Ilani ya CCM ni kitanzi cha watendaji wengi serikalini na mashirika ya Umma kutekeleza ahadi zote

Intelligence Justice

JF-Expert Member
Oct 23, 2020
3,036
3,479
Wakuu,

Huu ni mtazamo kwa yaliyomo kwenye Ilani ya CCM kwa kuzingatia yafuatayo

A:
1. Rasirimali asili
2. Rasirimali Watu
3. Rasirimali Vifaa na Teknolojia

B:
1. Elimu, Ujuzi, Weledi na Taaluma
2. Ubunifu, Bidii ya kazi na kujitoa kwa manufaa ya jamii
3. Uadilifu, Nidhamu na Uaminifu

C:
1. Kusikiliza kero, kuondoa manung'uniko ya wanananchi wa ngazi zote, kuchukua ushauri ujenzi na kutambua na kuthamini juhudi za wazalishaji mali au uendeshaji huduma
2. Kuchukua hatua dhidi ya ufisadi, ubadhirifu,, wizi, udanganyifu na unyanyasaji
3. Kutoa haki dhidi ya dhuluma na kuadhibu wakosaji kwa adhabu stahiki

D:
1. Uongozi bora na wenye tija
2. Utawala wa sheria
3. Kutambua, kuboresha na kujali maslahi bora ya kila mtu anayefanya shughuli halali za ama kuajiriwa au kujiari

Kuanzia Januari 21, 2021 yafuatayo yatajitokeza

1. Viongozi kadhaa wa serikali na mashirika ya Umma watashindwa kutimiza majukumu yao ya msingi kwa kutanguliza kutibu majeraha ya nafsi zao na familia zao ndipo nafasi zao zitatenguliwa na mamlaka husika.

2. Viongozi kadhaa pamoja na baadhi ya wafanya biashara maarufu kukabiliwa na kesi za uhujumu uchumi na njama ovu dhidi ya viongozi wanaosimamia maadili.

3. Bodi za makampuni binafsi hazitazingatia mwongozo huo hapo juu ndipo uvumilivu wa nguvu kazi utakapokwisha na migogoro mikubwa kuibuka ambao utapelekea kesi nyingi kufunguliwa kwa madai ambayo wengi wao watashindwa kuyalipa hivyo kuamua kufunga biashara au kutangaza kufilisika.

Mtazamo uko mezani mbele za nguli wa fikra kutafakari matokeo na athari zake kwa kushauri mbinu mtambuka kuepuka kutumbukia kwenye mtego huo.
 
Waheshimiwa Mawaziri Nendeni Mkafanye kazi hata Mnakosea, Kuliko Kuacha Kuamua Eti Mtakosea!!
Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania

** Kazi Ipo Kubwa **
 
Kila mtu anaogopa kukosea aje atumbuliwe,karibu zinatimia siku 100 kuna mawaziri hata hawajatia neno!

Ni kama wanasubiri maelekezo vile.
 
Sitegemei jipya zaidi ya uwajibikaji wa hofu, maigizo na propaganda. Utawala ulioingia madarakani kwa wizi wa kura na umwagaji damu, una nafasi ndogo sana ya kuwajibika kwa umma, kwani hauna ridhaa ya umma. Sitegemei uadilifu wowote kwa watu walioko madarakani kwa shuruti, sana sana tutashuhudia utawala wa mabavu, kukomoa wenye mitazamo mbadala, kutaka kusujudiwa, hila, hadaa na ghiliba za wazi.
 
CCM ishapigwa kitanzi siku nyingi. Ndiyo maana uchaguzi mkuu wa 2020 ilipigwa kumbo na wananchi, dola ikaingilia Kati.
 
Back
Top Bottom