Uchaguzi 2020 Ilani ya CHADEMA ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani 2020 - 2025

Sera za CHADEMA ni nzuri sana!

CHADEMA hawaaamini maendeleo ya "vitu" Kama barabara, madaraja, ndege, miradi ya kuzalisha umeme, kusambaza umeme wa REA na ujenzi wa hospitali.

CHADEMA ni chama kubwa inaamini maendeleo ya watu kama; kuongea vizuri kiingereza, kuvaa barakoa kama wazungu, haki ya mapenzi ya jinsia moja, kufanya maandamano nk.

Kipi ni chama "garasa"? Majibu unayo
 
Huna ishu, yaani umeshiba nguna ya ndondo ndio ukapata mzuka wa kuandika huu utopolo!?
20200912_081929.jpg
wenzako wamesombwa wapo kwenye mkutano kumpunguzia lissu aibu
 
Sera za CHADEMA ni nzuri sana!

CHADEMA hawaaamini maendeleo ya "vitu" Kama barabara, madaraja, ndege, miradi ya kuzalisha umeme, kusambaza umeme wa REA na ujenzi wa hospitali.

CHADEMA ni chama kubwa inaamini maendeleo ya watu kama; kuongea vizuri kiingereza, kuvaa barakoa kama wazungu, haki ya mapenzi ya jinsia moja, kufanya maandamano nk.

Kipi ni chama "garasa"? Majibu unayo
Ccm
 
Screenshot_20200912-220254_Chrome.jpg

Katika jambo ambalo lilitia moto kwenye moyo wangu ni Magufuli kuongeza makato kutoka 8% mpaka 15%. Watu walibaki weupe hawajui wafanyaje.

Hatimaye pele limepata mkunaji. Mnataka nini tena zaidi ya sera hizi za kujali maisha ya watu
 
CCM imetukata 15% kibabe bila huruma hasa ukizingatia hatujapandishiwa mshahara miaka 5 mfululizo.
 
Naomba nikiri sijafanikiwa kupata Ilani ya CHADEMA ya Uchaguzi Mkuu, 2020. Hivyo basi naelea katika maamuzi.

Nafuatilia hotuba za mgombea Urais ili niweze kufanya uamuzi sahihi (informed decision) tarehe 28/10/2020. Hadi sasa nilichoambulia sijui ni Sera au Kaulimbiu kwamba Uhuru, Haki na maendeleo.

Kwa kuwa maendeleo ni pamoja na kukua kwa uchumi, mwenye kujua ni kwa vipi CHAFEMA imejipanga kukuza uchumi wa Taifa na hatimaye wa mtu mmoja mmoja, asaidie kunielewesha.
 
Naomba nikiri sijafanikiwa kupata Ilani ya CHADEMA ya Uchaguzi Mkuu, 2020. Hivyo basi naelea katika maamuzi.

Nafuatilia hotuba za mgombea Urais ili niweze kufanya uamuzi sahihi (informed decision) tarehe 28/10/2020. Hadi sasa nilichoambulia sijui ni Sera au Kaulimbiu kwamba Uhuru, Haki na maendeleo.

Kwa kuwa maendeleo ni pamoja na kukua kwa uchumi, mwenye kujua ni kwa vipi CHAFEMA imejipanga kukuza uchumi wa Taifa na hatimaye wa mtu mmoja mmoja, asaidie kunielewesha.
Mimi nitaipigia kura hii ilani maana imejaa kila kitu,hata ikisimamishwa ilani na binadamu nitaipigia ilani,yaani kura yangu kwa chadema sababu ya ilani tuu
 
hakuna kitu kinaniumiza kama hiki cha mafao ya watumishi..
serikale ya CCM yenyewe imeamua kufuta FAO LA KUJITOA ili ukiacha kazi hata kama unamiaka 20 itabidi usubirie mpaka ufikie miaka 60 ndio uombe upewe sasa sijui kama CCM wanauhakika utaweza kuishi na kufikisha umri huo.
nawapongeza CHADEMA kwa kuja na mpango huu wa kuwakomboa wafanyakazi kwa kuwasaidia pindi wanapoacha kazi au kusitishwa ajira zao.
 
hakuna kitu kinaniumiza kama hiki cha mafao ya watumishi..
serikale ya CCM yenyewe imeamua kufuta FAO LA KUJITOA ili k=ukiacha kazi hata kama unamiaka 20 itabidi usubirie mpaka ufikie miaka 60 ndio uombe upewe sasa siui kama CCM wanauhakika utaweza kuishi na kufikisha umri huo.
nawapongeza CHADEMA kwa kuja na mpango huu wa kuwakomboa wafanyakazi kwa kuwasaidia pindi wanapoacha kazi au kusitishwa ajira zao.
Chadema hawajalizungumza kwa sauti ya juu
 
MAMBO YA SIKU 100 ZA KWANZA Ndani ya siku 100

tangu siku ya kuapishwa kwa Rais na Wabunge, watakaokuwa wamechaguliwa, Serikali ya Chadema itafanya taratibu zinazohusika ili kuhakikisha yafuatayo yanatendeka: i)
Serikali itapeleka Bungeni Muswada wa Sheria ya Maridhiano, ambayo pamoja na mambo mengine itaanzisha Tume ya Maridhiano kwa lengo la kuondoa hofu ya uwezekano wa vitendo vya kulipiza visasi na kuunganisha nguvu za wananchi wote bila ubaguzi wa vyama katika kuongoza Taifa letu.

ii) Serikali itapeleka Bungeni Muswada wa Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi juu ya Utoaji wa Elimu Bure kuanzia elimu ya awali hadi Sekondari.

iii) Serikali itapunguza kiwango cha marejesho ya mikopo ya elimu ya juu hadi kufikia asilimia tatu (3) ya mshahara wa mnufaika na kutanua wigo wa muda wa marejesho hadi kufikia miaka 25 tangu mnufaika apate ajira. Aidha, Serikali itafuta riba na tozo zote zitokanazo na adhabu ya kuchelewesha marejesho ya mkopo wa elimu ya juu.

iv) Serikali itashirikiana na sekta binafsi kuweka utaratibu wa kutoa huduma za afya ya msingi kwa wananchi bila malipo.

v) Serikali itarejesha mchakato wa Katiba Mpya kuanzia ilipoishia Rasimu ya Tume ya Marekebisho ya Katiba ya Jaji Warioba

vi) Serikali ya Chadema itatekeleza matakwa ya Katiba kuhusu Tume ya Pamoja ya Fedha ya Muungano ili kila nchi Mshirika wa Muungano ipate mgao wake wa fedha kwa mujibu wa Katiba na sheria.

vii) Serikali ya Chadema itarejesha uhuru wa vyombo vya habari ikiwa ni pamoja na kuruhusu vyombo hivyo kurusha moja kwa moja vikao vya Kamati za Bunge, Mikutano ya Bunge na Mwenendo wa Uendeshaji wa Mashauri Mahakamani.

viii) Serikali ya Chadema itapeleka miswada ya Sheria Bungeni kwa madhumuni ya kuzifuta Sheria zote kandamizi na zinazokiuka misingi ya haki za binadamu.

ix) Kuanzisha utaratibu wa mazungumzo kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Zanzibar kwa lengo la kufikia muafaka juu ya utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi, uvuvi wa bahari kuu na usajili wa meli.

x) Serikali ya Chadema itaandaa mazingira rafiki na wezeshi kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari walioshindwa kuendelea na masomo kwa sababu mbalimbali kama vile ugonjwa, kukosa ada, mimba n.k. kurejea kwenye mfumo rasmi wa elimu na kumalizia masomo yao.

xi) Serikali ya Chadema itapeleka bajeti ya Nyongeza Bungeni katika mwaka wa fedha 2020/2021 kwa ajili ya kuongeza Mishahara ya watumishi wote wa umma, kulipa malimbikizo; sambamba na kuwapandisha madaraja watumishi wenye sifa na kulipa mishahara inayoendana na madaraja yao.

xii) Serikali ya Chadema itaanzisha bima maalum ya afya kwa watumishi wote wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wawapo kazini na baada ya kustaafu vikiwemo Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Polisi, Magereza, Uhamiaji, Zima moto na Uokoaji.

xiii) Serikali ya Chadema itarejesha maduka yasiyotozwa kodi (Duty free shops) katika vyombo vya ulinzi na usalama vikiwemo Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Polisi, Magereza, Uhamiaji, Zimamoto na Uokoaji.

xiv) Serikali itapeleka Bungeni Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Hifadhi ya Jamii ili kurekebisha kikokotoo cha UHURU, HAKI NA MAENDELEO YA WATU 10 Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kwa wastaafu ili kiendane na mahitaji ya wastaafu. Aidha, Serikali ya Chadema itaruhusu wafanyakazi na watumishi waliochangia katika mifuko ya jamii kuchukua mafao yao wakati wowote (fao la kujitoa).

xv) Serikali ya Chadema itaweka utaratibu na kuwatafutia masoko wakulima, wavuvi na wafugaji ya kuuza mazao yao ndani na nje ya nchi bila kizuizi. xvi) Kurejesha utaratibu wa awali wa ukusanyaji wa kodi, ushuru na tozo mbalimbali kwa mamlaka ya serikali za MITAA.
 
21 Reactions
Reply
Back
Top Bottom