Uchaguzi 2020 Ilani ya CHADEMA ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani 2020 - 2025

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
25,123
2,000
Chadema Ni certified conmen balozi zote za nje zulisubiri siku ya uzinduzi wa kampeni mbagala kujua sera zao Nini wskijua siku hiyo ndio watazindua wengi walitoka ulaya na Marekani wakaweka kambi mahotelini wakilipa wakalimani per minute kuwatafusiria kwa pound 50 kwa dakika sawa na shilingi Kama laki tatu kwa dakika chadema hawakutoa ilani.

They were so disappointed ikabidi waondoke sababu walipewa time frame to cover only that event Mimi nilikuwa mmoja wa waliopata tenda ya kukalimani sera zitakazosemwa na Chadema.

Anyway Chadema walipoteza golden opportunity ile siku ya uzinduzi Mbagala balozi zote zilikuwa kwenye TV na wakalimani waKusibiri Chadema waseme kilichomo kwenye ilani.
 
Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,462
2,000
WanaJF

Wakati nchi nzima ikizizima na kumuunga mkono mgombea Urais wa Chadema Tundu Lissu kutokana na kauli Mbiu ya Uhuru,Haki na Maendeleo ya watu tayari Ilani ya uchaguzi ya Chama hicho imekuwa gumzo kila mahali.

-----------------------------------

BAADHI YA TOFAUTI YA ILANI YA UCHAGUZI YA CCM NA CHADEMA MWAKA 2020

1.Ilani ya CCM haizungumzii kupunguza Kodi wakati ilani ya CDM inalenga kupunguza Kodi ya ongezeko la thamani ili iendane na nchi jirani na kuondoa utitiri wa kodi (multiple taxation)

2. Ilani ya CCM haizungumzii kuongeza mishahara wala kufidia nyongeza ambazo watumishi walipunjwa miaka mitano iliyopita wakati CDM inategemea kuleta bajeti za ziada kufidia nyongeza mishahara ya miaka mitano ambayo watumishi hawakupata nyongeza ya mishahara wala kupanda madaraja.

3. Ilani CCM haizungumzii kupunguza marejesho ya mikopo ya elimu ya juu(HELSB) wakati CDM inategemea kuweka marejesho ya asulimia 3 kwa wahitimu wa vyuo vikuu badala ya asilimia 15 ya Sasa ambayo iliongezwa kinyume na mkataba wa mkopo kwa kufanya marekebisho ya sheria ya Sasa na kwamba mhitimu alipe baada ya kupata kazi.

4.Ilani ya CCM haizungumzii agenda ya Katiba Mpya wakati ile ya CDM inazungumzia kurudisha mchakato wa katiba mpya ulioasisiwa na jaji Warioba ndani ya siku mia za Kwanza.

5. CCM inaamini kwenye maendeleo ya vitu wakati CDM inaamini katika maendeleo ya watu zaidi. Yaani maisha yawatu ndio yawe bora zaidi badala ya vitu Kama ndege.

6. Ilani ya CCM haizungumzii kulinda uhuru wa habari Kama kipau mbele wakati ilani ya CDM inaweka kipaumbele mojawapo ni kurejesha Uhuru wa habari.

7. Ilani ya CCM haizungumzii kugatua madaraka na kufanya wananchi wawe na nguvu zaidi ya kuamua mambo yao wakati ilani ya CDM inapendekeza kupeleka nguvu zaidi kwa wananchi.

8. Ilani ya CCM haitoi mkazo wa uchumi kumilikiwa na sekta binafsi( wananchi) bali serikali wakati ilani ya CDM inaweka kipaumbele uchumi wa watu( sekta binafsi)

9. Ilani ya CCM haizungumzii bima ya afya kwa watu wote wakati ilani ya CDM inataka watu wote wawe na bima ya afya.

10. Ilani ya CCM inazungumzia kudumisha Muungano was serikali mbili wakati Ilani ya CDM inazungumzia Muungano wa serikali tatu zilizopendekezwa na wananchi kwenye tume ya Jaji Warioba.

11. Ilani ya CCM haizungumzii kuondoa Kodi kwenye maduka ya majeshi ya Polisi, jeshi la wananchi, magereza na Zimamoto Kama hapo awali ili kuwapa wanajeshi unafuu wa maisha wakati CDM inapendekeza kurejesha unafuu huo.

12. Ilani ya CCM haizungumzii marudhiano ya kitaifa wakati ilani ya CDM inapendekeza kuleta maridhiano ya kitaifa ndani ya siku mia za Kwanza.

13. Ilani ya CCM haizungumzii kufuta sheria kandamizi wakati ilani ya CDM inapendekeza kufuta sheria zote kandamizi.
---------------------------------------

Ifuatavyo ndiyo ILANI ya Chadema 2020 - 2025
 
Attachments

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
34,289
2,000
WanaJF

Wakati nchi nzima ikizizima na kumuunga mkono mgombea Urais wa Chadema Tundu Lissu kutokana na kauli Mbiu ya Uhuru,Haki na Maendeleo ya watu tayari Ilani ya uchaguzi ya Chama hicho imekuwa gumzo kila mahali.

Ifuatavyo ndiyo ILANI ya Chadema 2020 - 2025
Ngoja niipitie nitarejea.....kwa mbali naona inafanana na ya Nccr mageuzi!
 
MOTOCHINI

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
25,815
2,000
WanaJF

Wakati nchi nzima ikizizima na kumuunga mkono mgombea Urais wa Chadema Tundu Lissu kutokana na kauli Mbiu ya Uhuru,Haki na Maendeleo ya watu tayari Ilani ya uchaguzi ya Chama hicho imekuwa gumzo kila mahali.

Ifuatavyo ndiyo ILANI ya Chadema 2020 - 2025
Nchi nzima ikizizima
Hivi aliye waroga alikufa na Dawa yake au!!
Poleni sana
 
Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
15,654
2,000
Ilani hii inaifanya nchi kuwa ombaomba
WanaJF

Wakati nchi nzima ikizizima na kumuunga mkono mgombea Urais wa Chadema Tundu Lissu kutokana na kauli Mbiu ya Uhuru,Haki na Maendeleo ya watu tayari Ilani ya uchaguzi ya Chama hicho imekuwa gumzo kila mahali.

Ifuatavyo ndiyo ILANI ya Chadema 2020 - 2025
 
Savimbi Jr

JF-Expert Member
Sep 23, 2011
6,754
2,000
WanaJF

Wakati nchi nzima ikizizima na kumuunga mkono mgombea Urais wa Chadema Tundu Lissu kutokana na kauli Mbiu ya Uhuru,Haki na Maendeleo ya watu tayari Ilani ya uchaguzi ya Chama hicho imekuwa gumzo kila mahali.

Ifuatavyo ndiyo ILANI ya Chadema 2020 - 2025
Ilani KONKI sana hii.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom