Ilani ya CHADEMA Uchaguzi wa mwaka huu itakuwa na mambo gani?

BUSH BIN LADEN

JF-Expert Member
Mar 16, 2019
7,465
16,752
Ni matumaini yangu hamjambo na mnaendelea na shughuli za kila siku za ujenzi wa Taifa.

Wakuu nimeamua kuja na huu uzi ili tujaribu kushirikishana ni mambo yepi tunahisi/kudhani yanaweza kuwa kwenye ilani ya Uchaguzi ya chama kikuu cha upinzani nchini CHADEMA.

Kama tunavyojua kila chama kinapaswa kuwa na ilani (document) inayosimama kama ahadi ya chama kwa wananchi juu ya nini na yapi kitawafanyia wananchi endapo kitapewa ridhaa ya kuongoza Serikali.

Mwaka 2015 walikuja na ahadi nyingi kubwa kati ya hizo ilikua

1: Uboreshaji wa miundombinu

2: Kuboresha elimu ikiwa pamoja na kutoa elimu bure

3: Kuboresha huduma za afya

4: Kuboresha huduma za nishati ikiwa pamoja na kuanzisha vyanzo vipya vya nishati

5: Kuboresha usafiri ikiwa pamoja na kufufua shirika la ndege nchini, kuboresha usafiri wa majini, reli nk

Ahadi ndani ya ilani yao zilikuwa nyingi ambazo siwezi kuziorodhesha zote hapa.
Kilichonifanya nije na huu uzi ni kutaka kujua mwaka huu watatuahidi nini ikiwa waliyoyaahidi mengi yanafanywa/yamefanywa na mshindi wa uchaguzi wa mwaka 2015 ila chakushangaza Chadema wamekuwa wakipinga na kubeza haya yote yanayofanywa na rais Magufuli.

Wamepinga elimu kutolewa bure, ununuzi wa ndege, ujenzi wa reli mpya, ujenzi wa bwawa la kuzalisha umeme na karibu yote anayoyafanya pamoja na kwamba mengi ya anayoyafanya wao pia waliahidi kuwa wangeyafanya tungewapa ridhaa.

-Leo utatwambia utaboresha miundombinu wakati kuna anaefanya na mna mbeza?
-Utaahidi kuboresha upatikanaji wa nishati ya uhakika wakati kuna anaefanya na mnambeza
- Utalinda vipi rasrimali zetu wakati kuna anaefanya tayari na mnambeza na kumpinga?

Kwa haraka haraka unaweza kusema ndani ya ilani yao kutakuwa na ahadi mfano ya kuboresha utawala bora, haki za binadamu na kukuza demokrasia lakini hatuwezi kukuchagua ili ufanye mambo matatu tu kwa miaka 5 ni kituhadaa.

Hawa jamaa watakuja na ahadi ya kutufanyia nini tukiwapa ridhaa ya kutuongoza, naomba tufikiri pamoja.

Naomba kuwasilisha.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom