafasi kubwa yakurejesha muundo wa serikali mbili ambazo zimepitwa na wakati,Muundo wa serikali mbili umekuwa na utata na malalamiko ya wananchi wa pande zote mbili kiasi cha kufunika mapendekezo yaliyomo katika rasimu iliyo pendekezwa na wananchi.

Katiba inayo pendekezwa imeanzisha mgogoro kabla ya kupigiwa kura ya Maoni ni dhahiri kuwa Katiba inayopendekezwa imeongeza kero za muungano baada ya kuondoa na imerithi kero zilizomo katika katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 na kuufanya muungano wa nchi mbili kuwa ni wenye mashaka kwa sababu Katiba pendekezwa imehodhi kwa nguvu ardhi na mipaka ya Zanzibar ambayo haimo katika Mkataba wa kuanzishwa kwa Muungano ni dhahiri kuwa Tanzania bara imekusudia kuimeza Zanzibar kwa nguvu kwa kuvaa koti la Muungano kwa kupitia koti la Muungano katika Katiba pendekezwa.

Katika Serikali ya Chama cha Ukombozi wa Umma kitahakikisha kuwa rasimu ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika bunge maalumu la katiba la Machi 2014 itarejeshwa kwa utekelezaji kama ilivyopendekezwa na wananchi.

Kwa mujibu wa mageuzi haya,lengo la Chaumma ni kuwa na katiba mpya itokanayo na wananchi wenyewe katika mambo yafuatavyo:
 • Itaainisha misingi na maadili ya utaifa kutokana na rasimu pendekezwa, misingi ambayo itadumisha Haki,Muungano, Maelewano, Amani na Umoja.
 • Itaweka sheria mpya za uchaguzi utakaowawezesha wananchi kupata haki. Mfumo huo utaanzisha uchaguzi huru na Haki katika ngazi zote za uchaguzi. Itaamuru kuwepo na tume huru ya uchaguzi na itaweka masharti ya uundwaji wake;
 • Itapeleka muswada katika Bunge la Jamuhuri kutunga sheria mpya ya uchaguzi kuweka mazingira huru na sawa kwa wote kushiriki na kushindana katika uwanja ulio sawa.
 • Itaweka misingi ya mgawano wa mamlaka katika mihimili ya dola itakayoondoa utaratibu wa hivi sasa wa mihimili hii kuingiliana katika utendaji wa wajukumu yake na itaondoa utaratibu usiofaa wa kuwapa watumishi wa mihimili hii kinga ya kutoshtakiwa,Mfano Spika wa Bunge kujipa mamlaka ya kudharau amri za mahakama na maamuzi ya vikao vya vyama vya siasa Itaweka usawa wa kijinsia katika kutekeleza mfumo mpya wa uchaguzi.
 • Itatamkwa katika Katiba kuwa utaifa ni muungano wa Nchi mbili zilizo huru rasmi utaifa wa Watanzania nakuweka vigezo vya uraia.
 • Itaanzisha mahakama ya kudumu ya katiba itakayopokea na kusikiliza masharti ya kikatiba, raia binafsi au taasisi.
 • Bunge na baraza la wakilishi litakuwa na nguvu na chombo cha kutetea maslahi ya wananchi na kutunga sheria pamoja na kuoneshwa hadharani kupitia vyombo vya habari utendaji wa bunge namna unavyosimamia utendaji wa shughuli za Serikali. Kuwa na uamuzi wa mwisho katika utungaji kupitisha au kukataa uteuzi wa viongozi muhimu wa dola.
 • Itatenganisha wizara za muungano na zile ambazo sio za muungano.
 • Itatenganisha madaraka ya Rais wa jamuuhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Tanzania bara na Rais wa Zanzibar.
 • Itaweka muundo wa muungano wenye dola la shirikisho baina ya Tanganyika na Zanzibar ambayo itakuwa ndio Tanzania.
 • Itaainisha haki za binaadamu kwa viwango vinavyokubalika kimataifa ikizingatia utu huru mwafrika na utamaduni wake.
 • Itaruhusu wagombea huru wa nafasi ( udiwani, ubunge, na urais)
 • Itatilia mkazo uhuru wa mahakama pasipo kuingiliwa na kuamuru Bunge,Baraza la wawakilishi litunge sheria itakayorahisisha utoaji na upatikanaji wa Haki pamoja na kuwachukulia hatua watendaji wanaopokea maelekezo namna ya utoaji Haki kwenye vyombo vya maamuzi nchini itahakikisha ardhi na maliasili ya Tanzania na bara vinawanufaisha watanzania bara na ardhi na maliasili itainufaisha Zanzibar na haitakuwa mali ya muungano. utoaji na upatikanaji wa haki kwenye vyombo vya maamuzi nchini;
3.1.3 Muafaka wa kitaifa
Chaumma imezingatia maoni ya wananchi na imependekeza mambo kadhaa kubwa ni kuweka dira ya taifa.Sura pili yote ya Katiba inazungumzia dira ya Taifa.Madhumuni ya kuweka Malengo muhimu na Misingi ya shughuli za serikali ni kuhakikisha kuwa Serikali na manlaka zake zinapewa mwongozo wa kisera na mwenenlekeo wa kiutendaji.Pamoja na mambo mengine malengo yafuatayo yamewekwa kwa ajili ya wakulima, wafugaji ,wavuvi n awachimbaji wadogo wadogo wa madini.
 • Kuweka mazingiara bora ya uzalishaji wa mazao kwa wakulima,wafugaji ,wavuvi na wachimbaji wdogo wadogo wa madini wanakuwa na ardhi na nyenzo kwa ajili ya kuendeleza shughuli zao.
 • Kuweka mazingira bora kwa ajili kuanzisha n akuendeleza vyombo vya uwakilishi wa wakulima,wafugaji ,wavuvi na wachimbaji wadog wadogo wa madini(Social workers having special interst on ecology and environment)
 • Kuweka utaratibu mzuri wa upangaji wa usimamiaji wa mizani ya bei za mazao na pembejeo
Haki ya kumiliki mali itajumuishwa kiutekelezaji kwenye haki za binadamu, na hivyo, haki ya elimu bora ya msingi itapewa kipaumbele bila malipo kwa ubora ambao utakuza kiwango cha Elimu katika soko la Elimu kimataifa.

Wananchi walio wengi hawaridhishwi kwa kuporomoka maadili ndani ya jamii na ndani ya Uongozi wa Umma kwa Kiwango kikubwa.Hivyo Chaumma itasimamia na kuweka sheria zitakazo linda utamaduni ,mila, desturi za kila upande Tanzania bara na Zanzibar.

Kwa kuzingatia maoni ya wanachi na Taarifa ya utafiti,tume inapendekeza viongozi wa umma na miiko ya uongozi yawekwe katika Katiba.

Maadili ya Taifa lazima pia yaweke misingi ya kuheshimu itikadi za vyama vya siasa na wananchi ilivyo hivi sasa katiba ya nchi inatambua itikadi ya chama kilichoko madarakani siasa ya Ujamaa na kujitegemea kuwa ndiyo itikadi ya taifa ,wakati Katiba ni ya kudumu ya wananchi.

Hivyo wote tunajua kuwa taifa likishakubali mfumo wa vyama vingi haliwezi tena kufuata itikadi ya kisiasa ya chama kimoja,maadili ni pamoja na kutambua nafasi ya walemavu na vingozi wa dini katika maisha na maendeleo ya jamii. Mpaka sasa hakuna sheria inayolinda Haki za viongozi wa dini katika Taifa jambo linalo pelekea viongozi hao kukandamizwa,kunyimwa na kuwekwa kuzuizini kwa muda mrefu pasipo kutendewa haki inayostahiki kwa mujibu wa Katiba ya Nchi,Viongozi wa dini umuhimu wao hauonekaniki hadi pale nchi inapopata majanga,Mfano ukame,mafuriko,tetemeko la ardhi,covid-19 corona n.k hapo viongozi wa serikari huwaomba viongozi wa dini kufanya maombi kuondokana na majanga hayo pasipo kutambua umuhimu wao.

CHAUMMA itawatambua na kuwalinda viongozi wa dini kuwa ni walinda Amani ya mioyo ya watanzania na hivyo itawahifadhi na kuheshimu hadhi zao za kidini pasipo ubaguzi na hawatoweka kizuizini kwa makosa ya kuzingiziwa na endapo watapelekwa Mahakamani kesi zao zitasikilizwa kwa haraka na kutolewa uamuzi kwa mujibu wa sheria za Nchi.

3.1.4 Kutokomeza ufisadi na rushwa
Tangu mwaka 2015, maudhui ya ilani za uchanguzi za chama cha CHAUMMA kila mara yameelezea kuwa Rushwa ni balaa na tishio kubwa kwa taifa letu. Kwa sasa hali ni mbaya Zaidi, tunakabiliwa na Ufisadi.

Ufisadi kwa tafsiri yetu, ni uozo na uvundo wa dola na utawala wanchi. Uozo huu unaambatana na Rushwa inayoliguguna taifa na kuliangamiza. Serikali imegeuka kuwa la kifisadi kwa kuwa taratibu zake za kiutendaji, sera na kanuni zake hazijengi kuondoa ufisadi. Watendaji wa serikali na watumishi kadhaa wamegeuka mafisadi, rushwa imekolezwa kwa kufichwa ukweli wake tumelishuhudia hilo katika ripoti ya mkaguzi mkuu wa serikali (CAG) kutoka mwka 2016 – 2019 uwozo mkubwa wa matumizi mabaya ya fedha za umma pasipo bunge kuchukua hatua kwa maana hiyo bunge limekuwadhifu kuhoji matumizi mabaya ya fedha na kushindwa kuwajibika kama muhimili wa dola.

Hivi sasa Tanzania imekuwa Taifa lenye sifa yenye sera ya vitisho na matamko makali, Chama cha CHAUMMA kinatangaza rasmi kuwa rushwa na ufisadi ni adui wanne wa taifa. Chama cha CHAUMMA kimedhamiria kutokomeza ufisadi na rushwa kwa kutekeza mkakati ufuatao:
 • Kutengeneza vyombo vyenye nguvu kubwa na mtandao ulioenea Nchi nzima , Chombo chenye meno makali ya kutokomeza ulaji rushwa kiutendaji.
 • Kuunda dola kwa kuzingatia waledi, uwezo kitaaluma na maadili ya uongozi kwa watendaji na viongozi wa umma
 • Kuvipa uhuru mkubwa vyombo vya habari ili viandike bila hofu ufisadi utakao bainika katika taasisi yoyote nchini. Kwa muundo wa sasa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za serikali mara baada ya ripoti ya hesabu za ukaguzi kutolewa Takukuru imekuwa na mipaka ya kuwashughulikia vigogo wa serikali ambao wana hujumu fedha za serikali.
 • Kulinda haki ya kila raia kupata na kutoa habari ili kwa kufanya hivyo uwezekano wa kuficha siri za kifisadi kuondolewa, nakuhakikisha kwamba serikali inatoa taarifa za uendeshaji wa shughuli za umma kwa vyombo vya habari na asasi za kijamii zinazolinda na kutetea haki.
 • Kuelimisha,kulea na kufunda watumishi na viongozi katika misingi ya uadilifu na uongozi bora. Hili litaendana na kujenga taifa adilifu kwa njia ya elimu kwa watanzania tangu wakiwa na umri mdogo na kuwakuza katika madili mema.
 • Kurahisisha mfumo wa ulipaji kodi na kupunguza kiwango cha kodi ili kuwahamasisha wananchi kulipa kodi, ili waondokane na kishawishi cha kutoa rushwa badala ya kodi.
 • Kufuta umangimeza,kurahisisha taratibu za utoaji wa haki na huduma kwa umma kutoka taasisi za kiserikali.
 • Kuwafikisha mara moja mbele ya sheria watuhumiwa wote wa vitendo vya kifisadi.
 • Kuandaa mswada wa sharia itakayotoa adhabu kali Zaidi kwa walaji na watoa rushwa
 • Kufuta mara moja mikataba yote iliyosainiwa katika mzingira ya kifisadi.
 • Kutengeneza taratibu za kusaini mikataba ya serikali itakayo kua wazi kabisa mbele ya umma wa watanzania kabla ya mikataba hiyo kuwekwa saini.
3.2 Agenda katika sekta za kiuchumi
3.2.1 Uchumi, uwezeshaji na ajira

Mabadiliko ya kiutawala tuliyoyaeleza yanalipa taifa fursa na uwezo wa kutekeleza mageuzi ya kujikombao kiuchumi.Tunapozungumza uchumi tanamaanisha jumla shughuli zote za kuzalisha mali na utoaji wa huduma mbali mbali kaatika jamii, maadam vyote vinathamani inayoweza kupimwa kwa fedha. Matokeo ya shughuli za kiuchumi ni upatikanaji wa mahitaji ya wanadamu katika jamii husika. Katika kila jamii mgawanyo wa mafao au mahitaji huzaa matabaka ya walionacho na wasionacho.Kipimo cha maendeleo ya jamii yoyote ile ni uwezo wake wa kukidhi mahitaji ya lazima ya wanajamii walio wengi katika jamii husika.

Tanzania ni taifa la muungano wa nchi mbili ambazo kila upande umebeba utajili wa rasilimali zake lakini umma wa vijijini ambao wanashindwa kuuza katika soko lenye ubora wa bei,na kuwafanya kuendela kukosa mitaji ya kuwawezesha kujikwamua kiuchumi, umma walio wengi wanashindwa kupata mlo wa kutosha na hivyo kuishia kuishi kwa mazoea ili kupata ridhiki ya mlo usio na uhakika,mzunguko wa fedha umekuwa mdogo katika soko na bidhaa kupanda bei.

Tanzania inajengwa na umma na makundi mawili makubwa ya umma wa Tanzania.kundi la wafanya kazi ni la pili kwa ukubwa kufuatia kundi la wakulima na wafugaji. Makundi haya yameathirika sana na uchumi duni tulionao. Utafiti unaonesha kuwa kwa kipindi cha miaka mitano ukuaji kiuchumi kwa kiwango cha kati hauendani na maisha halisi ya Mtanzania ndio maana serikali imeshindwa kuongeza mishahara kwa wafanyakazi wake, mbali na hayo serikali imeshindwa kusimamia mazao ya wakulima kwa kupata soko la uhakika la ndani na nje na leo tunashuhudia uporomokaji mkubwa wa mazao kama Korosho,kahawa,chai,katani,karafuu, laslimali za misitu.

Serikali inayoongozwa na chama cha CHAUMMA itafanya mambo yafuatayo.

 • Kuinua uchumi
 • Itakua na mkakati wa makusudi wa kimarisha uchumi wa Tanzania
 • Itahakikisha mauzo ya bidhaa nchi za nje yanaongezeka kwa asilimia kubwa, nakupunguza bidhaa kutoka nje ili kulinda viwanda vya ndani ,kwa mfano uhaba wa sukari imekuwa janga kwa taifa kwa kipindi cha miaka mitano,umekuwa mdogo na kushindwa kukidhi mahitaji.
 • Serikali ya Chaumma itabuni njia na kuboresha mikopo isio na masharti magumu.
 • Serikali Italinda utajiri wa rasilimali tulizonazo na kuziwekea mkakati endelevu wa kuzitumia ili kuinua uchumi wa nchi.
(b) kuwezesha wananchi
1)
Serikali ya Chaumma itaandaa mikopo ya fedha kwa wahitimu wa vyuo kimataji wahitimu kutoka vyuoni\mashuleni pamoja na wananchi kwa ujumla kuanzisha miradi mbalimbali ya uchumi ndani na nje ya nchi.

2) Serikali ya Chaumma inaweka mikakati kwa wanachi kujiamini,kutambua na kutukmia uwezo wao wa kufanya kazi na kubadili changamoto ya sayansi,teknolojia na utandawazi.

3) Serikali ya Chaumma wananchi kushiriki katika soko la dunia kwa kutoa vivutio, vishawishi na motisha mbalimbali kwa washiriki wa soko la nje kwa sababu watanzania katika soko la nje wamekuwa nyuma na wasio kuwa na muamko.

4) Italinda maslahi ya taifa katika mikataba ya biashara ya uchumi katika soko la ndani na nje.

(c) Wafanyakazi
1)
Itawawezesha wafanyakazi kupata mishahara bora .

2) Itaandika upya sheria ya vyama vya wafanyakazi ili kuvipa vyama hivyo uhuru Zaidi wa kulinda na kutetea maslahi ya wafanya kazi,kupanua ushiriki wake katika uendeshaji wa mifuko ya hifadhi ya jamii.

3) Itaongeza pensheni za wastaafu ili wastaafu wapate kiwango cha 80% ya mishahara yao na pia hukakikisha kuwa serikali inachangia mifuko hiyo badala ya kuitumia tu kama chanzo cha mikopo kwa miradi ya serikali tumeshuhudia kuwa wafanyakazi wastaafu hawafaidiki na fedha zao kwa kuwa fedha zao hazitumiki katika miradi yao ya umma.

4) Itahakikisha kua wastaafu wanalipwa penshenni zao mara tu wanapostaafu. Hii ni pamoja na kuwarejesha katika malipo ya pensheni wanachama wa mfuko wa hifadhi ya jamii wa mashirika ya umma walioondolewa baada ya marekebisho ya mfuko huo,

5) Itaruhusu, itahalalisha na kuzijengea mazingira mazuri shughuli zote ambazo wananchi watazibuni kwa ajili ya kujipatia riziki.

3.2.2 Ufugaji chakula na ushirika
3.2.3 Uzalishaji wa mazao

Mpunga

Mabonde ya mpunga bado hayajaweza kuendelezwa kwa ukamilifu, yale yaliyowezwa kuendelezwa kwa kiasi miaka ya nyuma yanazidi kupotea kutokana na kukosekana kwa maji,pembejeo, sera na mipango madhubuti ya uzalishaji na masoko. Lakini pia upanuzi wa matumizi ya ardhi ukiwemo ujenzi holela wa makaazi na shughuli nyengine zisizo za kilimo ndani ya ardhi yenye rutuba, pia imesababisha kukatwa miti mingi, hasa mikarafuu na minazi, kupotea kwa misitu ya asili na ardhi yenye rutuba.

Viwanda
uzalishaji wa viwanda umeingia katika migogoro isiyoisha baina ya wawekezaji na wananchi na hali imekua mbaya Zaidi kwa serikali iliyopo kushindwa kusimamia haki na uadilifu baina ya wananchi wawekezaji binafsi wa sekta hii ya viwanda. Wafanyakazi wanashindwa kupata stahiki zao na kupunjwa stahiki zao wakulima wa miwa wanaendelea kubezwa na maslahi yao kupujwa.

Tanzania ina aina nyingi ya viwanda , lakini kuna viwanda vichache vya kusindika na hivyo vilivyokuwepo vipo duni sana , kwa hiyo vinashindwa kuongeza pato la taifa na kutoa ajira kwa vijana. Hakuna takwimu sahihi za kitaifa zinazoonekana kupima hali halisi Tanzania. Mara nyingi umuhimu wa mazao ya matunda kama, mananasi,embe,Machungwa,mafenesi,umekua ukibezwa na kuoza hata kukosa nafasi katika sera na mipango ya taifa.

Katika kuzishughulikia changamoto hizi na kufikia azma ya uchumi wa viwanda vya kilimo na uzalishaji, Serikali itakayoongozwa na CHAUMMA itakekeleza ifuatayo:

Kuwawezesha wananchi kuanzisha miradi mbalimbali ya kilimo kuzalisha mazao ya kilimo, pamoja na viwanda vya kusindika bidhaa za kilimo.

Kuwawezesha wananchi kujenga viwanda mbalimbali vya bidhaa za matumizi ya binadamu.

Bandari
Kupanua na kuwa na bandari huru, bandari ya Tanga kwa ajili ya soko la Afrika Mashariki,bandari ya Bagamoyo kwa ajili ya soko la kiuchumi la biashara kwa nchi za SADAC bandari ya Mtwara kwa ajili ya soko la kusini mwa Afrika na Bandari za Dar es salaam na Zanibar kwa ajili ya soko la Kimataifa.

Kuanzisha ujenzi wa uchimbaji wa bahari kutoka bahari ya hindi kwenda Dodoma na kuanzisha bandari ikayorahisisha soko la Afrika.

Inawezekana kuyatekeleza hayo kwa sababu Mfano hai ni Nchi ya Misri iliingia mkataba wa kimataifa na Kampuni ya ujenzi ya kigiriki juu uchimbaji wa bahari katika ardhi yake kavu yenye urefu wa miles 120,ujenzi na uchimbaji wa suez canal hadi kukamilika kwake ulichukua miaka kumi na ulikamilika mnamo mwaka 1868.

Nchi ya Miri ilishindwa kulipa gharama za uchimbaji na ujenzi na iliiingia mkataba na kampuni ya uchimbaji kuwa uendeshaji wa suez canal utakuwa mikononi mwa kampuni ya kigiriki hadi Misri itakapokuwa na uwezo wa kulipa gharama za ujenzi,mnamo mwaka 1963 Misri iliweza kulipa gharama hizo kwa kampuni ya uchimbaji na ujenzi, kutokea muda huo hadi sasa nchi ya misri imeweza kujenga uchumi mkubwa kutokana na faida ya ujenzi wa mfereji wa suez canal.

3.2.4 Sekta ya Mifugo
 • Ufugaji kwa Tanzania bado unafanywa kwa njia za kienyeji na haujatoa mchango mkubwa katika uchumi wa taifa. Wananchi wa Tanzania wanaoishi katika ardhi yenye rutuba nzuri na wamekua na utamaduni mzuri wa ufugaji na iwapo ufugaji utapewa msukumo unaweza kuchagia vizuri katika kunyanyua hali za maisha ya wafungaji wetu na Uchumi wa Tanzania bara utaimarika kwa njia za viwanda vya ngozi kwamba tukiamua tunaweza hata kuwa na viwanda vya bidhaa zitokanazo na mifugo ikiwemo, maziwa, samli, siagi na jibini.
 • Kwa mujibu wa takwimu za mifugo Afrika , nchi ya mwanzo inayoongoza kwa mifugo na kunufaika na rasilimali za mifugo ni nchi ya Ethiopia na nchi ya pili ni Tanzania kwa kua na wingi wa mifugo ya wanyama , lakini imekua hainufaiki vya kutosha kutokana na kushindwa kultumia soko la kimataifa katika biashara zitokanazo na rasilimali za mifugo , Serikali imeshindwa kuwahamasisha wanachi na kuwatafutia masoko ya kimataifa kuuza bidhaa kama Nyama , Ngozi na Mazalia yake kwa mfano Nchi ya Saudi Arabia kila mwaka inanunua kutoka nje ya nchi mbuzi na kondoo wapatao milioni kumi na tano (15,000,000) lakini Tanzania tumeshindwa kulitumia soko hilo amabalo ni mtaji mkubwa wa kibiashara kwa Taifa letu. Aidha tumeshindwa kutumia soko la jumuiya ya Ulaya kwa aajili ya kuuza bidhaa zetu.
 • Serikali itakayo ongozwa na Chama cha Umma itatekeleza mambo yafuatayo,
 • Kujenga viwanda vya zana za kisasa za kilimo na mifugo.
 • Kutoa ruzuku kwa wafugaji na wakulima,na fidia au upendeleo katika kodi kwa ajili ya kuendeleza kilimo na mifugo.
 • Kujenga viwanda vya kusindika bidhaa za kilimo na mifugo.
 • Kufufua huduma za ughani katika kilimo na mifugo
 • Kufufua na kupanua vyuo na taasisi za utafiti wa kilimo na mifugo
 • Kuanzisha masoko ya kimataifa ya mazao yatokanayo na kilimo na mifugo katika miji ya mipakani.

.Uvuvi wa bahari,maziwa na mito
 • Takwimu ya karibuni ya sekta ya uvuvi iliyofanya utafiti juu ya uvuvi wa bahari,maziwa na mito,kupitia miradi mbalimbali ya uvuvi inaonyesha kuwa uvuvi wa samaki katika bahari ulifikia tani 80,000 kwa mwaka 2018 na kuingiza wastani wa thamani ya shilingi Bilioni 323/- ,Uzalishaji katika sekta hii ya uvuvi katika kipindi cha miaka kumi na mbili ulionyesha wastani wa ongezeko la asilimia 9.7% kwa mwaka. Takwimu pia zinaonyesha kuwa bandari za kuuzia samaki inapanuka.
 • Uchumi wa bahari kuu (exclusive economic zone ) ni swala linalosimamiwa na mikataba ya kimataifa kwa sheria ya bahari chini ya United Nations on the Convention on the law of the sea(UNCLOS). Tanzania ni mwanachama katika mkataba huo lakini uvunaji wa rasilimali hizo umekuwa na mgogoro ndani ya Tanzania baina ya Tanzania bara na Zanzibar.
 • Tanzania bara inaendelea kuvuna raslimali za bahari kwa kuchimba gesi katika bahari tokea mwaka 2005 na mapato yatokanayo na mafuta na gesi yananufaisha Tanzania bara pekee pasipo Zanzibar kunufaika wala kushirikishwa.
 • Zanzibar imekuwa inasuasua katika utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi hali hiyo inatokana na kuwekewa vikwazo na Tanzania bara kwamba Mafuta na gesi ni raslimali za muungano,uvunaji wa mafuta na gesi hauna faida wala tija kwa upande wa Zanzibar na hivyo kuifanya Zanzibar kuwa kitega uchumi cha Tanzania bara,kwa muktadha huo ndio Chama Cha Mapinduzi kinasisitiza kuwa kinataka mfumo wa muungano wa serikali mbili kuelekea serikali moja ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania kwa lengo kuimeza na kuipoteza hadhi ya Zanzibar kitaifa na kimataifa.
 • Mpango wa Tanzania ni kuvuna mafuta na gesi ambayo ni raslimali ya Zanzibar kuifanya kuwa ni faida ya kiuchumi kwa upande wa Tanzania bara ushahidi wa hayo unapatikana katika katiba pendekezwa ya mwaka 2014 kuifanya ardhi kuwa raslimali ya muungano wakati ardhi sio sehemu ya orodha ya mambo ya muungano.
 • Serikali itakayo ongozwa na Chama cha Ukombozi wa Umma itatekeleza yafuatayo:
 • Mafuta na gesi yatokanayo na mazao ya bahari hayatakuwa mambo ya muungano, Tanzania bara itanufaika na raslimali zake na Zanzibar itavuna na kutumia raslimali zake.
 • Serikali ya Chama cha Umma itatoa ruzuku kwa wavuvi na fidia wanapopata hasara na kupunguza kodi kwa ajili ya kuendeleza uvuvi.
 • Itaanzisha na kuboresha vyuo vya uvuvi na kuanzisha taasisi zenye nguvu juu ya utafiti wa mazao ya bahari,maziwa na mito.
 • Itatafuta masoko ya bidhaa kimataifa juu ya mazao yatokanayo na uvuvi.

Utalii

 • Tanzania bado haijafanya juhudi kubwa kuwekeza katika uchumi wa utalii na hivyo wanachi walio wengi hawafahamu faida itokanayo na utalii,utalii wa bahari na uwekezaji ambao unatoa mchango mkubwa katika pato la taifa haukutangazwa na kuwekewa mikakati madhubuti kimkakati, mapato yatokanayo na utalii ni kidogo kulinga na vyanzo vya utalii vilivyopo Tanzania ambavyo ni tunu na lulu inayopendeza,serikali imeshindwa kuwekeza utalii wa kisasa katika mbuga za wanyama na hivyo kukosa mapato kwa kiwango kikubwa, aidha chama cha mapinduzi kimeshindwa kutumia fursa ya wananchi kushika dola kuufanya utalii kuwa sehemu ya uchumi wa nchi,utalii wa Tanzania umekuwa ni utalii wa burudani na starehe usioendana na ushawishi wa kimataifa ili kuwavutia watalii wengi wa nje kuzuru Tanzania na kuwekeza.
 • Uchumi wa visiwa vya Zanzibar ulipaswa kutegemea mapato yatokanayo na utalii lakini uwekezaji wa utalii Zanzibar hauna hadhi ya kimataifa hivyo watalii wanaoingia Zanzibar ni watalii wa daraja la tatu ambao kipato chao ni cha chini, na hivyo umma wa wanzanzibari kutonufaika na utalii kwa kiwango cha uchumi wa kipato
 • Hakufanyika jitihada za kuwasaidia wavuvi kusafirisha samaki nje za nje. Zaidi ya asilimia 90 ya samaki huliwa au kuharibika nchini. Uvuvi haramu umeongezeka na kusababisha kupugua kwa uzalishaji wa baharini na katika maziwa . Uharibufu wa matumbawe na maeneo mengine ya mwambao wa bahari unaoendelea bila ya jitihada zozote za kufuata suluhisho la kudumu la kuondoa migogoro baina ya wavuvi na wawekezaji wa sekta ya kitlii.

Utamaduni
 • Serikali ya Chama Cha Umma itatunga sheria ya kulinda na kuendeleza utamaduni wa taifa ikiwa ni pamoja na kukamilisha ubunifu juu ya vazi la kitaifa lenye heshima.
 • Itakipa Kiswahili hadhi inayostahili kama lugha rasmi ya taifa na kuunda taasisi ya kuendeleza Kiswahili na utamaduni wetu ndani nan je ya nchi.Pamoja na kutumia lugha ya kiingereza mashuleni ili kuwa lugha ya pili kitaifa kwa ajili ya biashara ya kimataifa.
 • Itawezesha na kuimarisha miradi ya raia ya kuendeleza fani zinazoelezea utamaduni kama vile muziki, michezo, ngoma, filamu, uchoraji,ufinyanzi uchogani na sanaa nyenginezo hii ni pamoja na kuwawezesha wasanii na kulinda na kulinda haki ya kazi zao.
 • Pia itaanzisha vyuo kuendeleza utamaduni wa taifa na fani zinazoelezea utamaduni wa taifa
 • Itaanzisha program maalumu ya kuwezesha vijana wenye vipaji katika kila fani zinazoelezea utamaduni wa taifa,ili kukuza ajira kwa vijana uzalishaji wa bidhaa za utamudini na kuinua pato taifa
 • Utaimrish ushirikiano kati ya serikal za mitaa,taasisi za kidini na jamii ktika kujenga maadili na utamaduni wa taifa.
 • Itajenga miundombinu ya michezo, ili kuiwezesha sekta hii kuajiri vijana wanamichezo ndani na nje ya nchi, kwa jinsi hii Tanzania itajiunga katika orodha ya mataifa mashuhuri katika medani za michezo duniani na itajiongezea pato la taifa.
 • Itaruhusu Zanzibar kuomba uanachama wa michezo kimataifa ikiwemo FIFA
 • .
3.2.9 Mawasiliano na uchukuzi
Sekta ya mawasiliano na uchukuzi ni uhai wa uchumi wa taifa inayoweza kulinganishwa na mishipa ya fahamu katika mwili wa binadamu. Serikali itayoongozwa na CHAUMMA, itaendeleza sekta hii kwa kufanya mambo yafuatayo:
 • Itajenga barabara kwa kiwango cha lami ili kuhakikisha kua kila makao ya halmashauri yanafikika kwa barabara ya lami
 • Itajenga mfumo mpya wa usafiri wa barabara na reli katika miji mikubwa ikianzia Dar es salaam ili kuondoa kero ya msongomano wa magari uhaba wa usafiri na kuondoa ajali zinazosababiswa na barabara mbovu na nyembamba
 • Serikali ya Chama Cha Umma itaanzisha ujenzi wa mfumo mpya wa reli za umeme nchini
 • Itahamasisha na kuwawezesha wananchi kujasiriamali katika sekta hii hasa kuanzisha viwanda vya bidhaa za mawasiliano na makampuni ya kutoa huduma ya mawasiliano kwa elektroniki badala ya kuicha sekta hii imilikiwe na makampuni ya kigeni peke yake
 • Itahamasisha na kuwawezesha wananchi kumiliki na kuendesha vyombo vya usafiri wa anga na baharini
3.2.10 Utaifishaji na Ubinafsishaji wa mali za watu binafsi
Kutokana na historia isiyopendeza ya serikali kutaifisha mali binafsi kwa jazba badala ya kuongozwa na sera makini na baadae kubinafsisha holela mali ya umma bila sera makini, serikali itakayoongozwa na CHAUMMA itakabiliana na hali zilizotokana na matukio hayo na kurejesha imani ya wananchi katika serikal yao kwa kufanya mambo yafuatayo:
 • Itaweka masharti kwenye katiba ya nchi ili kuzui utaifishaji wa mali ya watu binafsi.
 • Itatunga sharia inayoiwajibisha serikali kulipa fidia inayokidhi thamani ya mali iliyotaifishwa bila ucheleweshaji wa malipo na pia kuwalip fidia wenye mali iliyotaifishwa bila kulipwa fidia.
 • Itaanzisha mjadala kuhusu ubinafsishaji wa nyumba za serikali ili kungalia upya uhalali wa tendo hilo.
 • Itafuta sharia iliyopo inayoipa serikali mamlaka ya kuchukua ardhi ya wananchi bila kushauriana nao na kutunga sheria mpya inayoweka msharti ya kuiwajibisha serikali kushauriana na wananchi kabla ya kuchukua ardhi, kufanya tathimini ya ardhi inayochukuliwa na serikali kwa bei ya soko,kulipa fidia na kuhakikisha kuwa wananchi husika wamepata makazi mbadala kabla ya bomoa bomoa kufanywa.
3.2.11 Uwekezaji wa kigeni
Wawekezaji wa kigeni ni kichocheo muhimu cha mendeleo ya uchumi wan nchi. Hata hivyo sio sera nzuri kwa taifa husika uwekezaji holela hadi kuwaruhusu wageni kuwekeza katika kuuza na kufanya biashara ndogo ndogo.utaratibu umeleta chuki miongoni mwa wananchi ambao wanaona kama uchumi wa nchi yao umeuzwa kwa wageni, ili kuondoa chuki dhidi ya wawekezaji wa kigeni na kuweka mazingira ya amani, maelewano na utulivu, sekta itakayo ongozwa na CHAUMMA, itafanya mambo yafuatayo;
 • itaainisha na kutenga maeneo ya uwekezji kwa ajili ya wageni na kuhakikisha kuwa wageni hawawekezi katika sekta zilizotengwa kwa ajili ya wananchi
 • Itaweka msharti na kudhibiti ubora wa uwekezaji wa wageni nchini ili kukinga taifa lisivamiwe na matapeli wezi na majangili waliojificha kwenye ngozi ya uwekezaji.
 • Itaweka msharti ya uwekezaji yanayohakikisha kuwa wawekezaji wageni wanakuza ajira, uzoefu na teknolojia kwa wananchi na pia wanabakiza kiasi cha kuridhisha cha pato nchini kwa kuwekeza upya faida yao katika miradi mengine mipya
 • Itawashawishi wawekezaji wa kigeni waliopo nchini kuingia ubia na watanzania kwa manufaa ya watanzania.
 • Itawawezesha wananchi wajasiriamali kuingia ubia na wawekezaji wa kigeni.
3.3 Huduma za jamii
3.3.1 Elimu na malezi ya taifa

Uhai wa taifa lolote hutegemea sana misingi ya kielimu na kimaadili inayowaunganisha wananchi wake kuwa taifa moja lenye utamaduni mmoja.ili kujenga mtanzania kiroho na kiakili, ili tuwe na mafanikio ya kiuchumi na kisiasa na ili tue na taifa lenye utamaduni mmoja hatuna budi kuwa na mfumo wa elimu na malezi ya taifa wenye maudhui na vionjo vya kitanzania.

Ili kufanikisha mageuzi hayo serikali iitakayoongozwa na CHAUMMA itafanya mambo yafuatayo;

Elimu
 • Itabadili mitaala ya elimu kwa kuanzia elimu ya msingi hadi vyuo vikuu ili kuipa ubora wa hali ya juu na maudhui na vionjo vya kitanzania na kimataifa.
 • Itahakikisha kwa mitaala yote nchini ni ile tu yenye manufaa na maana katika misha halisi ya mtu mmoja mmoja.
 • Itaazisha mpango bora wa elimu ya uraia na elimu ya maisha kwa jamii, mahali pa kazi, pamoja kuzipa ruzuku tasisi za dini na binafsi zinazotoa elimu kuziongezea uwezo wa kutoa huduma ya elimu kwa jamii na kuondoa ushuru kwa bidhaa za elimu zinazo zalishwa ndani
 • Kuboresha marupurupu ya walimu na wafanyakazi na kuwekeza katika tafiti wa kisayansi.
3.3.2 Afya na mazingira
Afya ya binadamu hubebwa na mazingira anayoishi.watanzania tunaishi katika mazingira hatarishi kiafya. Jambo ambalo linathibitishwa na magonjwa mengi ya mlipuko na kushindikana, kufuatika wagonjwa kama kipindupindu na homa za matumbo ambayo yanaashiria mazingira machafu chanzo kikubwa cha maradhi hayo ni kukosekana kwa huduma bora za kiafya.

Huduma za tiba zimeporomoka kiasi kwamba hospitali zinazoaminika sasa ni zile zinazoendeswa na sekta binafsi. Hali hii ni hatari kwa kua huduma za hospitali binafsi hakuna vijijini isipokua pale ambapo zipo zahanati za mashirika ya kidini.

Mijini pia hali si nzuri na wakubwa serikalini hujitibia nje kwa fedha za kodi ya wananchi gharama za dawa ni kubwa mno hata kwa dozi ya kawaida ya malaria. Hivyo tumefikishwa pabaya na kifo kinadukodolea macho kila mara tunapojihisi ni wagonjwa.

Ili kuweza kupambana na maradhi na kua na jamii yenye afya njema serikali itayoongozwa na CHAUMMA itafanya mambo yafuatayo;

Afya
 • Itaanzisha program za kudumu vya kudhibiti vyanzo vya magojwa nchini, na kuzuia maambukuzi. Mpango huu utajumuish elimu ya afya kwa watu wote, na uangamizaji wa mazalia ya wadudu wanaoeneza maradhi.
 • Itaanzisha mfumo wa tiba utakao hakikisha kuwa huduma ya afya msingi hutolewa kwa afya yote.
 • Itaimarisha huduma ya afya ya mama na mtoto ili kuhakikisha uzazi salama na kujenga taifa lenye watu wenye afya bora na maish marefu
 • Itawezesha sekta ya tiba ya jadi kwenda kwa wakati uliopo na kuchangia zaidi ya ilivyo sasa katika huduma ya kuzuaia na kutibu maradhi nchini.
 • Itazipa ruhusa taasisi binafsi zinazoshiriki katika utoaji huduma ya tiba ili kuziongezea uwezo wa kutoa hudum ya tiba kwa jamii na kuondo ushuru kwa vifaa vya hospitali.
 • Itawezesha madaktari na watafiti wananchi katika sekta ya afya kuwekeza na kuanzisha hospitali za kisasa zenye uwezo wa kutibu maradhi yote ikiwa na pamoja na dawa kupatikana.
 • Itawahamasisha na kuwawezesha wafamasia wananchi na wawekezaji wengine wananchi kuanzisha viwanda vya utengenezaji w dawa za binadamu na vifaa vya hospitali.
Mazingira na makazi
Kwa kuwa ni haki ya binadamu na msingi mkuu wa afya ya binaadamu kuishi katika mazingira safi na salama, serikali itakayoongwaza na CHAUMMA itafanya mambo yafuatayo kuhusina na masuala ya mazingira:
 • Itatunga sharia ya vyakula, madawa na usafi wa mazigira ambayo itazuia uingizaji nchini bidhaa zizizofikia viwango vinavyokubalilika kitaalaumu na kisheria nchini.
 • Itaweka wazi kwa wananchi, ramani za mipango miji ili watambue ni wapi wajenge na wapi wasijenge. Hii inaambatana na kukomesha ujenzi holelea.
 • Itashawishi vyombo vya fedha, taasisi za serikali na za binafsi kuwekeza katika makazi bora ya watu( ujenzi wa nyumba bora na nafuu) na pia kufanya tathmini ya ardhi (land adjudication plan)
3.3.3 Ulinzi na usalama
Umma tunatambua kwamba moja wapo ya mahitaji muhimu ya mwanaadamu ni usalama ya nafsi yake, jamaa zake na mali zake. Katika taifa letu sasa usalama huu sio wa uhakikika sana. Bado tunashuhudia uwepo wa tishio la vitendo vya ujambazi, unyanganyi, ubakaji, mauwaji ya watu wasio na hatia na maovu megineo. Ili kuwahakikishia wananchi usalama, Chama cha CHAUMMA pamoja na mambo mengine itafanya yafuatayo:
 • Itahakikisha vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vinapatiwa zana za kisasa kabisa ili viweze kumudu kudhibiti uhalifu.
 • Itaweka utaratimu wa kudumu wa kuwapati sikari wetu mafunzo kazini ya mbinu bora zaidi, na kuhakikisha kuwa wamejengeka na kuwa wadilifu wa hali ya juu.
 • Itaweka vituo vya ulizi karibu sana na wananchi, lengo ni kuwahakikisha kuwa vijiji vyote nchini vinapatiwa vituo vya ulinzi na usalama.
3.4 Makundi maalumu
Kila taifa lina walemavu na wnajamii wengi mbao wanahitaji uwezeshwaji wa ziada serikali itakayoongozwa na CHAUMMA itatekeleza sera zifuatazo kuhusu makundi haya maalumu.

Walemavu
 • Itatoa na nafasi maalum katika mabaraza ya uwakilishi kwa ajili ya walemavu
 • Itatunga sharia za kusimamia maslahi ya walemavu katika huduma za umma na kuwawezesha kufanya shuhuli za kujipatia kipato
Yatima na watoto walio katika mazingira magumu
 • Itakabiliana na chimbuko la watoto yatima na watoto walio katika mazingira magumu
 • Itatoa ruzuku kwa asasi zisizo za kiserekali zinazohudumia watoto yatima na watoto walio katika mazingira magumu
Makabila yalio katika hatari ya kutoeka
 • Itashirikiana na asasi zisizo za kiserekali kuainisha na kukabiliana na hali inayotishia uwepo wa makabila hayo.
3.5 Vyombo vya habari na asasi zisizo za kiserikali
Sera za CHAUMMA kuhusu vyombo vya habari na taasisi zisizo za kiserekali zinatoa kipao mbele maalumu kwa taasisi hizi kwa kuwa zimekuwa zikitoa mchango mkubwa sana katika kidemokrasia nchini na maendeleo ya kijamii kwa ujumla. Ili kuviwezesha vyombo vya habarina na asasi zisizo za kiserekali kuwa huru na kufanya kazi vizuri tumeshuhudia katika kipindi cha miaka mitano vyombo vya habari na asasi zisizo za kiserikali namna ambavyo vimepitia hatua ya ukandamizwaji na vitisho na hata baadhi ya waandishi au wanaharakati kutishiwa kuuwawa au kuuliwa,kuwekwa vizuizini na kufungwa jela ili kuwanyamazisha wasiendelee kuupasha umma maovu yanayofanywa na serikali, wananchi wamekosa fursa ya kupata habari kupitia bunge lao kwa njia ya Mubashara katika televisheni na redio jambo linalopelekea wananchi kukosa na kupima uwezo na uweledi wa wabunge waliochaguliwa, hali hiyo imedhoofisha nakuvunja katiba amabayo inatoa fursa kwa kila mtanzania anahaki ya kupata habari bila kufichwa.

kwa manufaa ya wananchi serekali itayoongozwa na CHAUMMA itatekeleza mambo yafuatayo:
 • Itatunga sheria za uhuru wa vyombo vya habari na haki ya vyombo hivyo kupata habari kutoka taasisi za umma na idara za serikali.
 • Itapunguza kodi kwa vyombo vya habari vitakavyotoa huduma vijijini nn kuendesha programu za elimu na maendeleo na pia kupunguza kodi za karatasi
 • Itapanua mafunzo ya uwandishi wa habari na utangazaji
 • Itarahisisha utaratibu wa usajili wa asasi zisizo za kiserikali
3.6 Usawa wa jinsia
Ili kujenga usawa baina ya jinsia ya kiume na ya kike na kutokomeza maonevu ya kihistoria na mila potofu zinazomdhalilishaa mwanamke, wanawake watapewa nafasi na fursa maalumu ili kurekebisha athari za maonevu walioyapata katika historia kama ifuatavyo:
 • Kuwezesha matumizi ya vifaa vya kisasa majumbani ili kiwe rahisi kwa jinsia zote kushiriki katika kazi za kuhudumia familia.
 • Kuw na idadi ilio sawa ya wanaume na wanawake katika vyombo vya uwakilishi na kupanua mfumo wa uwakilishi wa uwiano.
 • Kuridhia na kutekeleza mikataba yote ya umoja wa mataifa, umoja wa afrika na jumuiya za umoja wa kusini mwa afrika kwa manufaa ya watanzania ili kujenga jamii yenye kutamalaki Haki za binadamu na yenye kufurahia usawa kati ya wanaume na wanawake
 • Uwepo wa wanawake katika ngazi mbali mbali muhimu za uwongozi wa nchi kama ifuatavyo
 • Kuweko kwa kiongozi mwanamke miomgoni mwa viongozi wakuu wa serikali wa nchi yetu pamoja na raisi, makamo wa raisi na waziri mkuu wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania.
 • Kuwa na spika makini wa bunge au Baraza la wawakilishi asiyekuwa na utashi wakujipendekeza na kujikomba mbele ya Serikali, spika mwenye sifa na weledi wa kusimamia na kuongoza vikao vya bunge/baraza la wakilishi kwa kuzingatia vigezo vya kitaifa na kimataifa.
 • Kuzingatia usawa wa jinsia katika nafasi mbalimbali za kiutaalamu kama vile mawaziri, wakuu wa mikoa na wialaya, mabalozi, makatibu wakuu wa wizara, makamishna, makatubu tawala wa mikoa na wilaya na wilaya na wenye viti na wajumbe wa bodi ya mashrikia ya umma.
MWITO KWA WANANCHI
Katika uchaguzi huu tayari tumeshuhudia matumizi makubwa ya fedha kununua wapiga kura yanayofanywa na wagombea wa chama tawala. Hii ni pamoja na kuwa sheria ya kudhibiti matumizi ya fedha katika uchaguzi,na hivyo TAKUKURU/ZAECA kuhamasishwa vichukue hatua kali kwa wahalifu wa sharia za uchaguzi.

Wengi wetu watakuwa wamesoma na kuona katika vyombo vya habari vya serikali matangazo ya kuwasifu na kuwapongeza wagombea wa chama kilichopo madarakani. Haya ni matumizi mabaya ya taasisi hizo kwa manufaa ya chama kimoja dhidi ya vyama vyengine vya siasa, ni uvunjaji wa sharia za uchaguzi, na vitendo hivyo haviweki uwanja sawa kwa wote.

Watanzainia wameona jinisi miaka mitano ilivopita ilivyogeuka kuwa miaka ya kero, mateso na ufukara. Waliahidiwa maisha bora kwa wote na wameshuhudia maisha bora kwa viongozi wa serikali na dhiki kwa walio wengi, sifa ya kiongozi nilazima awe mtetezi wa Haki umma hautaki kuona mgombea Uraisi atae fumbia macho uvunjaji wa haki za binadamu kama walivyofanyiwa wananchi wa Zanzibar katika uchaguzi mkuu wa 2015.

Raisi wetu awe mtetezi wa Haki za binadamu atakaye ongoza kwa katiba sheria na Haki awe mtetezi wa wanyonge asiwe mbaguzi wa vyama vya siasa,aepukane ukabila,dini na kuwaunganisha umma wote bila kujali itikadi za chama

Awe na uwezo wa kupambana na umaskini kuongoza kwa uwadilifu na asiwe na upendeleo,chuki,ufisadi na asitumie vyombo vya ulinzi na usalama kubaki madalakani endapo umma wa watanzania umekataa kumchagua,lazima aheshimu matakwa ya umma na astumie mihimili ya dola kuamuru ili kupata haki kinyume cha matakwa ya umma.

Tusifanye makosa kuwachagua viongozi wa aina hiyo ambao wana ng’ang’ania kubaki madarakani kwa kutumia nguvu,wizi wa kura na kuteka kimabavu uhuru wa tume za uchaguzi.. Tuwe jasiri na kuthubutu kuwapigia kura wana CHAUMMA,tujipe moyo na tuwe na ujasiri wa kuliokoa Taifa letu katika kipindi hiki kigumu achacho uchumi umedhoofishwa na kukandamizwa.

Lazima tukubali mabadiliko Dunia inakwenda kwa mabadiliko wakati hautusubiri,nchi nyingi za Afrika zimethubutu kuviondoa vyama vingi vikongwe vizilivyodumu Madarakani,vyama ambavyo vimejijengea taswira ya kurithishana madaraka kwa Koo(Masultan wa Africa) mfumo huo wa kibeberu na kisultani lazima tuukatae kwa njia ya uchaguzi ili CHAUMMA iweze kujenga Tanzania yenye Mabadiliko ya kisiasa,Kiuchumi na Kitamaduni.

Nidhahiri kuwa chama kilichopo madarakani kinahitaji mapumziko ili kutoa nafasi kwa wagombea wa Chama Cha Ukombozi wa Umma kuleta mabadiliko fursa za kiuchumi na kisiasa na kuliletea taifa Haki.

Tukubali kubadilika, tuchague Chama Cha Ukombozi Umma walioletwa kwenu na CHAUMMA ili tupate fursa ya kulitendea taifa haki. Tupeni kura zote na sisi tutawapa uwezo wetu nguvu zetu na maarifa yetu ili tufike katika Tanzania inayopendeza.

Tunaomba kura zenu bila kujali dini kabila, chama au rangi kura yako inathamni ya kheri, amani na matumaini kwa miaka mitano. kupiga kura watawala wa sasa ni kutufunga minyororo ya umasikini, tabu na kero kwa miaka mengine mitano. Sisi tunaahdi kutekeleza hoja na matakwa yenu kwa uaminifu na kwa umakini kama yalivoainishwa katika ilani hii.

CHAUMMA! NGUVU YA UKOMBOZI!

Mungu ibariki Tanzania Bara!

Mungu ibariki Zanzibar!
 

Attachments

 • ILANI YA CHAUMMA.pdf
  505.1 KB · Views: 15

Louis II

JF-Expert Member
Mar 9, 2018
3,028
2,000
CCM walitakiwa wawe na ilani imara kama hii kuliko kukumbatia mandege na Mabarabara tu!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom